Slider

CECAFA: KILIMANJARO STARS YASONGA MBELE
Slider

Michuano ya Cecafa iliendelea tena hapo jana kwa michezo miwili katika hatua ya makundi, Kilimanjaro Stars wakiandikisha ushindi mwingine. Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) imeichapa Rwanda bao 2-1 katika mchezo uliopigwa mjini Awassa na kupaa kileleni mwa Kundi A wakiwa na pointi 6 kwa Mechi 2 na kujihakikishia kucheza hatua ya robo fainali. Mabao ya Kilimanjaro stars yalifungwa na Said Ndemla pamoja na Simon Msuva huku bao la Rwanda likifungwa na mchezaji Tisiyege. Zanzibar hata hivyo walifungwa 4-0 na Uganda ikiwa...

Like
385
0
Wednesday, 25 November 2015
NATO YAIUNGA MKONO UTURUKI KUTUNGUA NDEGE YA URUSI
Global News

 JUMUIA ya kujihami ya nchi za magharibi NATO imesema inasimama pamoja na Uturuki baada ya kuitungua ndege ya kivita ya Urusi.   Akizungumza baada ya mkutano wa dharura ulioitishwa na Uturuki, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema tathmini ya tukio hilo inaonyesha kuwa ndege ya kivita ya Urusi iliruka katika anga ya Uturuki.   Huku kukiwa na hali ya wasiwasi, Stoltenberge ametaka kuwepo na hali ya utulivu kutoka pande...

Like
253
0
Wednesday, 25 November 2015
WANANCHI WAMETAKIWA KUITUMIA SIKU YA UKIMWI KUPIMA AFYA ZAO
Local News

WITO  umetolewa kwa wananchi kote nchini kuyatumia maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Desemba Mosi ya kila mwaka kupima afya zao ili kudhibiti maambukizi mapya ya VVU.   Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania Dkt. Fatma Mrisho amesema  Siku ya Ukimwi Duniani nchini itaadhimishwa kwa  kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi  kupima afya zao na kupata elimu ya kujikinga  na maambukizi ya...

Like
256
0
Wednesday, 25 November 2015
SERIKALI IMESEMA HAINA KUHATARISHA USALAMA WA WANAHABARI
Local News

SERIKALI imesema haijawahi, haina na haitokuwa na nia yeyote ile ya kuhatarisha usalama wa Wanahabari na kuwa ni jambo la maana kujenga mahusiano mazuri ya kuaminiana baina ya Serikali na Wadau wa habari kwa kuwa pale ambapo uaminifu unakosekana ndipo hisia na dhana potofu zinapojitokeza. Akizungumza na Efm leo jijini Dar es salaam  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Elisante Olegabriel amesema kuwa sekta ya habari ni  muhimu  kwa kuwa inabeba sekta zingine zote za Taifa...

Like
282
0
Wednesday, 25 November 2015
MELI YA IRAN YATEKWA NYARA SOMALIA
Global News

MAHARAMIA wa Somalia wameiteka nyara meli moja ya Iran iliyokuwa na wafanyi kazi 15. Taarifa iliyotolewa na maafisa wakuu wa Somalia imeeleza kuwa Meli hiyo imetekwa nyara licha ya tahadhari iliyotolewa awali kuwa kuna uwezekano wa maharamia kuanza tena shughuli za kiharifu katika maeneo ya bahari ya Hindi. Hata hivyo imeelezwa kwamba ingawa matukio ya uharamia yamejitokeza kwenye maeneo ya bahari hiyo karibu na ufuo wa Somalia, imebainika kuwa vitendo hivyo vimepungua kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka mitatu...

