Slider

VIONGOZI WA ULAYA WAUNGANA KUIKABILI URUSI
Global News

VIONGOZI wa Ulaya wamemaliza kikao chao mjini Brussels Ubelgiji, wakisema kwa sasa wameungana zaidi kuliko ilivyokuwa katika kuikabili Urusi. Viongozi hao wameonyesha kuwa vikwazo vya kiuchumi havitadhoofishwa licha ya matatizo ya kifedha yanayoikabili Urusi. Rais mpya wa Baraza la Ulaya, DONALD TUSK akifunga kikao cha viongozi wa EU amesema Urusi na vitendo vyake ni tatizo kubwa la kimkakati linaloikabili Ulaya....

Like
276
0
Friday, 19 December 2014
MAHIZA AMSHAURI MENGI KUWEKA PAMOJA WAFANYABIASHARA KATIKA SEKTA BINAFSI
Local News

 MKUU wa Mkoa wa Lindi MWANTUMU MAHIZA amemshauri Mwenyekiti wa Taasisi za Sekta Binafsi Tanzania-TPSF Dokta REGINALD MENGI kuwaweka pamoja Wafanyabiashara katika sekta binafsi ili waweze kupata fursa zaidi za kibiashara nje ya nchi. MAHIZA ameeleza hayo wakati akipokea shukrani kutoka kwa Dokta MENGI kutokana na kuliwakilisha vema Taifa nchini China. Amebainisha kuwa alipokuwa China pamoja na Ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka nchini pia amesaini mkataba kwa niaba ya Taasisi hiyo kwa lengo la kufanya biashara kati ya nchi hizo mbili....

Like
300
0
Friday, 19 December 2014
RAIS KIKWETE KULIHUTUBIA TAIFA LEO KUPITIA WAZEE
Local News

RAIS JAKAYA KIKWETE leo anatarajiwa kuhutubia Taifa kupitia Wazee wa Mkoa wa Dar es salaam. Katika Mkutano wake huo utakaofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Blue Pearl jijini Dar es salaam, pamoja na mambo mengine pia anatarajiwa kuzungumzia mwelekeo wa Taifa. Akizungumza na EFM Katibu wa Chama Cha Mapinduzi-CCM ABDALLAH MIHEWA amethibitisha kufanyika kwa mkutano huo....

Like
282
0
Friday, 19 December 2014
ERIC ABIDAL ATANGAZA KUSTAAFU SOKA
Slider

Beki wa Kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Olympiacos, Eric Abidal ametangaza kustaafu kucheza soka ikiwa ni takribani miaka kumi na nne toka aanze kucheza soka la kulipwa. Abidal alijiunga na klabu ya Olympiacos msimu huu na kusaini mkataba wa miaka miwili uliokuwa uishe msimu wa 205/2016 lakini ameamua kuuvunja kwasababu za kiafya. Beki huyo wa kushoto amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa toka mwaka 2011 na kumfanya akose michezo mingi akiwa na klabu ya FC Barcelona walioamua kumpa heshima...

Like
295
0
Friday, 19 December 2014
FA YAMUADHIBU BALLOTELI KUFUATIA VITENDO VYA UBAGUZI WA RANGI
Slider

Chama cha soka cha nchini England (FA) kimemuadhibu mshambuliaji wa klabu ya Liverpool, Mario Balloteli kwa kumfungia kutocheza mchezo mmoja wa ligi kuu nchini England na kumtaka alipe fidia ya kiasi cha paundi ishirini na tano elfu baada ya mchezaji huyo kukutwa na hatia ya vitendo vya ubaguzi. Hatua hiyo imefikiwa na chama hicho baada ya Muitaliano huyo kutuma ujumbe ulionyesha vitendo vya kibaguzi katika mtandao wa kijamii wa twitter kwa kuandika “ruka juu kama mtu mweusi ila tafuta fedha...

