PAKISTAN imesema itaondoa marufuku ya kutolewa adhabu ya kifo katika kesi zinazohusiana na ugaidi. Ofisi ya Waziri Mkuu imetoa tangazo hilo leo, siku moja baada ya wapiganaji wa Taliban kuwaua watu 141 katika shambulizi lililofanyika kwenye shule moja inayoendeshwa na jeshi. Shambulizi hilo la kigaidi lililofanyika kwenye mji wa Peshawar, ni baya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Pakistan. Hukumu za kifo ziko katika amri za kitabu cha Pakistan na majaji wameendelea kutoa adhabu hiyo, lakini amri ya kusitisha adhabu...
RAIS Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone amesema kuwa msako wa nyumba kwa nyumba unaanza kote nchini humo kuwatambua watu walio na ugonjwa hatari wa ebola, na amepiga marufuku biashara kufanyika siku ya Jumapili. Katika hotuba yake aliyoitoa kupitia televisheni ya taifa, Rais Koroma ametoa amri ya kuzuia usafiri kutoka wilaya moja hadi nyingine. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni kutoka shirika la afya Duniani WHO, Sierra Leone ni taifa ambalo limeathirika kwa kiwango kikubwa na ugonjwa wa ebola...
KUFUATIA kujiuzulu kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema, Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA- kimemtaka Rais JAKAYA KIKWETE kuwawajibisha haraka viongozi wengine waliohusika katika sakata la Akaunti ya TEGETA ESCROW. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Naibu katibu mkuu wa chama hicho JOHN MNYIKA amesema Rais alipaswa kumuwajibisha kabla hajachukuwa uamuzi huo wa kujiuzulu hivyo amemtaka kuchukua hatuwa za haraka kuwawajibisha watuhumiwa waliobaki akiwemo Waziri wa Nishati na Madini...
OFISI ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa -TAMISEMI- imetoa maamuzi ya kutenguwa uteuzi, kuwasimamisha kazi, na kutoa onyo kali kwa wakurugenzi walioshindwa kutekeleza wajibu wao katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Disemba 14 mwaka huu. Akitangaza maamuzi hayo leo jijini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI- HAWA GHASIA amesema wizara yake imetekeleza wajibu wake kwa kutoa mafunzo na kuwezesha kifedha, hivyo kasoro zilizojitokeza ni uzembe...
Mnenguaji mkongwe wa Bendi ya Twanga pepeta AISHA MBEGU MADINDA amefariki Ghafla leo jijini Dar es salaam. Akizungumza na Efm muda mfupi uliopita Mwimbaji wa bendi hiyo Luiza Mbutu amesema mwili wa Marehemu Aisha Madinda umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa Taarifa za awali shughuli za Msiba huo zitafanyika Kigamboni nyumbani kwao na Marehemu. Tutaendelea kukupa taarifa kupitia vipindi vyetu hapa EFM. Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Marehemu mahali pema Amina. ...
watangazaji na maDJS wa 93.7 EFM wakifanya maandalizi ya tamasha la muziki mnene liliofanyika Dar alive mbagala . watangazaji na maDJS wa 93.7 EFM wakifanya maandalizi ya tamasha la muziki mnene liliofanyika Dar alive mbagala. RDJS wa 93.7 EFM wakianza kutoa burudani katika tamasha la muziki mnene lililofanyika Dar alive mbagala. Baadhi ya mashabiki waliowahi kufika katika tamasha la muziki mnene la 93.7EFM lililofanyika Dar alive mbagala. Godwin Mawanja pamoja na Sada Nassoro wakianza amsha amsha ya...
WAZIRI WA MAMBO ya Nje wa Marekani, JOHN KERRY, ameelezea upinzani wa nchi yake dhidi ya juhudi zozote alizodai zinahujumu mchakato wa uchaguzi wa Israel, huku akisema Marekani inatarajia kutakuwa na njia ya kuendeleza mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati na kuondoa wasiwasi wa Wapalestina. Mkutano wa KERRY umewajumuisha Mkuu wa ujumbe wa wapatanishi wa Palestina, SAEEB ERAKAT, na mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, NABIL El-ARABI. Kabla ya hapo, KERRY amekutana na Waziri Mkuu wa Israel, BENJAMIN...
Pakistan imeingia siku yake ya pili ya maziko na maombolezo, baada ya kundi la wanamgambo wa Taliban kuivamia Shule moja ya Kijeshi na kuwauwa watu 141, wengi wao watoto. Mashambulizi hayo ya kikatili zaidi kuwahi kutokea katika siku za karibuni, yamelaaniwa na viongozi na watu kadhaa mashuhuri duniani. Aidha kundi la Taliban katika nchi jirani ya Afghanistan limeyaita mauaji hayo kuwa ni ya kinyama na yasiyo na uhalali wowote kidini. Waziri Mkuu wa Pakistan, Nawaz Sharif, ametangaza siku tatu za...
SERIKALI INAENENDELEA na mpango wake wa kutoa Elimu ya msingi kwa watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule nchini. Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dokta SHUKURU Kawambwa wakati akiwasilisha mada inayohusu “Namna Tanzania inavyoboresha Usawa wa Kinga ya Jamii katika Sekta ya elimu” katika kongamano la Kimataifa linaloendelea katika siku ya pili jijini Arusha kuhusu Kinga ya Jamii. Dokta KAWAMBWA ameeleza kuwa mpango huo umeanzia Elimu ya Awali, shule ya Msingi na Sekondari ambapo kila...
RAIS JAKAYA KIKWETE amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dokta FENELLA MUKANGARA kuomboleza kifo cha mwanamuziki mkongwe, SHEM IBRAHIM KARENGA kilichotokea Desember 15 mwaka huu katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam alikokuwa amepelekwa kwa matibabu ya ugonjwa wa shinikizo la damu. Enzi za uhai wake, Marehemu KARENGA alijaaliwa kipaji cha muziki hususan upigaji wa gitaa la solo na uimbaji, kipaji ambacho kilimwezesha kufanya kazi katika bendi mbalimbali za muziki hapa nchini akianzia na...
Mwimbaji mwenye umri wa miaka 26 kutoka Marekani Rihanna kwa sasa yupo huko Herzogenaurach, nchini Ujerumani kumalizia dili alilopewa na kampuni ya Puma kuwa balozi mpya wa kimataifa wa bidhaa za michezo za Puma Rihanna atakuwa mkurugenzi kwenye idara ya ubunifu kwa upande wa wanawake atakaeanza kutoa mafunzo kwa jamii mapema mwakani, mkataba huo utadumu kwa miaka kadhaa Kupitia mtandao wa Instagram Rihanna alishea picha akiwa amevaa baadhi ya bidhaa za Puma kama sehemu ya kutangaza bidhaa...