VIONGOZI wa muungano wa Ulaya wamesema wako tayari kufikia mapatano ya kuiwezesha Uingereza kusalia katika Muungano huo. Hata hivyo viongozi hao wanaokutana mjini Brassels, wamesisitiza kuwa makubaliano yoyote hayapaswi kuvunja kanuni za muungano wa Ulaya. Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema kumekua na mafanikio, lakini akasema bado kuna kazi ngumu inayowasubiri mbele...
SERIKALI Mkoani TABORA imewataka wawekezaji katika kiwanda cha Nyuzi cha TABORA kurejesha kiwanda hicho mikononi mwa serikali kutokana na kushindwa kukiendesha kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa na kuwakosesha wananchi ajira. Akizungumza katika ziara ya kushitukiza kiwandani hapo, Mkuu wa Manispaa ya TABORA, Bwana SULEIMAN KUMCHAYA amesema kufuatia wamiliki wa kiwanda hicho kutoka INDIA kushindwa kukiendesha,iko haja ya kukirudisha mikononi mwa serikali. Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la TABORA mjini, Mheshimiwa EMMANUEL MWAKASAKA...
WITO umetolewa kwa Watanzania kuungana kwa pamoja na kufuata mafundisho yanayo jenga amani katika nchi na kuacha mafundisho ambayo yana weza kuleta mfalakano ili kuilinda amani ya nchi iliyopo. Wito huo umetolewa Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Usalama wa jeshi la wananchi wa Tanzania -JWTZ Meja Jenerali VENANCE MABEYO wakati wa uzinduzi wa utafiti uliofanywa na taasisi isiyo ya kiserikali ya TWAWEZA ambao ulilenga kuangalia matukio ya kiitikadi ambapo amesema kuwa sababu kubwa inayo sababisha vitendo hivyo kuwepo...
Luis Suárez awa mchezaji wa kwanza kufunga hat trick katika michuano ya klabu bingwa dunia huko nchini Japan, rekodi hiyo imewekwa na nyota huyu muda mfupi uliopita katika mchezo kati ya Barcelona vs Guangzhou mechi iliyomalizika kwa Barcelona kuibuka na ushindi wa...
WAZIRI MKUU wa Ethiopia Hailemariam Desalegn amesema serikali yake itakabiliana vikali na makundi yanayohujumu amani baada ya watu kadha kuuawa kwenye maandamano eneo la Oromia. Serikali inasema watu watano wameuawa kwenye makabiliano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama lakini makundi ya upinzani na watetezi wa haki za kibinadamu yanasema idadi ya waliofariki inakaribia 40. Akihutubu kupitia runinga ya taifa ya Ethiopia, Bw Desalegn amesema umma pia una jukumu la kutekeleza katika kukabiliana na makundi hayo. ...
MKUTANO maalum wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa unaendelea mjini Geneva kujadili hali nchini Burundi. Kabla ya mkutano huo kufanyika mjini Geneva, Uswizi, Katibu Mkuu wa umoja UN Ban Ki-moon alikuwa ameonya kuwa taifa hilo limo hatarini ya kutumbukia kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo yanaweza kuathiri kanda yote. Amesema machafuko yaliyotokea nchini Burundi siku za hivi majuzi yanatisha na kwamba atamtuma mshauri wake maalum kwenda Burundi kwa mashauriano ya dharura na serikali....
SHIRIKA la Maendeleo ya Vijana nchini (RESTLESS) linatarajia kukutana na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wakiwemo wabunge na madiwani kutoka vyama tofauti pamoja na viongozi wa Serikali ili kujadili mapendekezo yaliotokana na ilani ya vijana ya mwaka 2015 -2020. Akizungumza jijini dare s Salaam kwenye semina iliyoandaliwa na shirika hilo na kuwakutanisha vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini walioshiriki kuandaa ilani hiyo, Mkurugenzi wa Restless development Margaret Mliwa, amesema kuwepo kwa viongozi hao kesho kutawasaidia vijana...
IMEELEZWA kuwa, ili kuhakikisha kwamba wananchi wanaishi kwa raha na amani kipindi chote cha mwaka hasa kipindi cha masika, serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania leo imeanza kubomoa baadhi ya maeneo yanayo zunguka bonde la mto msimbazi. Efm imetembelea maeneo ambapo zoezi la bomoa bomoa limetekelezwa na kushuhudia katapila la serikali likivunja nyumba hizo ambapo mpaka efm inaondoka zaidi ya nyumba 30 zilikuwa zimevunjwa . Wakizungumza na e fm huku zoezi likiwa linaendelea baadhi ya viongozi wanao simamia zoezi...
Wiz Khalifa na Amber Rose wamethibitisha kuwa msimu wa sikukuu huunganisha familia pamoja. Wawili hawa wameweka tofauti zao pembeni na kutoka pamoja mapema jumatano iliyopita ikiwa ni sehemu ya kuonyesha mapenzi kwenye malezi ya motto wao Sebastian huko Loss...
Uvumi kuhusu hatma ya maisha ya boss wa Chelsea Jose Mourinho huenda ni miongoni mwa mambo yanayojadiliwa zaidi kwenye ulimwengu wa soka kwa sasa. Chelsea imekuwa ikifanya vibaya kwenye michezo yake hali iliyopelekea hadi Mourinho kutoa kauli ya kuwa anasalitiwa na wachezaji wake. Akizungumza kuhusu hatma ya boss huyu Pat Nevin mchezaji wa zamani wa klabu hiyo amesema tetesi za kutimuliwa kazi kwa boss huyo si jambo geni na hadhani kama linaweza kutokea Nevin ameongeza kuwa anakubali kuwa hatma ya...
KIMBUNGA kilichokuwa na kasi ya kilometa 200 kwa saa kimeukumba mji wa Sydney nchini Australia leo , na kuezuwa mapaa ya nyumba katika kitongoji cha kusini ya pwani ya mji huo na kusababisha mafuriko na mvua ya mawe. Kimbunga hicho , kilichokuwa na upepo mkali kuwahi kuonekana katika mji wa Sydney , kilikuwa sehemu ya kimbunga kikubwa kilicholikumba eneo la pwani ya kusini ya New South Wales na Sydney kabla ya kuelekea upande wa ...