Slider

THAILAND YAANZA KUCHUNGUZA MAGAIDI
Global News

POLISI nchini Thailand wanachunguza ripoti zinazoeleza kuwa wanamgambo kumi kutoka kundi la wapiganaji wa Islamic state wameingia nchini humo na wanapanga kushambulia sehemu zinazomilikiwa na Urusi. Taarifa hizo zimeeleza kwamba Sita kati yao wameripotiwa kuelekea maeneo ya kifahari ya Pattaya na Phuket huku wengine wakiwa hawajulikani waliko. Hata hivyo Polisi nchini humo wamesema kuwa hawajafanikiwa kuthibitisha uwepo wa raia hao wa Syria nchini...

Like
229
0
Friday, 04 December 2015
BOMU LAUA 16 MISRI
Global News

WATU 16 wameuawa katika mji mkuu wa Mirsi, Cairo, baada ya bomu kulipuliwa kwenye mgahawa mmoja lililopo eneo la Agouza, katikati ya jiji hilo. GAZETI la The Cairo Post linasema watu watatu waliokuwa wamejifunika nyuso zao walirusha bomu mgahawani na kisha kutoroka. Shirika la habari la Reuters limemnukuu afisa mmoja wa usalama, ambaye hakutajwa jina lake, akisema mmoja wa washukiwa ni mfanyakazi wa zamani wa mgahawa...

Like
239
0
Friday, 04 December 2015
ZAHANATI KUNUFAIKA NA MITAMBO YA SOLA
Local News

ZAIDI ya mitambo ya sola 30 imetolewa kwa jamii mbalimbali yenye uhitaji zikiwemo Zahanati, vituo vya afya, ofisi za watendaji kata  na shule mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia kuboresha huduma zao wanazotoa kwa jamii.   Hayo yamesemwa na Meneja masoko wa kampuni ya Sola ya  Mobisol Seth- Joseph Zikhali wakati akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kutangaza ofa mpya ya msimu wa sikukuu kwa wateja...

Like
277
0
Friday, 04 December 2015
ASKARI MAGEREZA KUAZIMISHA SIKU YA UHURU KWA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO
Local News

KATIKA kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika Disemba 9 mwaka huu, watumishi wapatao 39 wa Jeshi la Magereza nchini wanatarajiwa kuadhimisha siku hiyo kwa kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro. Washiriki hao wanatoka katika vituo vya Makao Makuu ya Magereza, Chuo cha Taaluma ya urekebishaji Ukonga Dar es salaam, Kikosi Maalum cha Kutuliza Gasia ambao kwa gharama zao wameamua kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wa Tanganyika kwa kufanya utalii wa ndani. Akizungumza na...

Like
458
0
Friday, 04 December 2015
BAN KIN MOON AZITAKA NCHI ZENYE NGUVU KUTIMIZA AHADI ZAO
Global News

KATIBU MKUU wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema nchi zenye nguvu zaidi kiuchumi duniani lazima zitimize ahadi zao za kuchangisha kiasi cha dola bilioni 100 kufadhili juhudi za kulinda mazingira ifikapo mwaka 2020. Ban Ki-moon amewaambia wanahabari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuwa nchi zinazostawi zinataka msimamo thabiti kuhusu ufadhili huo uliokubalika katika mkutano wa kilele wa mazingira mjini Copenhagen, Denmark mwaka 2009. Nchi maskini zinatafuta mabilioni ya fedha ili kuepusha athari za kutolewa kwa gesi chafu...

Like
218
0
Friday, 04 December 2015
MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE URUSI NA UTURUKI WAKUTANA BELGRADE
Global News

MAWAZIRI wa mambo ya nje wa Uturuki na Urusi wamekutana mjini Belgrade, katika mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu kati ya viongozi wa nchi hizo mbili tangu kudunguliwa kwa ndege ya Urusi na Uturuki wiki iliyopita. Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov alikutana na mwenzake wa Uturuki Mevlut Cavusoglu pembezoni mwa mkutano wa shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya OSCE. Lavrov amesema alikutana na Cavusloglu baada ya kumuomba mara kadhaa kukutana naye lakini hakuna jipya...

