Uongozi wa klabu ya FC Barcelona upo mbioni kumuongeza mkataba wa miaka miwili nahodha wa timu ya taifa ya Brazil na mshambuliaji wa klabu hiyo Neymar utakaomalizika mwaka 2018. Mkataba wa sasa wa Neymar unataraji kuisha mwaka 2018 ila kiwango kizuri alichokionyesha Mbrazil huyo kimewashawishi viongozi hao kutaka kumsainisha mkataba mpya ili kumzuia asijiunge na klabu nyengine. Neymar amefanikiwa kuunda mahusiano mazuri na nahodha wa timu ya taifa ya Argentina na mshambuliaji hatari duniani Lionel Messi pamoja na Luis Suarez....
Klabu ya soka ya Chelsea imefanikiwa kupata ushindi wa magoli mawili kwa sifuri dhidi ya Stoke City na kujihakikishia nafasi ya kwanza kuelekea katika msimu wa sikukuu ya Christmas. Magoli ya Chelsea yamefungwa na beki na nahodha wa klabu hiyo John Terry huku kiungo wa Kihispania Cesc Fabregas akifunga goli la pili la mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Brittania. Chelsea imefikisha alama 42 ikiwa ni 5 dhidi ya klabu ya Manchester City inayoshika nafasi ya pili huku historia ikionyesha...
Zari Hassan mkali kutoka Uganda hatimae amefunguka kuhusiana na tuhuma iliyokuwa ikimkabili kuwa amevujisha picha za makalio yake akiwa kitandani kwenye mitandao ya kijamii kwa kusema kwamba si yeye aliekuwa kwenye picha hizo na anawapa pole wote waliomfikiria vibaya Takribani siku kadhaa nyuma picha zilizoonyesha makalio zilivuja kwenye mtandao huku ikidaiwa kuwa Zari ndie mwenye picha hizo na Diamond ndie alimpiga picha hiyo wakati yupo nae kitandani siku moja kabla ya party ya Zari iliyofnyika Guvnor Dec. 18. Kupitia...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya leo, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Jacob Zuma. Mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, yalichukua kiasi cha saa moja na dakika 45 na yalihusu uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Rais Zuma ambaye aliwasili nchini usiku wa jana, Jumapili, Desemba 21, 2014, ameondoka nchini mara baada ya kumalizika mazungumzo hayo. ...
PAKISTAN imewanyonga wapiganaji Wanne wenye Itikadi Kali za Kiislamu, baada ya kuondolewa marufuku ya kutolewa adhabu ya kifo katika kesi zinazohusiana na ugaidi. Watu hao ni kundi la pili la watu walionyongwa tangu kundi la Taliban lilipofanya mashambulizi na kuwaua zaidi ya watu 140, wengi wao wakiwa watoto kwenye shule moja ya jeshi mjini...
MGOMBEA WA URAIS nchini Tunisia, anayepinga Itikadi Kali za Kiislamu, BEJI CAID ESSEBSI, amejitangazia ushindi mkubwa katika uchaguzi wa kwanza huru. Hata hivyo, mpinzani wake, Rais aliyeko madarakani, MONCEF MARZOUKI, amepuuza madai hayo akisema hayana msingi na amekataa kukubali kuwa ameshindwa. Wananchi wa Tunisia wamepiga kura katika awamu ya Pili, huku wengi wao wakiuita uchaguzi huo kama uchaguzi wa Kihistoria wa Demokrasia katika nchi hiyo ambapo vuguvugu la mageuzi katika nchi za Kiarabu limeanzishwa....
WAZIRI wa Fedha Mheshimiwa SAADA MKUYA amewataka Watendaji wa Sekta ya Bima Nchini kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu yao kwa Wahanga wa ajali za Barabrani ambao wanazidi kuongezeka hivyo kuhitaji huduma ya haraka ya Kibima kutoka kwao. Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mheshimiwa MKUYA amesema kumekuwa na ongezeko la ajali za barabarani ambazo zinazotokea kila sehemu jambo linalopelekea kupoteza Taifa la kesho ikiwa ni pamoja na watu kupata Ulemavu wa maisha kutokana na ajali hizo....
MAKAMU wa Rais Dokta MUHAMMED GHARIB BILALI amewataka Wataalamu wa Sheria katika taasisi ya mafunzo ya Sheria kwa vitendo nchini kusaidia kutoa huduma za msaada wa Kisheria kwa Watanzania wa hali ya chini wasioweza kumudu gharama za huduma hiyo ili kuongeza chachu ya haki kutendeka. Dokta BILAL ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Sheria kwa vitendo ambapo amewataka wahitimu wa taasisi hiyo kuutumia Weledi wao katika kusimamia haki nchini...
Rais wa Marekani BARACK OBAMA amesema Serikali yake inatafakari kuiorodhesha upya Korea Kaskazini kama taifa linalofadhili ugaidi. Hatua imekuja kufuatia uingiliaji wa Mtandao wa Kampuni ya Filamu ya Sony, hatua iliyoilaazimu kufuta uzinduzi wa filamu yake inayoonyesha mauaji ya kutungwa ya kiongozi ya Korea Kaskazini KIM JONG UN. Maafisa mjini Pyongyang wamekanusha kufanya mashambulizi hilo la...
WAGOMBEA URAIS nchini Tunisia wamebishana juu ya matokeo ya uchaguzi wa Duru ya pili uliyofanyika hapo Desember 21 mwaka huu. Mwanasiasa wa muda mrefu BEJI CAID ESSEBSI amedai kushinda, lakini mpinzani wake, ambaye ni Rais wa sasa MONCEF MARZOUKI amekataa kukubali kushindwa. Matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa hii leo, huku Bwana ESSEBSI mwenye umri wa miaka 88 anaaminika kushinda asilimia 54 ya kura, akiwa mbele ya Bwana MARZOUKI kwa asilimia...