Slider

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUMUWAKILISHA RAIS UINGEREA
Local News

WAZIRI mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kuondoka nchini leo kwenda London nchini Uingereza kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa.   Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa anaenda kumuwakilisha Mheshimiwa Rais kwa sababu siku hiyo ya mkutano atalazimika kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Yower Museven   Akizungumzia kuhusu suala la kupambana na rushwa waziri Mkuu amesema kuwa Tanzania inafanya jitihada...

Like
913
0
Tuesday, 10 May 2016
ASHTAKIWA KWA ULANGUZI WA PEMBE ZA NDOVU
Global News

Kesi dhidi ya mwanamke mfanyabiashara raia wa China anayetuhumiwa na mashtaka ya kuendeleza mtandaoa wa kihalifu wa ulanguzi wa pembe barani Asia imeahirishwa kwa wiki mbili nchini Tanzania. Alifikishwa mahakamani Jumatatu asubuhi mjini Dar es Salaam. Waendesha mashtaka wanasema Yang Feng Glan, anayejulikana kwa umaarufu pia kama Malkia wa pembe, aliendesha biashara haramu ya kuwaua ndovu katika mbuga za wanyama ili kupata pembe zao ambazo wanazisafirisha na kuziuza katika mataifa ya bara Asia. Anashutumiwa kwa kuendeleza shughuli hiyo kwa...

Like
263
0
Monday, 09 May 2016
JUMBA LA GHOROFA LAPOROMOKA MOMBASA
Global News

Sehemu ya jumba kubwa la kibiashara mjini Mombasa imeporomoka siku chache baada ya jumba la makazi kuporomoka jijini Nairobi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40. Sehemu ya jumba hilo la Nyali Centre iliporomoka usiku wa kuamkia Jumatatu. Hakuna aliyeripotiwa kujeruhiwa wakati wa mkasa huo. Polisi, maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu na maafisa wa Mamlaka ya Taifa ya Ujenzi (NCA) wamefika eneo hilo kufanya uchunguzi...

Like
347
0
Monday, 09 May 2016
PICHA: SHIKA NDINGA KIBAHA 2016
Local News

Odinga zikiwa jukwaan zikisubiri kushindaniwa Majaji wakiandaa eneo la kufanya mashindano Swebe Santana akisherehea Choggo Chema Mmoja ya washiriki akipokea maelekezo Mashabiki wakifuatilia mtanange Mashindano yakiendelea David Urasa akikabidhi zawadi kwa baadhi ya washiriki walioingia kwenye fainali kuiwakilisha Kibaha Washindi wa pikipiki wakiwa kwenye pikipiki zao Matery Mushi akikabidhi zawdi kutoka Vodacom Meneja Mkuu E-fm, Denis Ssebo akizungumza na wakazi wa Kibaha Mzee Kungu baya akitoa burudani ya...

Like
674
0
Monday, 09 May 2016
EUROPA LEAGUE: LIVERPOOL YATINGA FAINALI
Slider

Jurgen Klopp amefanikiwa kuifikisha Liverpool katika hatua ya fainali ya ligi ya Uropa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Villarreal. Wakiwa nyuma kwa bao moja katika mchezo wa awali, Liverpool walisawazisha matokeo baada ya Bruno Soriano kujifunga. Daniel Sturridge aliongeza bao la pili baadaye na kuanza kuidididmiza timu hiyo kutoka Uhispania baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Roberto Firmino. Baada ya mchezaji wa Villareal Victor Ruiz kutolewa kwa kadi nyekundu, Adam Lallana alipigilia msumari wa...

Like
284
0
Friday, 06 May 2016
SPIKA PAUL RYAN AMPINGA DONALD TRUMP
Global News

SPIKA wa Republican katika Baraza la Wawakilishi la Marekani Paul Ryan amesema hayupo tayari kumuunga mkono Donald Trump kuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho. Mfanyabiashara huyo bilionea anaonekana dhahiri kushinda katika mbio za uteuzi kukiwakilisha chama hicho lakini Ryan amesema kuwa kabla hakuweza kuidhinisha suala hilo Trump alipaswa kuwaonyesha watu kuwa anaheshimu taratibu za Republican na angepata kura za Wamarekani wengi zaidi. Mapema Marais wa zamani wa Marekani George W Bush na baba yake George Bush waliweka wazi kuwa...

