Kamati ya maamuzi ya shirikisho la soka barani Afrika (CAF) imewapa muda wa siku tano mpaka siku ya jumamosi ya tarehe nane mwezi wa kumi na moja mwaka huu kutoa tamko rasmi juu ya uaandaaji wa michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2015 Morocco walipewa kibali cha kuandaa michuano hiyo lakini kutokana na hofu ya ugonjwa wa Ebola iliwaomba CAF waisogeze mbele au kuahirisha kabisa michuano hiyo iliyopangwa kuanza tarehe 17 mwezi januari mpaka Februari 8 mwaka 2015. Wakati huohuo...
TENNIS Kuelekea katika michuano ya ATP World Tours pale jijini London nchini England, makundi na ratiba ya michuano hiyo inayotarajiwa kuanza tarehe 9 mpaka 16 mwezi huu yapangwa rasmi hapo jana usiku. Bingwa namba moja katika mchezo huo, Novak Djokovic amepangwa katika kundi A pamoja na wachezaji wengine watatu nafasi zao duniani katika mabano, Satnislas Wawrinka (4), Tomas Berdych (7) na Marin Cilic (9). Katika kundi B limewakutanisha vigogo Roger Federer anayesika nafasi ya pili kwa ubora duniani, Muingereza Andy...
KITUO cha Wanawake Mkoa wa Ruvuma Wilaya ya Namtumbo –MKOMANILE, kimeiomba serikali kuwapatia msaada wa mashine za kisasa za kushonea nguo pamoja na umeme. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Kituo hiko JANETH LOPENZA amesema kuwa lengo la kikundi ni kuinua uchumi wa wanawake vijijini kupitia uzalishaji wa ujasiriamali. LOPENZA amethibitisha kuwa kupitia msaada wa taasisi mbalimbali imewasaidia kujenga maabara ya vifaa vya samani, malighafi na mashine za...
MELI ya Jeshi la Libya imeshambuliwa na watu 13 wameuawa katika mapigano makali yaliyoshirikisha ndege na vifaru kati ya jeshi na wanamgambo wenye itikadi kali karibu na mji wa Benghazi. Jeshi la serikali likiungwa mkono na vikosi vitiifu kwa jenerali wa zamani, Halifa Khaftar lilifanya mashambulizi dhidi ya wanamgambo hao. Wakaazi wa eneo hilo wamesema, raia kadhaa wanauhama mji huo,wakiitika wito wa jeshi kuwataka waondoka katika mji huo wa bandari ambako maafisa wa usalama wamesema wanamgambo wa wamejificha baada ya...
DAKTARI mwingine amekufa kwa ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone. Daktari huyo ambaye alikuwa muuguzi mkuu katika hospitali ya Kambi kaskazini mwa Siearra Leone ni wa tano kuuawa na ugonjwa huo nchini humo na inaaminika kwamba aliambukizwa Ebola na mgonjwa ambaye alimtibu maradhi mengine, kwa sababu hakuwahi kumtibu mgonjwa mwenye maradhi hayo hatari. Kwa ujumla, wahudumu wa afya wapatao 100 wameuawa na maradhi hayo nchini Sierra Leone. Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limesema watu zaidi ya 4,900 wamekufa kutokana na...
VIKAO vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vimeanza leo mjini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine bunge litakaa kama kamati ya Mipango kwa mujibu wa masharti ya kanuni ya 94 kifungu cha kwanza na kupokea, kujadili na kutoa maoni na ushauri kuhusu bajeti ya Serikali, vyanzo vya mapato pamoja na mapendekezo ya utekelezaji wake. Baadhi ya Miswada itakayosomwa ni pamoja na muswada wa Sheria ya kodi ya ongezeko la thamani ya mwaka 2014, muswada wa sheria ya...
Mtendaji wa bodi ya TFF inayosimamia ligi kuu na ile ya daraja la kwanza, Sylas Mwakibinga ameamua kuachana na kibarua chake kwenye taasisi hiyo nyeti ya soka nchini. Uchunguzi wa E.sports umegundua kwamba Mwakibinga ameamua kuachia ngazi katika nafasi yake kutokana na mvutano mkubwa unaoendelea kati ya rais wa TFF -Jamali Malinzi na wakali Damas ndumbaro aliyezawadiwa kifungo cha miaka 7 kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje nchi kwa madai ya kutoa siri nzito zilizojificha ndani ya shirikisho...
BARAZA la vijana la chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, – Bavicha, limelaani vikali kitendo cha kudhalilishwa kwa Jaji mstahafu Josefu Sinde Warioba na kusema kuwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa haki na fedhea kwa Taifa. WAKATI HUO HUO, kufuatia tukio la vurugu zilizotokea katika mdahalo wa Katiba ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere zikihusishwa na aliyekuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba PAUL MAKONDA, Mjumbe huyo amekanusha tuhuma hizo…. MAKONDA Jana, mara baada ya vurugu hizo lilijitokeza kundi la...
Bei za mauzo ya fedha sokoni leo. Dola ya imenunuliwa kwa shilingi 16 na sent 80 na kuuzwa kwa shilingi 17 na senti 15 Pound imenunuliwa kwa shiling 26 na senti70 na kuuzwa kwa shilingi 2,800 Euro imenunuliwa kwa shilingi 2,na senti 80 na kuuzwa kwa shilingi 2,190 Fedha ya Kenya imenunuliwa 18.na senti 4 kwa shilingi na kuuzwa kwa shilingi 19na senti 8 Na fedha ya Uganda imenunuliwa kwa shilingi 0.50 na kuuzwa kwa shilingi 0.80 ...
BARAZA la wafanyabiashara Afrika mashariki –EABC- limetoa mafunzo kwa wahandisi wasanifu kuihamasisha Serikali ya Tanzania iweze kusaini mkataba wa makubaliano ya kutambulika katika nchi tano ili kuwawezesha kupata fursa za biashara na kazi. Hatua hiyo imefikiwa baada ya Tanzania kuwa nchi pekee iliyobakia kusaini makubaliano hayo kutokana na kutokukubaliana na baadhi ya mambo ambayo wana uhakika yanaweza kurekebishwa na kuruhusu mkataba huo kusainiwa. Akizungumza na EFM mjumbe wa EABC ADRIAN NJAU amesema mpaka sasa wameshasaini makubaliano...
VIONGOZI wa vyama vya ushirika wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi wameiomba wizara ya kilimo na ushirika kutoa elimu kwa wanachama juu ya sheria mpya ya ushirika ili iweze kutambulika na upunguza migogoro na mivutano inayosababisha vyama kugawanyika na kukosa nguvu ya kiuchumi na uzalishaji. Ombi hilo limetolewa na viongozi wa vyama vya ushirika vya MAKINI , MKOTOKUYANA,NDOMONI na MARAMBO wakati walipokuwa wanazungumza na waandishi wa habari wilayani humo. MOHAMEDI MUSA mwenyekiti wa chama cha msingi Makini...