Slider

KAMATI BORA ZA KUDHIBITI UKIMWI ZAZAWADIWA PANGANI
Local News

SHIRIKA lisilo la kiserikali Wilayani Pangani la-UZIKWASA linalojishughulisha na kuziwezesha kamati za kudhibiti Ukimwi, limetoa zawadi kwa kamati bora za kudhibiti ukimwi Wilayani humo.   Katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Jaira, kata ya Madanga wilayani Pangani na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi kutoka halmashauri ya Wilaya ya Pangani mgeni rasmi alikuwa Kaimu Afisa Maendeleo wa Wilaya hiyo, Bi.Patricia Kinyange.   Akizungumza katika hadhara hiyo Bi. Kinyange amelipongeza shirika hilo kwa kuzijengea uwezo kamati hizo...

Like
451
0
Monday, 21 December 2015
VYUO NA TAASISI ZA ELIMU ZIMETAKIWA KUTOA MAFUNZO YANAYOENDANA NA SOKO LA AJIRA
Local News

KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amevitaka vyuo na taasisi za elimu nchini kuhakikisha vinatoa mafunzo bora yanayoendana na mahitaji ya soko la ajira.   Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika mahafali ya kwanza ya Shahada ya Takwimu Rasmi katika Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Balozi Sefue amesema ni vyema vyuo na taasisi za elimu zikahakikisha zinafanya tafiti ili kujua mahitaji ya wataalamu wanaotakiwa.   Hata hivyo serikali imekuwa mstari wa mbele kupitia Wizara ya Fedha kuhakikisha inakisaidia...

Like
254
0
Monday, 21 December 2015
PEP GUARDIOLA AFIKIA TAMATI BAYERN
Slider

  Pep Guardiola kuondoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu na nafasi yake kuchukuliwa na Carlo Ancelotti .   Guardiola, 44, amekuwa akitajwa kujiunga na moja kati ya klabu za  Manchester City, Manchester United, Chelsea na Arsenal. Mwalimu huyu wa zamani wa Barcelona amefanikiwa kutwaa mataji mawili ya ligi na kombe la Ujerumani toka ajiunge na Bayern katika msimu wa kiangazai mwaka 2013.   Bosi wa zamani wa klabu ya Chelsea Ancelotti, 56, amekuwa akipewa kipaumbele kujiunga na Bayern toka kibarua chake...

Like
269
0
Monday, 21 December 2015
VIBURI VYA WACHEZAJI WA KIGENI,VINAVYOVURUGA MIPANGO YA SIMBA NA YANGA.
Slider

Na Omary Katanga. Ni jambo la kawaida kuwepo na wachezaji wa kigeni katika Klabu za soka kwenye mataifa mbalimbali,lengo likiwa ni kuongeza ushindani na kutoa changamoto kwa wachezaji wazawa ili nao waongeze juhudi katika usakataji kandanda uwanjani. Lakini uwepo huo wa wachezaji wa kigeni,unategemea sana uwezo wa kifedha kwa klabu husika kutokana na ukweli kwamba huwa wanalipwa kiasi kikubwa cha mshahara na marupurupu mengine kuliko mchezaji wa ndani,na hii inadhihirisha pia utofauti wa kiuchezaji kati yao. Klabu za Simba na...

Like
432
0
Saturday, 19 December 2015
E-FM YAILAZA BOKO BEACH VETERANI 3-1
Slider

E-fm imeufunga mwaka kimichezo kwa kipute cha dakika 90 za mpira wa miguu dhidi ya maveterani wa Boko Beach katika uwanja wa Boko Beach. E-fm ilifanikiwa kutawala mchezo katika kipindi cha kwanza na kuweza kuzitandika nyavu za Boko Beach Veterani magoli mawili. Kasi ya mchezo ilibadilika katika kipindi cha pili baada ya E-fm kuandika bao lake la tatu kupitia nyota wake John Makundi, goli hilo liliamsha kikosi cha Boko Beach Veterani  kwa kuutumia vizuri mpira wa adhabu kwa E-fm kujipatia...

