Kundi la mabaharia ambao waliachiliwa huru Jumamosi baada ya kuzuiliwa na maharamia kwa miaka mitano nchini Somalia walikula hata panya ili waishi, mmoja wao ameambia BBC. Arnel Balbero, kutoka Ufilipino amesema walikuwa wanapewa maji kidogo sana na walijihisi kama “wafu waliokuwa wakitembea” kufikia wakati wa kuachiliwa huru kwao. Mabaharia hao walitekwa wakiwa kwenye meli mwaka 2012 kwenye pwani ya Ushelisheli na wakapelekwa Somalia bara na kuzuiliwa mateka. Waliachiliwa huru Jumamosi. Taarifa zinasema waliokuwa wanawazuilia...
Waungaji mkono mswada mpya wa katiba wenye utata, wamezindua kampeini ya kuwapata wapigaji kura wengi zaidi, ili kubioresha katika kura ya maoni, itakayopigwa mnamo Octoba 30 mwaka huu, licha ya wito wa upinzani wa kuipinga. Kambi ya Ndio inayoongozwa na serikali ya Rais Alassane Ouattara, inachukulia kura hiyo ya maoni kama fursa ya kufungua ukurasa mpya wa kutanzua mzozo wa muda mrefu nchini Ivory Coast, na kutanzua maswala yenye utata ya ni nani anayefaa kuwania kiti cha Urais. Baadhi ya...
Dodoma. Vuta nikuvute iliibuka jana kwenye Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira baada ya wajumbe wake kuikataa taarifa ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kuhusu utekelezaji wa malengo ya sekta ya viwanda na biashara, wakidai imejaa porojo. Hali hiyo ilisababisha mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk Dalali Kafumu kuwaondoa ukumbini Waziri, Katibu na wataalamu waliofika hapo kwa ajili ya kutoa ufafanuzi na kujibu maswali ya wabunge. Taarifa ya maandishi ya utekelezaji wa malengo ya sekta ya...
Taifa la Burundi hatimaye limekuwa taifa la kwanza kujiondoa rasmi katika mkataba wa Roma unaosimamia mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC. Hatua hiyo inajiri baada ya rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza kutia saini sheria iliopitishwa na bunge pamoja na seneti ya kuiondoa Burundi katika mkataba huo. Wiki iliopita ,bunge la Burundi liliidhinisha mpango wa baraza la mawaziri kukata uhusiano na mahakama hiyo ya mjini Hague. Tayari mahakama ya ICC imeitaja mipango ya Burundi ya kujiondoa katika mahakama...
Dodoma. Wakati wananchi wakilalamikia fedha kutoweka mifukoni, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inatumia Sh900 bilioni kati ya Sh1.33 trilioni inazokusanya kila mwezi, kulipa madeni. Alisema hayo wakati akifungua mkutano wa waganga wakuu wa mikoa na wilaya nchini mjini hapa jana. Kauli yake imekuja wakati kukiwa na mjadala kuhusu uchumi, baadhi ya watu kusema hali inazidi kuwa mbaya wakati taasisi za Serikali zikitoa takwimu zinazoonyesha kuwa uchumi uko...
Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini na Makamu wa Rais aliyetimuliwa Riek Machar aliyesafiri na kuingia Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo yupo Afrika Kusini na kuapa kurejea nyumbani na kusema heshima yake bado ipo pale pale. Sudan Kusini imekumbwa na mapigano kuanzia mwezi julai na kufunika kabisa makubaliano ya amani yaliyomaliza vita. Makamu huyo wa zamani wa Rais Riek Machari ametupilia mbali madai kwamba yeye ndiye aliyehamasisha vita. Miezi mitatu baada ya mashambulizi ya anga na majeshi ya serikali kumlazimisha...
Mtanzania Riula Daniel amebuni mradi wa kutengeneza chakula cha mifugo kwa kutumia mende na funza badala ya kutumia soya na dagaa bidhaa ambazo zimekuwa zikipanda katika soko kufuatia mahitaji yake...
Dar es Salaam. Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr), imesema kutokana na mbu wa malaria kujenga usugu wa dawa yaPyrethroids kwa baadhi ya maeneo nchini, ugonjwa huo sasa umeanza kurudi kwa kasi hasa sehemu zilizofanyiwa utafiti na kugawa vyandarua. Akizungumza katika kongamano la 30 la Kimataifa la Wanasayansi Watafiti jijini Dar es Salaam jana, Mtafiti katika Mradi wa Amani Medical uliopo chini ya Nimr, Said Magogo alisema kufuatia tatizo hilo kituo hicho kipo kwenye mchakato wa...
Matamshi ya Jose Mourinho kuhusu uteuzi wa mwamuzi anaeshabikia Manchester United Anthony Taylor kwa mchezo wa ligi kuu England kati ya Manchester United dhidi ya Liverpool utakaochezwa leo jumatatu yatachunguzwa na Shirikisho la Mpira wa miguu nchini humo FA. Mourinho amesema itakuwa vigumu kwa mwamuzi huyo kuchezesha vizuri baada ya uteuzi wake kukosolewa. ‘Mtu mmoja akiwa na lengo anaweka shinikizo kwake’ alisema Mourinho Kwa kawaida makocha hawatakiwi kuzungumza lolote kuhusiana na mwamuzi kabla ya mchezo. FA inataka kuchunguza...
Wapokezi wa wagonjwa hospitalini wanao wahoji wagonjwa kuhusu ni kwanini wanahitaji kumuona daktari huenda yanawasababisha baadhi kutowatembelea madaktari wao , utaifiti umedhihirisha. Karibu watu wazima 2000 waliohojiwa na taasisi ya utafiti wa Saratani Uingereza, 4 kati ya 10 wamesema hawapendi kujadili magonjwa yao na maafisa wa ofisi ili kupata nafasi ya kumuona daktari. Wengi walikuwa na wasiwasi ya kupanda hamaki. Wataalamu wanasema ni lazima wagonjwa wasisitize kumuona daktari na wasikubali kuambiwa haiwezekani, iwapo wanakabiliwa na...
Mshambuliaji wa Ubelgiji Christian Benteke alifunga bao la kasi zaidi katika mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia, baada ya kufunga bao sekunde 8.1 dhidi ya Gibraltar. Mchezaji huyo wa Crystal Palace alifunga mabao matatu wakati wa mechi hiyo ya Kundi H ambayo Ubelgiji walishinda 6-0. Wafungaji wengine walikuwa Eden Hazard, Axel Witsel na Dries Mertens. Bao hilo la kwanza la Benteke pia ndilo la kasi zaidi kuwahi kufungwa na mchezaji wa Ubelgiji. Benteke alivunja rekodi ya awali ya bao...