Like
328
0
Friday, 19 December 2014
SERIKALI YATANGAZA WANAFUNZI WATAKAOJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2015
Local News

WANAFUNZI 438,960 kati ya 451,392 waliofaulu katika mtihani wa darasa la saba wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2015 katika shule za sekondari za serikali Nchini. Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwa upande wa elimu KASSIM MAJALIWA alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema idadi hiyo ni sawa na asilimia 97.28 ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.8 ikilinganishwa na mwaka jana ambao ilikuwa ni asilimia 96.3. Mheshimiwa MAJALIWA amesema...

Like
430
0
Thursday, 18 December 2014
PRO. TIBAIJUKA: KAMWE SITAJIUZULU
Local News

WAZIRI wa Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi Mhe Profesa Anna Tibaijuka amesema kamwe hawezi kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow kwa kuwa hausiki na wizi wa fedha hizo na kusema kuwa kama akijiuzulu atakuwa hatendei haki dhana ya kuchakalika ili kuleta maendeleo. Akizungumza na Waandishi wa habari jijini dare s salaam Tibaijuka amesema kuwa fedha aliyoipokea ni mchango wa shule katika taasisi ya Shirika la JOHA TRUST wa shilingi Bilioni moja milioni mia 6 kumi na saba na laki...

Like
371
0
Thursday, 18 December 2014
SERIKALI YAPITISHA AZIMIO LA KINGA YA JAMII
Local News

SERIKALI ya Tanzania imepitisha Azimio linalohusu Kinga ya Jamii lenye msingi imara wa kusimamia masuala hayo nchini na Afrika kwa ujumla ili kuwa na maendeleo halisi kwa watu wake.   Azimio hilo limepitishwa na kusainiwa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum kwa niaba ya Serikali jijini Arusha wakati wa kufunga kongamano la kimataifa la siku tatu kuhusu Kinga ya Jamii ambalo limeshirikisha wajumbe kutoka nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika.   Akitoa hotuba ya kufunga kongamano hilo...

Like
259
0
Thursday, 18 December 2014
MAONYESHO YA KITAIFA YA ELIMU YAFUNGULIWA RASMI
Local News

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dokta Shukuru Kawambwa amesema kuwa Maonyesho ya Kitaifa ya Elimu –TIEE yatasaidia kuangalia namna ya kuisukuma ajenda ya elimu nchini.   Dokta Kawambwa ameyasema hayo leo wakati akifunguwa rasmi Maonyesho ya siku saba ya Elimu kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.   Maonyesho hayo ya siku saba yanayohusisha zaidi ya kampuni 80 za Elimu, Wadau, Taasisi na Walimu yamelenga kutengeneza jukwaa moja la kutoa taarifa za Elimu na Taasisi zake...

Like
251
0
Thursday, 18 December 2014
RAIS AMTEUA DK. MATARAGIO KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA TPDC
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Dokta James Mataragio kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania -TPDC.   Kulingana na, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue uteuzi huo ulianza tarehe 15 Desemba, 2014.   Dokta Mataragio ni Mtanzania ambaye hivi sasa anaishi na kufanya kazi nchini Marekani akiwa Senior Geoscientist wa Kampuni ya Bell Geospace, Houston, Marekani.   Aidha, Dokta Mataragio pia ni mmoja wa wataalam wa sekta ya madini, mafuta...

Like
312
0
Thursday, 18 December 2014
KUTANA NA MWANAUME ALIETUMIA $ 150,000 KUJIBADILI SURA AFANANE NA KIM KARDASHIAN
Entertanment

    Jordan James Parke mwenye umri wa miaka 23 huenda ndie shabiki mkubwa zaidi duniani wa mwanamitindo ambae ni drama queen Kim Kardashian mke wa rapa Kanye West   Jordan alipohojiwa kwenye gazeti la The Sun alidai kuwa amezama kimapenzi kwa msanii huyo baada ya kutazama kipindi cha Tv cha Kim kinachokwenda kwa jina la Keeping Up With The Kardashians alinukuliwa akisema ‘I love everything about Kim,’ ‘She’s the most gorgeous woman ever. Her skin is perfect, her hair,...

Like
496
0
Thursday, 18 December 2014