Like
187
0
Friday, 04 December 2015
TEMEKE WAANZA KUPATIWA HUDUMA YA AFYA KWA NJIA YA KADI
Local News

MFUKO wa afya ya jamii   umezindua rasmi huduma ya tiba (TIKA) kwa kadi katika Manispaa ya Temeke utakao mwezesha mwananchi  kupata hudua hiyo kwa gharama nafuu. Akizungumza katika ufunguzi huo,  mkurugenzi wa mfuko  wa afya ja jamii – CHF, bwana Eugen Mikongoti amesema kuwa mpango huo ni mpango wa hiari ulioanzishwa kwa sheria namba 1 ya mwaka 2001  ambapo chini ya mpango huo mwana jamii anaweza kuchangia kiasi cha fedha kilicho kubalika katika mamlaka ya jamii ili kumwezesha kupata matibabu...

Like
275
0
Friday, 04 December 2015
TCRA: SOFT BOX HAINA UWEZO WA KUFANYA UDUKUZI WA TAARIFA ZA MAWASILIANO
Local News

MAMLAKA ya Mawasiliano imefanya uchunguzi kubaini kuwepo kwa Programu (Application) ya simu ikijulikana kama SOFTBOX TANZANIA iliyosemekana iko kwenye Google PLAYSTORE ambayo inadaiwa kuwa na uwezo wa kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi na kubaini kuwa Application hiyo haina uwezo huo. Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kuwepo kwa Application hiyo ya simu hivyo baada ya kufanya uchunguzi wa kina, Mamlaka ya Mawasiliano ilibaini...

Like
251
0
Friday, 04 December 2015
UINGEREZA YATHIBITISHA KUHUSIKA NA MASHAMBULIZI DHIDI YA IS
Global News

WIZARA ya Ulinzi ya Uingereza imethibitisha kuwa ndege za kijeshi za Uingereza zimetekeleza mashambulio ya angani dhidi ya kundi la Islamic State nchini Syria saa chache baada ya bunge kuidhinisha mashambulio hayo, Duru za serikali zimesema ndege hizo tayari zimerejea kambini katika visiwa vya Cyprus. Awali, wabunge nchini Uingereza walikuwa wamepiga kura kwa wingi kuunga mkono mashambulio hayo, wabunge 397 wakiunga mkono dhidi ya 223, baada ya mjadala mkali uliodumu saa 10 katika bunge la...

Like
188
0
Thursday, 03 December 2015
WASHUKIWA WA MAUAJI WAUAWA MAREKANI
Global News

POLISI katika jimbo la California wametaja majina ya washukiwa wawili ambao wameuawa na polisi baada ya watu 14 kuuawa kwa kupigwa risasi katika mji wa San Bernardino.   Mwanamume Syed Rizwan Farook, mwenye umri wa miaka  28, na mwanamke Tashfeen Malik, mwenye umri wa miaka 27, wameuawa kwenye ufyatulianaji wa risasi na polisi.   Mkuu wa polisi wa San Bernardino Jarrod Burguan amesema kuwa Farook alikuwa ameajiriwa na baraza la mji kwa miaka mitano. Mmoja ya ndugu wa wafiwa...

Like
228
0
Thursday, 03 December 2015
MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII IMETAKIWA KULIPA MAFAO YA WASTAAFU KWA WAKATI
Local News

MAMLAKA ya udhibiti na usimamizi wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini (SSRA) imeiagiza mifuko yote  nchini kuzingatia kanuni na sheria zinazoitaka kulipa mafao ya wastaafu kwa wakati na endapo watachelewesha malipo hayo wanapaswa kulipa fidia ili kuepusha usumbufu.   Agizo hilo limetolewa na  Mkurugenzi wa fedha na rasilimali watu wa (SSRA) Mohamed Nyasama wakati akitoa elimu kwa wanafunzi wanaotegemea kumaliza  chuo cha mipango ya maendeleo vijijini (IRDP) mjini Dodoma ambapo amesema  wastaafu wengi wamekuwa wakilalamikia usumbufu...

Like
210
0
Thursday, 03 December 2015