KAMPUNI ya Uchimbaji madini ya Geita Gold Mine leo imeungana na Watanzania kuadhimisha siku ya ukimwi duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Disemba mosi kila mwaka. Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es salaam Makamu wa Rais wa kampuni hiyo Simon Shayo amesema kuwa nchi nyingi zinazoendelea zimekuwa hazipati fedha nyingi kama ilivyokuwa mwanzoni kutoka kwa Mataifa makubwa hali inayosababisha utoaji huduma kuwa mgumu. Aidha Shayo ameongeza kuwa ndoto ya mkakati wa kutoa Elimu juu ya ugonjwa huo ni kufikia mahali ambapo...
MAMLAKA ya Mapato Tanzania-TRA-kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamekamata Makontena tisa ambayo bado haijafahamika yana vitu gani ndani katika eneo la Tangibovu Mbezi Beach Jijini Dar es salaam yaliyosafirishwa kinyume na utaratibu usiku wa manane. Akizungumza na Waandishi wa habari katika eneo la tukio Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa Mlipa kodi kutoka-TRA-Richard Kayombo amesema Mamlaka imebaini kuwa Muagizaji wa makontena hayo ni Heritage Empire Company Limited na wakala wa Forodha aliekuwa akishughulikia ni Napock Africa Company...
Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz aamuru mpira kumalizwa kwa penati kabla ya dakika 90 baada ya mchezo huo kukosa mvuto hali iliyopelekea kuchoka kuendelea kuutazama akiwa kama mgeni rasmi. Mchezo huo wa fainalii uliozikutanisha klabu za FC Tevragh-Zeina na ACS Ksar ulimalizika kwa mikwaju ya penati baada ya kuchezwa kwa dakika 63 pekee. Rais wa Shirikisho la soka nchini humo Ahmed Ould Abderrahmane amekanusha vikali na kusema kuwa maamuzi hayo yalifikiwa kwa kumhusisha marais na waalimu wa timu...
Napoli yaiengua Inter Milan kileleni mwa ligi ya Serie A baada ya Gonzalo Higuain kutekenya nyavu mara mbili na kuwalaza vijana wa Roberto Mancini waliomaliza mchezo wakiwa 10. Mshambuliaji wa Argentina Higuain alifungua mvua ya magoli katika sekunde 64 kabla ya Inter kumkosa Yuto Nagatomo aliyepigwa kadi mbili za njano. Adem Ljajic alifanikiwa kuliona lango la Napoli na kufanya matokeo ya mchezo huo kuwa...
David Moyes aonyesha nia ya kutaka nafasi ya kunoa klabu moja wapo katika bara la Ulaya. Moyes ambae alitimuliwa katika klabu ya Real Sociedad anatazamiwa kupata nafasi katika klabu nyingine. Meneja huyu wa zamani wa klabu ya Everton, 52, alitimuliwa siku moja ya kumbukumbu ya kufikisha mwaka mmoja katika ligi ya Uhispania “La Liga” Katika mahojiano yake na kituo cha BBC Moyes ameeleza matumaini yake ya kufanikiwa kuja kuwa meneja mzuri zaidi kufuatia uzoefu aliopata “La Liga”...
WAZIRI wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius amesema kufanya kazi na jeshi la Syria sio jambo wanalolizingatia hadi Rais wa Syria Bashar Al Assad atakapoondolewa madarakani. Fabius amesema ni dhahiri kuwa Rais Assad hawezi kufanya kazi na waasi wenye misimamo ya wastani nchini Syria na kwamba iwapo hataliongoza jeshi la Syria, huenda kukawa na ushirikiano baina yao wa kupambana dhidi ya ugaidi. Ufaransa inataka Assad aondolewe madarakani ikimtaja kuwa ni kiongozi anaye wauwa watu wake...
MWANAMKE mmoja amefariki huku zaidi ya wanafunzi 20 wakijeruhiwa katika oparesheni ya kuiga shambulio la kigaidi ilioendeshwa nchni kenya, katika chuo kikuu cha Strathmore. Oparesheni hiyo imepangwa na chuo hicho pamoja na maafisa wa polisi bila kuwaarifu wanafunzi na wafanyakazi, ili kubaini ikiwa chuo hicho kiko tayari kukabiliana na tukio la kigaidi. Kauli rasmi kutoka chuo kikuu cha strathmore, imethibitisha kwamba mfanyakazi mmoja amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuruka kutoka ghorofa ya...
ZAIDI ya kaya Elfu 18 katika kata nane za Halmashauri ya wilaya ya IGUNGA mkoani Tabora zitanufaika na mpango wa ruzuku za pembejeo katika msimu huu wa mwaka 2015-2016. Afisa Maendeleo ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa wilaya ya Igunga, Hossea Samaruku ameeleza hayo wakati akizungumzia hali halisi ya upatikanaji wa pembejeo za ruzuku katika wilaya hiyo. Samaruku amesema vijiji 43 vya wilaya hiyo vitashiriki kutekeleza mpango huo na kata zitakazonufaika na ruzuku ni pamoja na Nyandekwa, Nkinga na...
WATANZANIA leo wanaungana na watu wote duniania kuadhimisha siku ya Ukimwi ikiwa ni sehemu ya kupanua ufahamu kuhusu maafa yanayoletwa na ugonjwa huo. Kama ilivyo katika maadhimisho ya Uhuru, Maadhimisho ya leo hayatafanyika kama ilivyozoeleka na badala yake fedha ambazo zingetumika katika siku hiyo zitatumika kununulia dawa za kupunguza makali ya Ukimwi- ARV. Hatua hii inafuatia Agizo lililotolewa hivi karibuni na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli ambapo Katika uamuzi wake baada ya...
MAHAKAMA moja nchini Israel imewakuta waisraeli wawili na hatia ya kumuua kijana wa kipalestina mwaka wa 2014. Washtakiwa hao wawili hawakutajwa kwa majina kwani wana umri mdogo. Mashtaka ya mshukiwa wa tatu ambaye anatajwa kuwa ndiye aliyepanga mauaji hayo yameahirishwa ili kuruhusu uchunguzi wa kiakili. Kijana mwenye umri wa miaka kumi na sita Mohammed Abu Khadair alichomwa moto akiwa hai mwezi julai mwaka jana baada ya kutekwa nyara Mashariki mwa...
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ambaye yuko nchini Jamhuri ya Afrika ya kati amezuru msikiti mmoja katika mji mkuu wa Bangui. Msikiti huo wa Koudoukou uko katikati ya mji wa Bangui uliosakamwa na vita vya kidini kati ya wakristu na waislamu. Papa Francis alikutana na waislamu waliokwama katika sehemu ya mji unaojulikana na PK5, eno ambao umezingiriwa na wapiganaji wa Kikristu waliojihami vikali wa...