Baada ya kipigo cha magoli 4-0 dhidi ya timu yake, Meneja wa klabu ya Man Utd Van Gaal amelia na kikosi chake ambacho jana usiku kiliendelea kupata matokeo mabaya tangu kuanza kwa msimu mpya wa soka huko nchini Uingereza Agosti 16. Kocha Van Gaal amesema kikosi chake hakikucheza vizuri wakati wa mchezo wa michuano ya kombe la ligi dhidi ya klabu ya Milton Keynes Dons ambao waliibuka na ushindi wa mabao manne kwa sifuri na kuwatupa nje ya michuano hiyo...
Israel na wapiganaji wa Ki Palestina wamekubaliana kusitisha mapigano kwa muda mrefu katika ukanda wa Gaza. Kusitishwa kwa mapigano hayo, kumehitimisha wiki saba za vita vilivyosababisha vifo vya watu zaidi ya 2,200, wengi wao wakiwa Wapalestina. Mazungumzo hayo yalisimamiwa na Misri na yalianza kutekelezwa jana kuanzia majira ya saa moja usiku. Hamas wamesema mpango huo unawakilisha “ushindi wa upinzani wao”.Maafisa wa Israel wamesema Israel italegeza vikwazo ilivyoiwekea Gaza ili kuruhusu misaada na vifaa vya ujenzi kuingia Gaza....
Rais Jakaya Kikwete anatarajia kukutana na viongozi wa Vyama vya Siasa vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ili kuzungumzia mchakato wa Katiba wakati wowote wiki hii. Katika mkutano huo, ambao unasubiriwa kwa hamu, Rais Kikwete atakutaka na wajumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao unaundwa na vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema na CUF. Aprili 16, mwaka huu wajumbe wa Ukawa na baadhi kutoka Kundi la 201, walisusia vikao vya Bunge hilo wakitaka msingi wa mapendekezo ya Rasimu ya Katiba...
Rais JAKAYA KIKWETE ametoa wiki moja kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro, kuwapatia viwanja vya kujenga nyumba wahanga wa mafuriko ya kiasi cha miaka minne iliyopita mjini Kilosa.Rais KIKWETE ametoa agizo hilo mkoani Morogoro alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kilosa katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Kilosa baada ya kutembelea Wilaya hiyo kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo.Agizo hilo limekuja kufuatia malalamiko yaliyotolewa na wahanga hao kwa njia ya maneno na mabango baada ya kuwa wameahidiwa...
Shirikisho la Soka Tanzania TFF leo lilikuwa linatarajiwa kutuma rasmi maombi ya kuandaa michuano hiyo inayotakiwa kufanyika mwaka 2017, baada ya Libya kujitoa. Akizungumza leo mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za shirikisho hilo Karume Ilala jijini Dar-Es-Salaam, katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa, amewaambia waandishi wa habari kuwa, baada ya kupata taarifa za libya kujitoa, wajumbe wa kamati ya utendaji ya TFF jana walikutana kujadili na kupitisha uamuzi wa kutuma maombi rasmi ambapo kwanza watapeleka taarifa rasmi serikalini...
Aliyekuwa mtangazaji wa Redio One katika kipindi cha “Spot Leo” Omary Katanga amefuata nyayo za pacha wake Maulid wa Kitenge aliyejiunga na kituo cha redio 93.7 E FM mapema wiki hii.Katanga na Kitenge walikuwa wote Redio One, na wataanza kusikika E FM kesho(Leo) katika kipindi cha michezo cha E Sports, ambacho kitakuwa kikiruka kila siku saa 7:00 – 7:30 usiku.Watangazaji hao wanajiunga na watangazaji wengine maarufu kama Dennis Ssebo, Dickson Ponnela (Dizzo 1), DJ Majay, na Kanky...
Welcome to WordPress. This is your first post. Edit or delete it, then start...
Watangazaji mahiri wa michezo nchini, Maulid Kitenge na Omari Katanga jana usiku wameanza kazi rasmi katika kituo chako cha Radio EFM. Watangazaji hao mahiri ambao wote wamejiunga wiki hii watakuwa wakitangaza katika kipindi cha michezo cha E Sports kinachoruka hewani kuanzia mida ya saa moja kamili usiku. Kwa kuanzia pia Mtangazaji Maulid Kitenge alikuwa uwanja wa ndege wa Kimataifa jana usiku kukutangazia moja kwa moja yaani live kuwasili kwa nyota wa timu ya wakongwe wa real...
Timu ya soka ya Azam Fc ambayo ilikuwa inashiriki mashindano ya cecafa kwa timu za ukanda wa Africa Mashariki nchini Rwanda imeyaaga rasmi mashindano hayo jioni hii baada ya kufungwa na timu ya Sudan El marreikh kwa penati 4 kwa tatu. Timu hizo ambazo zimekutana katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya Cecafa Kagame Cup zilishindwa kufungana magolo ndani ya dakika 45 za kila upande na hivyo kuamuliwa zipige penati iliyoamua mshindi kati yao. Mabao ya Azam ya penati...
Mtangazaji mahiri wa michezo wa siku nyingi Maulidi Baraka Kitenge amejiunga na kituo cha radio kiitwacho EFM 93.7 kilichopo Kawe jijini Dar Es salaam. Kutokana na tafiti ya ipsos ya mwaka 2013,inasemekana kuwa mtangazaji huyo wa zamani wa kituo cha redio one,ndie mtangazaji bora wa michezo nchini Tanzania. Mkurugenzi wa vipindi wa Radio EFM,Dickson Ponela,ameeleza kufurahishwa kwakwe kwa mtangazaji huyo kinara kuhamia katika kituo hicho. “Mpaka sasa Maulidi Kitenge ameshasign mkataba na kituo chetu na anatarajia kusikika hivi karibuni...
Hi ni baadhi ya Picha ya Matukio katika Tamasha Lilifanyika mwembe...