KITUO cha Kulea Wazee wasiojiweza cha Fungafunga kilichopo Manispaa ya Morogoro kinakabiliwa na tatizo la Umeme kwa takribani miezi miwili sasa na kuwafanya kuishi kwa shida bila kujua muafaka wao kutoka Serikalini. Akizungumza na EFM Mwenyekiti wa Wazee hao JOSEPH KANIKI ameeleza kuwa wamekuwa wakikatiwa Umeme mara kwa mara na Shirika la Umeme Tanzania –TANESCO kwa kutolipa bili kwa muda mrefu huku wakiamini Shirika hilo na Serikali wana mawasiliano mazuri. KANIKI amebainisha kuwa kukosekana kwa umeme kunawafanya kushindwa kujihudumia hasa...
MKURUGENZI wa Umoja wa Wakulima wa Chai Rungwe –RSTGA LEBI GABRIEL ameeleza kuwa Wakulima wa zao hilo wanatakiwa kutumia mbegu mpya zilizofanyiwa utafiti wa Kitaalamu ili waweze kupata mazao bora zaidi. GABRIEL ametoa kauli hiyo alipotembelea Shamba la Chai la Kimbila lililopandwa Mbegu mpya za Chai. Amebainisha kuwa Mbegu hizo mpya za kisasa zitamsaidia Mkulima kuondokana na umasikini pindi atakapoanza kilimo chenye tija kwa sababu zinazaa zaidi kuliko mbegu nyingine....
SHIRIKA la Posta TPC wamebadilishana makubaliano ya msingi waliyoyaingia na kampuni ya simu ya Zantel ya huduma mpya ya biashara iitwayo POSTGIRO leo jijini Dar es salaam. Huduma hiyo mpya ya kibiashara ya kukusanya na kulipa fedha kwa niaba ya kampuni, shirika, kiwanda au taasisi za serikali na binafsi itarahisisha ulipaji wa ada, amana, gawio, kodi, pensheni, michango na mishahara. Akizungumza na waandishi wa habari jiijini Dar es salaam Mkurugenzi mtendaji wa TPC DEOS MNDEME amesema inaridhisha kutambua kuwa TPC...
Tanzania imekuwa kwa kiwango kikubwa katika usindikaji na utengenezaji wa bidhaa za Mlonge hali iliyochangia soko la bidhaa hizo kuwa katika ushindani wa kibiashara. EILEEN KASUBI ni mkurugenzi wa kampuni ya MOKAI MORINGA MLONGE amesema bidhaa za mlonge zimekuwa zikiuzika zaidi katika masoko ya ndani na nje kutokana na kuwepo kwa wajasiriamali wengi wanaosindika mlonge ingawa watanzania wengi wahajapata elimu juu ya matumizi ya bidhaa hizo. Amesema wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa za mlonge wanategemea zaidi masoko ya maduka makubwa na...
TAKRIBAN waisreli wanne wameuawa na wengine 8 kujeruhiwa katika kile polisi wanasema ni shambulio la kigaidi dhidi ya Sinagogi eneo la magharibi ya Jerusalem. Kwa mujibu wa Polisi wanaume waliojihami kwa visu na mapanga wanaoshukiwa kuwa Wapalestina ndio waliofanya mashambulizi hayo. Israel imekuwa katika hali ya tahadhari kuu baada ya mashambulio kadhaa na Wapalestina wakizozana na Waisraeli kuhusiana na eneo takatifu ambalo wamekuwa wakizozania kwa muda mrefu....
WATU wanne wameuawa kwa kuchomwa visu na vijana waliokuwa wamejihami mjini Mombasa Pwani ya Kenya. Watu kadhaa pia wamejeruhiwa katika shambulio hilo la usiku wa kuamkia leo kwenye vituo vya basi Kisauni. Bado haijajulikana waliouawa lakini inaaminika walikuwa raia wa kawaida waliokuwa kwenye shughuli zao. Aidha inadaiwa vijana hao walikuwa wameziba nyuso zao, wakipeperusha bendera nyeusi sawa na ile iliyopatikana katika msako wa jana kwenye misikiti ya Musa na Sakinah, jijini Mombasa....
IMEELEZWA kuwa, ili kupunguza msongamano wa Magari Jijini Dar es Salaam Wizara ya Ujenzi imepanga kujenga Daraja la pili pembeni ya Daraja la Salenda litakalo gharimu zaidi ya fedha za kitanzania shilingi bilioni mia moja. Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Ujenzi Dokta JOHN MAGUFULI ameeleza kuwa Daraja hilo jipya litakuwa na uwezo wakupitisha magari zaidi ya elfu sitini kwa...
SERIKALI kupitia ofisi ya Waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji imeshauriwa kuweka kipaumbele suala la uwekezaji katika sekta binafsi ili kuimarisha uchumi wa nchi kwa kuwa sekta hiyo ni mojawapo ya nyenzo muhimu katika maendeleo ya Taifa. Ushauri huo umetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na mwenyekiti wa kamati ya uchumi ya bunge mheshimiwa LUHAGA MPINA wakati akichangia muswada wa marekebisho ya sheria baina ya sekta ya umma na sekta binafsi uliyosomwa kwa mara ya pili na Waziri wa nchi ofisi ya...
muda mfupi uliopita kupitia katika kipindi cha Genge alisikika msanii kutoka Uganda Jose Chameleone akizungumzia taarifa iliyotoka kwamba amemuomba mkali kutoka Tanzania Diamonda wafanye wimbo wa pomoja...
UMOJA wa Ulaya umeahidi kutoa euro milioni 12 kama msaada kwa mataifa yanayopakana na nchi zilizoathiriwa na ugonjwa hatari wa Ebola Afrika Magharibi. Mali, Senegal na Ivory Coast zitanufaika na fedha hizo kuzisadia kujiandaa kukabiliana na kitisho cha mlipuko wa Ebola kupitia kampeni ya kuuhamasisha umma na kutambua mapema maambukizi. Msaada huo mpya umetangazwa na mratibu wa juhudi za kudhibiti Ebola wa Umoja wa Ulaya Christos Stylianides kufuatia ziara yake mwezi huu katika nchi zilizoathirika sana na Ebola, Sierra Leone,...
SHIRIKA la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema polisi katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Kinshasa, walifanya mauaji kadhaa katika operesheni iliyodumu miezi mitatu dhidi ya makundi ya kihalifu. Shirika hilo limesema operesheni hiyo iliyopewa jina Likofi iliyozinduliwa Novemba mwaka uliopita ililenga kukomesha ongezeko la wizi wa kutumia silaha na uhalifu mwingine unaofanywa na makundi madogo yanayojulikana kama kuluna. Katika ripoti iliyotolewa leo shirika la Human Rights Watch linasema polisi walioshiriki...