NCHI zenye nguvu duniani zinakutana mjini Vienna, Austria leo kujadili kupanuka kwa shughhuli za kundi la wanamgambo wenye itikadi kali la Dola la Kiislamu IS nchini Libya. Mkutano huo unaongozwa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Italia Paoli Gentiloni. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani John Kiry amesema mkutano huo wa Vienna utajadili uungwaji mkono wa serikali ya Umoja wa kitaifa ya Libya na jumuiya ya kimataifa kwa...
MAMLAKA ya chakula na dawa-TFDA imekutana na adau mbalimbali wa usalama wa chakula na dawa kutoka nchi 12 za bara la Africa ikiwemo Tanzania kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa kiutendaji kazi utakaochangia kutatua changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo. Akizungumza jijin dar es salaam, Mkurugenzi mkuu wa TFDA HIIT SILLO amesema kuwa kupitia mkutano huo wadau wataweza kuchambua ubora wa maabara zinazozingatia viwango vya upimaji vya vakula, dawa pamoja na viwango vya uchunguzi wa vyakula. Hata hivyo sillo ametoa...
KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina la Ramadhani Saidi mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa kijiji cha Manyinga Turiani Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro amenusurika kifo baada ya kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi wakati wakiwa doria usiku wa kuamkia leo. Mkuu wa upelelezi wilaya ya mvomero ASP Peter Majengo akizungumza na wananchi waliokusanyika katika hospitali hiyo amesema tukio hilo lilitokea usiku wakati askari wakiwa doria na walipomuona walimsimamisha kijana huyo na kumtilia shaka kuwa ni jambazi ndipo...
WAZIRI wa Mambo ya nje wa Marekani John Kerry amefanya mazungumzo na Mfalme Salman wa Saudi Arabia kuhusu mizozo ya Syria, Libya na Yemen, kabla ya mikutano ya kimataifa inayopangwa kuandaliwa wiki ijayo barani Ulaya kuhusu mizozo hiyo. Ziara ya Kerry, ambaye pia amefanya mazungumzo na mwanamrithi wa ufalme na naibu mwanamrithi wa ufalme na waziri wa mambo ya nje, inakuja katika wakati muhimu wa kuimarisha juhudi za kudhibiti mapigano na kuhimiza mazungumzo ya kisiasa katika nchi zote tatu ambazo...
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wanawake wamekuwa ni chanzo cha ufisadi nchini kutokana na kupokea zawadi zitokanazo na fedha za kifisadi. Makonda aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mnyamani Vingunguti Jijini Dar es Salaam jana katika mkutano wa kujadili namna ya kupata mikopo mbalimbali kutoka Benki ya Wananchi Dar es Salaam (DCB). Makonda amewaambia wanawake hao kuwa hata katika suala la usafi linaanzia na malezi ya usafi ya akina mama kwa watoto...
Watu 31 wameuawa kwa bomu la kujitoa muhanga nchini Yemen,shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Islamic state. Polisi wamethibitisha kutoka kwa shambulizi hilo katika ngome iliyoko kusini mwa nchi hiyo ya Mukalla. Vyanzo kutoka idara ya afya vinasema kuwa zaidi ya watu sita wamejeruhiwa katika shambulizi hilo. Maafisa wanasema kiongozi mmoja wa ulinzi na usalama alilengwa katika shambulizi la pili,ambapo aliponea chupuchupu, lakini walinzi wake wapatao sita waliuawa. Mashambulizi haya yanakuja pakiwa panafanyika mzungumzo ya...
Mahakama nchini Misri imewahukumu kwenda jela watu sita kwa tuhuma za kumpiga hadi kumuua raia wa Ufaransa katika kituo cha Polisi walikokuwa wamewekwa kizuizini. Eric Lang mwenye umri wa miaka 49 aliyekuwa mwalimu wa lugha aliwekwa kizuizini nchini Misri miaka mitatu iliyopita. Kwa mjibu wa upande wa mashitaka ni kwamba Lang aligombana na wenzake wakiwa rumande ambapo walianza kumshambulia hadi kumsababishia kifo chake. Hata hivyo Polisi wa Misri wamekuwa wakituhumiwa kuhusiaka na mauaji ya mwanafunzi raia wa Italia Giulio Regeni...
Polisi nchini Uingereza imethibitisha kuwa kitu kilichokuwa kinadhaniwa kuwa ni bomu kilichoonekana kwenye uwanja wa timu ya Manchester United wa Old Trafford hakikuwa bomu kama ilivyodhaniwa bali kilikuwa ni kifaa cha wanausalama cha mazoezi kwa ajili milipuko. Kifaa hicho kiliachwa na walinzi wa kampuni moja ya binafsi baada ya kufanya mazoezi yaliyowahusisha mbwa wenye kunusa vifaa na vitu vya kihalifu. Kutokana na kuonekana kwa kifaa hicho mechi kati ya Manchester United na Bournemouth iliahirishwa. Tayari kifaa hicho kimeshaharibiwa chini...
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linalosimamia wakimbizi UNHCR limeitaka serikali ya Kenya kubatilisha msimamo wake wa kutaka kuzifunga kambi mbili za wakimbizi ikiwemo ya Dadaab nchini humo. Awali siku ya Ijumaa iliyopita Serikali ya Kenya ilisema kwamba kambi hizo mbili zitafungwa kufuatia wasiwasi wa usalama na ukosefu wa fedha. Aidha imetoa tangazo kama hilo mapema, lakini wakati huu serikali imesema kuwa inazifunga kambi zake za wakimbizi katika kile kinachoonekana kama hatua ya kwanza ya kusitisha uhifadhi wa wakimbizi Laki...
MEYA wa jimbo aliyeongoza kampeni kali ya urais nchini Ufilipino, Rodrigo “Digong” Duterte ameshinda uchaguzi huo kufuatia kujitoa kwa wapinzani wake. Licha ya kwamba matokeo rasmi hayajatangazwa, mpinani wake mkuu Mar Roxas amekiri kushindwa baada ya kura zinazohesabiwa kudhihirisha Duterte anaongoza kwa kura nyingi. Mgombea huyo aliye na umri wa miaka 71 alizusha mzozo wakati wa kampeni kwa matamshi yake makali....
KATIKA kutekeleza agizo la serikali la kuwafikia wateja laki 4 ifikapo June mwaka 2016 Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (Dawasco) limesema linaendelea na zoezi la uunganishaji wa huduma ya Maji kwa wananchi wote wa jiji la Dar es salaam. Akizungumza na waandishi wa habari Afisa mtendaji mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja ameeleza kuwa kwenye awamu hii ya zoezi la uunganishaji wateja wapya shirika litagharamia gharama zote za maunganisho ambazo ni gharama za uunganishaji mabomba na vifaa...