Like
251
0
Friday, 06 May 2016
IDLIB: 30 WAHOFIWA KUFA KWA MASHAMBULIZI YA NDEGE KATIKA KAMBI YA WAKIMBIZI
Global News

AFISA mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amesema mashambulizi ya ndege za angani katika kambi ya wakimbizi,yanahofiwa kuwaua zaidi ya watu 30. Mkuu wa kitengo cha haki za binaadamu katika umoja wa mataifa, Stephen O’Brien ametaka pawepo uchunguzi juu ya shambulizi hilo lililotokea katika jimbo la Idlib, karibu na mpaka wa Uturuki. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Philip Hammond amemtuhumu Rais wa Syria Bashar Al-Assad kwa kuonyesha dharau juu ya juhudi za kimataifa kumaliza mapigano nchini...

Like
234
0
Friday, 06 May 2016
MUFTI MKUU AWATAKA WATANZANIA KUJENGA UMOJA NA USHIRIKIANO
Local News

MUFTI Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber bin Ally amewataka watanzania kudumisha umoja na mshikamano ili kujenga taifa na kuleta maendeleo. Sheikh Zuber ameyasema hayo wakati akizungumza na baraza kuu la waislamu Tanzania BAKWATA katika semina elekezi kwa viongozi wa baraza hilo Taifa. Naye Sheikh mkuu wa mkoa wa Mtwara Nurdin Abdala Athumani ameongeza kuwa watanzania ili wapate maendeleo ni lazima watumie viwanda ipasavyo kuzalisha na kudumisha suala la umoja pamoja na amani iliyopo kwa manufaa ya...

Like
366
0
Friday, 06 May 2016
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO YAKUSUDIA KUTOA TAARIFA YA WANAWAKE WANAOFARIKI KWA MATATIZO YA UZAZI
Local News

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa inakusudia kutoa taarifa ya wanawake wanaofariki Dunia kutokana na matatizo ya uzazi kila baada ya miezi mitatu ili kukabiliana na tatizo la vifo vya wanawake nchini.   Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Viongozi Wanawake kuhusu masuala ya Afya.   Ameeleza kuwa, katika uteuzi atakaoufanya kwenye bodi zilizo chini ya Wizara...

Like
305
0
Friday, 06 May 2016
UGANDA YAPIGA MARUFUKU MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA
Global News

SERIKALI ya Uganda imepiga marufuku urushwaji wa matangazo ya moja kwa moja yanayopinga uchaguzi wa rais Yoweri Museveni. Usalama katika mji mkuu wa Uganda- Kampala umeimarishwa kabla ya maandamano yalioitishwa na chama cha Forum for Democratic Change (FDC). Vyombo vya habari nchini Uganda vimetakiwa kutofanya matangazo ya moja kwa moja na wanachama wa upinzani ambao wanapinga kuchaguliwa kwa rais...

Like
253
0
Thursday, 05 May 2016
MWANAMKE ATOLEWA AKIWA HAI KWENYE KIFUSI NAIROBI
Global News

IMEBAINIKA kwamba Mwanamke amepatikana akiwa hai kwenye vifusi ikiwa ni siku sita baada ya jengo kuporomoka katika mtaa wa Huruma jijini Nairobi. Kwa mujibu wa Pius Masai, mkuu wa kitengo cha taifa cha kukabiliana na majanga, amesema kuwa maafisa wa uokoaji bado wanajaribu kutengeneza njia ya kumtoa kwenye vifusi hivyo. Hata hivyo, mwanamke huyo amekuwa akiwasiliana na matabibu ambao wanasubiri kumpatia matibabu punde...

Like
276
0
Thursday, 05 May 2016