UMOJA wa Mataifa umesema ubakaji na njia nyingine za matumizi ya nguvu yanafanywa na pande zote katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan kusini. Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya nguvu kingono katika mizozo ya kivita, Zainab Hawa Bangura, amesema hali hiyo imesambaa mno ambapo hadi mtoto wa miaka miwili alikuwa miongoni mwa wahanga. Mapigano yalizuka Desemba mwaka jana nchini Sudan kusini baada ya miezi ya hali ya...
MWANARIADHA wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp. Hii ni baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia ya mauaji bila ya kukusudia. Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo. Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka...
KAMPUNI kubwa ya mafuta ya Ufaransa, Total imetangaza kwamba mkurugenzi wake mkuu, Christophe de Margerie ameuawa katika ajali ya ndege iliyotokea katika uwanja wa ndege wa Moscow nchini Urusi. Taarifa zimeeleza kuwa ndege ya binafsi aliyokuwa akisafiria afisa huyo imeanguka kwenye uwanja wa nukovo ulio nje kidogo ya jiji la Moscow. Vyombo vya habari vya Urusi vimesema kuwa ndege hiyo ilikuwa na abiria mmoja tu, pamoja na wahudumu watatu, wote wakiwa raia wa Ufaransa....
RAIS wa Nigeria Goodluck Jonathan amesema mafanikio ya nchi yake dhidi ya maradhi ya Ebola yametokana na imani ya wananchi wa kawaida kwa maagizo yaliyotolewa na serikali, kuwataka wabadili mienendo yao ya kila siku maishani kama vile kusalimiana kwa kupeana mikono, na utaratibu wa mazishi. Amesema serikali yake ilikuwa na wasiwasi kwamba makanisa yangekataa kuitikia wito huo katika suala la komunio ambapo watu wapatao 1,000 wanaweza kushiriki kikombe kimoja. Ameyasifu makanisa kwa kuusimamisha utaratibu huo, na hata ule wa kutakiana...
baada ya msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond kufanya show akiwa na mavazi yanayosemekana kuwa ni sare ya Jeshi yeye na dancers wake, lakini pia kuonekana kwenye baadhi ya picha akiwa na mavazi hayo huku ameshika siraha na kuvuta sigara hii ndio kauli kutoka kwa msemaji wa jeshi akisema siruhusa kwa vikundi ama mtu mmoja mmoja kutumia sare hizo, pamoja na said Fella moja ya watu wanaomsimamia Diamond akieleza kuhusu mavazi hayo kupitia interview ya redio leo kwenye 411...
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Yessaya Ambikile amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Efm imezungumza na kaka wa marehemu na kuthibitisha hilo kwa kusema Yp alikuwa anasumbuliwa na kifua.. EFM inawapa pole wanafamilia na wapenzi wa msanii huyu alieitumikia sanaa ya muziki wa kizazi kipya, Bongo fleva katika kipindi cha uhai wake ...
Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake. Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti wake wa mgongo baada ya kupiga pindu uwanjani akisherehekea bao lake la kusawazisha kw atimu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC. Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini baadaye alifariki. Mechi hiyo ambapo alipata jerehe la mgongo, ilikuwa mechi muhimu katika ligi ya nchi hiyo. Taarifa...
IMEELEZWA KUWA, Imani Potofu dhidi ya Chanjo za Surua na Rubella zinazoendelea kutolewa kote nchini, zimekuwa kikwazo katika kufanikisha kampeni hiyo yenye lengo la kupunguza ongezeko la magonjwa ya milipuko kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi tisa hadi miaka 15. Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Ilala RAYMOND MUSHI wakati wa uzinduzi wa chanjo ya Surua na Rubella… Naye Mgeni rasmi katika uzinduzi huo, bwana REGINALD MENGI amesema hilo. Kwa upande wake mratibu wa chanjo mkoa wa Dar...
CHAMA Cha Wataalam wa Habari za afya Afrika-AHILA kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wameandaa mikakati ya kusambaza taarifa muhimu za afya kwa wananchi kwa kutumia mitandao ya habari ikiwemo simu za mikononi Akizungumza na wadau mbalimbali jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa mkutano wa kumi na nne wa wataalam wa habari za afya Afrika, Makamu wa Rais Dokta AHMED BILALI amesema kuwa taarifa za afya kutoka kwa wataalam mbalimbali wa afya nchini zitawafikia wananchi...
Shirika la afya duniani linatarajiwa kutangaza rasmi kuwa taifa la Nigeria halina ugonjwa wa bola baadae hii leo, wiki sita baada ya kutoripotiwa kwa visa vya ugonjwa huo . Nchi giyo yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, alipokea sifa tele kwa hatua zake za haraka kukabiliana na Ebola baada ya mwanmadiplomasia Mliberia mwenye ugonjwa huo kwenda Nigeria mwezi Julai. Shirika la afya duniani lilitangaza Senegal kutokuwa tena na Ebola mnamo siku ya Ijumaa. Mlipuko unaoshuhudiwa wa Ebola, umewaua watu...
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake waliyehasimiana Riek Machar, leo wamealikwa kuhudhuria uzinduzi wa mazungumzo ya kutafuta muafaka ndani ya chama cha SPLM kinachoongoza taifa hilo lenye machafuko ya kisiasa. Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika Arusha chini ya usimamizi wa CCM, chama tawala nchini Tanzania. Endapo mahasimu hao wawili watafika na kukaa meza moja itakuwa ni hatua muhimu katika jitihada ambazo zimekuwa zikifanyika na jumuiya ya kimataifa kupata muafaka wa machafuko yanayoendelea katika taifa hilo changa...