Like
576
0
Saturday, 19 December 2015
VATCAN YATHIBITISHA MOTHER TERESA KUWA MTAKATIFU
Global News

MAKAO MAKUU ya Vatican yemedhibitisha kwamba mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel na mtawa Marehemu ‘Mother Teresa’ atatangazwa mtakatifu. Taarifa ya Vatican inasema Papa Francis ameridhia utaratibu wa kumtangaza mtakatifu mtawa huyo baada ya kutambua muujiza wa pili uliohusishwa naye. Muujiza huo alipokea mwanamme raia wa Brazil ambaye alipona saratani kwenye ubongo wake....

Like
311
0
Friday, 18 December 2015
AU YATANGAZA KUTUMA WALINDA AMANI BURUNDI
Global News

MUUNGANO wa Afrika umetangaza mpango wa kutuma walinda amani nchini Burundi kuzuia machafuko zaidi nchini humo. Muungano huo umepanga kutuma walinda Amani elfu 5,000 wa kulinda raia.   Umoja wa Mataifa unakadiria watu 400 wameuawa tangu machafuko kuzuka mwezi Aprili  baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kwamba angewania urais kwa muhula wa tatu.   AU huenda ikalazimika kutuma walinda amani bila kupewa idhini na taifa mwenyeji, muungano huo utatumia kwa mara ya kwanza kifungu kwenye mkataba wake, kinachouruhusu kuingilia kati...

Like
254
0
Friday, 18 December 2015
CHADEMA YAITAKA NEC KUONDOA VIKWAZO MAJINA YA MADIWANI
Local News

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini –NEC,  kuhakikisha inaondoa vikwazo vyote  katika mchakato wa kutangaza majina ya madiwani wa viti maalumu . Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dae Es Salaamu leo,  Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho SALIMU MWALIMU,  ameitaka tume hiyo kutenda haki katika kugawanya viti maalumu vya udiwani kwa kufuata kanuni na taratibu za ugawaji .  ...

Like
231
0
Friday, 18 December 2015
DK KIGWANGALLA ATUMBUA MAJIPU YA WACHELEWAJI WIZARA YA AFYA
Local News

NAIBU  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dokta. Hamisi Kingwangalla amefanya ukaguzi wa kushtukiza katika ofisi za wizara hiyo kwa kusimama getini kuzuia wafanya kazi wote wa wizara ambao walikuwa wamefika ofisini baada ya saa 1:30 asubuhi muda ambao ndiyo mwisho wa wafanyakazi kuingia ofisini.   Awali Dkt. Kingwangalla alifika ofisini saa 1:05 asubuhi huku akiingia ofisini kwa kutembea mwenyewe bila kutumia usafiri wa gari na kwenda moja kwa moja ofisini kwake ambapo alitoka ilipofika saa...

Like
317
0
Friday, 18 December 2015
MAISHA YA MOURINHO YAFIKIA TAMATI NDANI YA CHELSEA
Slider

Meneja wa klabu ya Chelsea ya Uingereza amefutwa kazi baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya. The Blues walishinda Ligi ya Premia msimu uliopita lakini msimu huu mambo yamekuwa kinyume, na wamo alama moja tu juu ya eneo la kushushwa daraja ligini. Bodi ya klabu hiyo ilikutana jana kujadili hatima ya Mourinho chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman Abramovich. Klabu hiyo kupitia taarifa imesema mkataba kati ya klabu na meneja hiyo umekatishwa kwa maelewano kati ya...

Like
283
0
Friday, 18 December 2015
UN KUKATA MIFUMO YA FEDHA KWA IS
Global News

BARAZA la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio lenye lengo la kukata mifumo ya fedha kwa kundi la Islamic State. Mkutano wa kwanza wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa mawaziri wa fedha umeafiki juu ya azimio hilo lililobuniwa kwa ajili ya kuzuia fedha kuwafikia wanamgambo wa Islamic State. Mkutano huo umeyataka mataifa kufanya juhudi za haraka kukata mifumo ya udhamini wa fedha kwa kundi hilo kwa kuzuia wizi wake wa mafuta na raslimali nyingine.  ...

Like
213
0
Friday, 18 December 2015