KIONGOZI wa upinzani nchini Myanmar Bi. Suu Kyi amesema kwamba uchaguzi mkuu uliofanyika Jumapili iliyopita nchini humo haukuwa huru lakini ulikuwa wa haki. Kwenye mahojiano ya kipekee, Bi Suu Kyi aliwapongeza wananchi wa Myanmar kwa kumpigia kura ingawa Chini ya katiba ya nchi hiyo hawezi akawa rais, lakini amesema kwamba kama kiongozi wa chama atamteua rais. Uchaguz huo umechukuliwa na wengi kuwa ndio wa kidemokrasia zaidi katika kipindi cha miaka 25, baada ya miongo kadhaa ya uongozi wa...
IMEELEZWA kuwa tangu Agosti 15 Mwaka huu jumla ya Wagonjwa 106 wa kipindupindu wameshapoteza maaisha sawa na asilimia 1.3 ya idadi yote ya Wagonjwa 7825 walioripotiwa kuwa na ugonjwa huo. Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Elimu ya Afya kwa umma kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Hellen Semu amesema jumla ya Wagonjwa 53 waliokuwepo katika Manispaa ya Ilala, Temeke na Kinondoni wamepoteza maisha huku bado kukiwa na Wagonjwa katika vituo mbalimbali vinavyotumika kutibu...
IKIWA ni miaka 40 tangu kuwepo kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na jumuiya ya umoja wa nchi za ulaya, wito umetolewa kwa serikali ya Tanzania kuhakikisha inaendeleza ushirikiano na jumuiya ya umoja huo. Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaamu na balozi wa jumuiya ya umoja wa nchi za ulaya Filiberto Sebregondi wakati wa uzinduzi wa kitabu chenye kuelezea ushirikiano kwa vitendo baina ya jumuiya ya ulaya na nchi za Afrika Mashariki....
CHAD imetangaza hali ya hatari eneo la Ziwa Chad baada ya kuongezeka kwa mashambulio kutoka kwa wapiganaji wa Boko Haram kutoka Nigeria. Uamuzi huo umechukuliwa baada ya watu wawili kuuawa katika shambulio la kujitoa mhanga linalodaiwa kutekelezwa na kundi la wanamgambo hao. Boko Haram wanashukiwa kuhusika katika mauaji ya watu wawili katika kijiji kimoja nchini Chad Jumapili iliyopita na wakimbizi watatu kutoka Nigeria kaskazini mwa Cameroon...
UFARANSA imependekeza hatua kali zichukuliwe kwaajili ya kusitisha mauaji ambayo yamekuwa yakiendelea nchini Burundi. Taifa hilo liliwasilisha muswada wa mapendekezo kwa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu iliyopita likieleza wasiwasi wake juu ya hali ya usalama nchini Burundi. Ghasia zilianza mwezi Aprili baada ya maandamano ya kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania urais kwa muhula wa tatu huku ikiaminika kuwa Machafuko hayo ndiyo mabaya zaidi nchini humo katika kipindi cha miaka kumi...
BAADHI ya wazee wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza wameiomba serikali kuangalia upya utaratibu wa utoaji huduma za Afya katika hospitali ya wilaya hiyo kwani haukidhi mahitaji. Wakizungumza na Efm wazee hao wamesema kuwa tangu utaratibu wa kutolewa huduma bure kwa wazee uanze suala hilo limekuwa ni kitendawili kwao kutokana na kutopatiwa huduma hiyo kama inavyoelekezwa. Aidha wamesema kuwa serikali imefanya suala zuri la kuanzisha dirisha maalumu kwa ajili yao lakini utaratibu huo kwa baadhi ya hospitali na zahanati bado haujawa mzuri...
VYOMBO vya habari nchini vimepongezwa kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kutoa taarifa kwa wananchi hasa wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 25 mwaka huu. Pongezi hizo zimetolewa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza na viongozi wa menejimenti ya wizara na taasisi zake kwenye kikao cha kazi kilichofanyika Jijini Dar es Salaam. Profesa Gabriel amesema kuwa kipindi cha uchaguzi vyombo vya habari vimefaya kazi kubwa ya kuwapa habari za...
Na Omary Katanga Mfumo wa vilabu vinavyotajwa kuwa ni vikubwa nchini,Simba na Yanga,wa kuwa na wanachama wenye kutoa maamuzi yanayohusu klabu zao,ni wazi kuwa umepitwa na wakati kwa karne hii ya sasa katika soka lenye ushindani duniani. Mfumo huu umekuwa ukiwapa nguvu wanachama ya kufanya kile wanachotaka kwakuwa katiba za vilabu vyao vinawatambua,na ndiyo maana wakati mwingine wamekuwa wakishinikiza uongozi kufanya maamuzi yasiyofaa kwakuwa tu wanayohaki y kuamua. Ukiangalia utaratibu uliopo kwa vilabu vya bara la ulaya na maeneo mengi...
MKURUGENZI Mkuu wa kampuni ya simu ya MTN amejiuzulu kufuatia kampuni hiyo kutozwa faini kubwa ya dola bilioni 5.2 na Nigeria Mkuu huyo wa kampuni hiyo kubwa zaidi barani Afrika Sifiso Dabengwa, aliwasilisha barua ya kujiuzulu mara moja kwa maslahi ya wenye hisa na uendelevu wa kampuni hiyo. Faini hiyo ilitozwa na Tume ya mawasiliano ya Nigeria kufuatia uamuzi wa MTN kukataa kuzima namba za simu ambazo hazijasajiliwa kwa mujibu wa kanuni mpya za Taifa hilo....
IMEELEZWA kuwa nchi ya Iran imenunua silaha kali ya ulinzi dhidi ya ndege za kivita na makombora kutoka Urusi ikiwemo Mtambo wa S-300 wenye uwezo wa kudungua ndege na makombora yakiwa umbali wa kilomita 300. Hii si mara ya kwanza kwa Urusi kufanya makubaliano kama hayo na Iran ambapo Mwaka wa 2007 mataifa hayo yalikubaliana kuhusiana na mitambo hiyo ya ulinzi wa anga lakini walisitisha utekelezaji wake kufuatia marufuku iliyowekewa Iran kutokana na mipango yake ya kumiliki silaha za nyuklia....
VYAMA vya siasa nchini vimetakiwa kufanya kazi kwa kushirikiana ili kujenga umoja wa kitaifa utakaoleta mshikamano wa kudumu kati ya viongozi wa vyama hivyo na wafuasi wao. Wito huo umetolewa na diwani wa kata ya Ilala Saady Khimji kweye hafla fupi ya kuwashukuru wananchi kwa kumpa ridhaa ya kuwaongoza kupitia nafasi hiyo. Khimji amebainisha kuwa ili kuleta maendeleo katika kata ni vyema kwa kila mwananchi kuhakikisha anatoa ushirikiano wa kutosha kwenye shughuli za...