Like
278
0
Tuesday, 24 November 2015
MAREKANI: KIJANA ALIYEUNDA SAA ADAI FIDIA
Global News

MVULANA mwenye umri wa miaka 14 aliyejipatia umaarufu baada ya kukamatwa kwa kupeleka saa ya kujitengenezea shuleni, anadai fidia ya dola za marekani milioni 15. Ahmed Mohammed alitiwa mbaroni na polisi wa mji wa Irving, jimbo la Texas nchini Marekani baada ya saa yake kudhaniwa kuwa kilipuzi na baadaye akafukuzwa shule. Mawakili wake wanadai dola milioni 10 za marekani kutoka kwa mji wa Irving na dola milioni5 kutoka kwa shule ya Irving Independent, wakisema Ahmed alifedheheshwa na kuathirika...

Like
284
0
Tuesday, 24 November 2015
BODI YA SUKARI IMETAKIWA KUSHUGHULIKIA MADAI YA WAKULIMA WADOGO WA MIWA KILOMBERO
Local News

KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Bi. Sophia Kaduma ameiagiza Bodi ya Sukari nchini, kushughulikia haraka madai ya wakulima wadogo wa miwa katika Kiwanda cha Sukari cha Kilombero Mkoani Morogoro ili kuleta usawa. Katika Agizo hilo, Katibu Mkuu huyo ameiagiza Bodi hiyo kukutana na Uongozi wa Kiwanda  cha Sukari cha Kilombero na  ule wa wakulima wadogo wa miwa ili kupata ufumbuzi wa kudumu kuhusu soko la miwa wanayozalisha.   Aidha, Katibu Mkuu ametoa muda wa siku saba kwa...

Like
289
0
Tuesday, 24 November 2015
MAKAMU WA RAIS MH. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA UONGOZI WA MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA LEO
Local News

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amekutana na uongozi wa Mtandao wa Wanawake na Katiba Tanzania na kuzungumzia dhamira ya serikali katika kuyatafutia ufumbuzi matatizo yanayowakabili wanawake na watoto wa kike nchini.   Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais ameueleza ujumbe huo kuwa wakati wa kampeni aliahidi pamoja na kazi za kumsaidia Rais bado kama mama atafuatilia kwa karibu utekelezaji wa ahadi ya kupatikana kwa maji safi na salama, kuboresha afya ya...

Like
768
0
Tuesday, 24 November 2015
HALI YA TAHADHARI KUENDELEZWA BRUSSELS
Global News

WAZIRI Mkuu wa Ubelgiji, Charles Michel amesema hali ya tahadhari itaendelea kubaki kwa kiwango cha juu katika mji wa Brussels. Waziri huyo amesema wasiwasi wa tishio la ushambulizi kama lililowahi kutokea siku kumi zilizopita mjini Paris bado ni mkubwa ingawa kuanzia Jumatano shule zitafunguliwa na usafiri wa treni katika mji mkuu utakuwepo. Mamlaka ya Ubelgiji imesema hadi sasa inawashitaki watuhumiwa wanne kwa kujihusisha katika shughuli zinazohusiana na...

Like
256
0
Tuesday, 24 November 2015
TISHIO LA UGAIDI: MAREKANI YATOA TAHADHARI KWA RAIA WAKE
Global News

SERIKALI ya Marekani imetoa tahadhari ya kusafiri duniani kote kwa raia wake, ikiwaonya kuwepo kwa ongezeko la tishio la kigaidi. Tahadhari hiyo imeeleza kuwa taarifa zilizopo kwa sasa zinaashiria kwamba makundi ya kigaidi ikiwemo Islamic State, Al-Qaeda na Boko Haram wanaendelea kupanga mashambulio katika maeneo tofauti. Hata hivyo, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amesema kwamba hakuna sababu ya kuamini kwamba raia wa Marekani ndio walengwa wa mashambulio...

Like
280
0
Tuesday, 24 November 2015
WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU WATAKIWA KUHUDUMIA WANANCHI
Local News

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu watambue jukumu walilonalo la kuwahudumia wananchi kutokana na majukumu ya ofisi hiyo.   Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wakuu wa Taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye mkutano uliofanyika ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es Salaam.   Mbali na hayo amewataka watumishi hao kuwa tayari kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ambayo imekuwa ikisisitizwa na Rais...

Like
307
0
Tuesday, 24 November 2015