Slider

MARAIS CHINA NA TAIWAN KUFANYA MKUTANO WA KIHISTORIA
Global News

RAIS wa China Xi Jinping anatarajiwa kukutana na Rais wa Taiwan, Ma Ying-Jeou siku ya Jumamosi.   Shirika la habari la China, Xinhua limesema kuwa mkutano huo utakaofanyika Singapore, utakuwa wa kwanza tangu viongozi wa nchi hizo mbili walipokutana mwaka 1949, baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.   Awali serikali ya Taiwan ilitangaza kuhusu mkutano huo, ikisema viongozi hao wawili watajadiliana kuhusu masuala muhimu ikiwemo kuimarisha amani kwenye eneo la Taiwan na kwamba utafungua njia mpya ya...

Like
201
0
Wednesday, 04 November 2015
WAFUGAJI WAMETAKIWA KUUZA MIFUGO KUNUNUA VYAKULA SIMANJIRO
Local News

MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amewataka wafugaji wa wilaya hiyo kupunguza mifugo yao kwa kuiuza ili wanunue vyakula kwenye wakati huu unaokabiliwa na upungufu wa chakula.   Kambona ameyasema hayo wakati akizungumzia tukio la Tarafa ya Moipo kupatiwa msaada wa chakula tani 150 za mahindi zilizotolewa na serikali kutokana na eneo hilo kukumbwa na ukame hivyo kukosa chakula. Amesema tani hizo 150 za mahindi baadhi yake zitauzwa sh500 kwa kila kilo moja na sh5,000 kwa gunia...

Like
314
0
Wednesday, 04 November 2015
VIONGOZI WA MATAIFA WATUA NCHINI KUSHUHUDIA KUAPISHWA KWA MAGUFULI
Local News

VIONGOZI mbalimbali wameanza kuwasili nchini kwa ajili ya kushiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo kesho Novemba tano.   Miongoni mwa Viongozi wanaotarajiwa kushiriki sherehe hizo ni pamoja na marais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Robert Mugabe wa Zimbabwe, Yoweri  Kaguta Museveni  wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Jacob Zuma  wa Afrika Kusini , Joseph Kabila  wa DRC, Filipe Nyusi  wa Msumbiji na  Edgar Lungu  wa Zambia.   Akiwa amevuta hisia za watu wengi hususani...

Like
275
0
Wednesday, 04 November 2015
JELA WIKI 6 KWA KUPIGA PICHA KATIKATI YA MBIO ZA F1 LANGALANGA
Slider

Kijana raia wa Uingereza ambaye aliingia katika njia ya magari yakiwa kasi Mahakama ya Singapore imemtupa jela wiki sita jela. Kijana Yogvitam Pravin Dhokia, mwenye miaka 27, aliingilia njia ya mbio za magari ili achukue picha. Alifanya tendo hilo mwezi septemba wakati wa Singapore Grand Prix. Kijana huyo alikubali kosa hilo alilolifanya katikati ya njia ya magari ya Fomula 1 ambayo yalikuwa yanakimbia kwa kasi ya 280km/h (175mph). Akitangaza hukumu hiyo, Jaji Chay Yuen Fatt alisema, kuingilia kokote njia ya...

Like
231
0
Wednesday, 04 November 2015
BOKO HARAM LAZINDUA KIWANDA CHA MABOMU
Global News

KUNDI la wapiganaji wa Kiislamu la Boko Haram limezindua kiwanda wanachotumia kuunda mabomu na silaha zingine kali Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Wachunguzi wamesema kuwa picha zilizopigwa wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho zinaonesha kuwa zilipigwa katika chuo cha kiufundi cha Bama. Haijabainika iwapo mashine hizo za chuo hicho zilinaswa na maafisa wa jeshi la Nigeria licha ya waasi hao kupigwa na kuondolewa katika maeneo mengi ya kaskazini mwa...

Like
298
0
Tuesday, 03 November 2015
NKURUNZIZA ATOA ONYO LA MWISHO KWA WAPINZANI
Global News

WAKATI Burundi ikiendelea kukabiliwa na ghasia kutoka wa upinzani baada ya kuchaguliwa kwa Rais Pierre Nkurunziza kuongoza kwa mhula wa tatu katika mazingira yenye utata, rais huyo ametoa ilani ya mwisho kwa wale aliowataja kuwa watenda mabaya kujisalimisha. Katika hotuba yake kwa Taifa, Nkurunziza amesema kuwa wale ambao hawatajisalimisha katika kipindi cha siku tano zijazo watashtakiwa kama maadui wa Taifa. Hayo yamejiri wakati mauaji yakiendelea kuripotiwa katika mji mkuu wa Bujumbura ambapo watu kadhaa wameuwawa kutokana na...

Like
243
0
Tuesday, 03 November 2015
UCHAGUZI KINONDONI MISINGI YA DEMOKRASIA ILIKIUKWA
Local News

IMEELEZWA kuwa uchaguzi wa wabunge na madiwani katika jimbo la kinondoni  uliofanyika oktoba 25 mwaka huu haukuzingatia baadhi ya misingi ya haki inayoongozwa na demokrasia ya kweli kutokana baadhi ya wagombea wa vyama mbalimbali vya siasa kutoshirikishwa katika hatua zote.   Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu mwenezi wa Taifa wa chama cha Sauti ya Umma-SAU-ambaye pia alikuwa mgombea wa nafasi ya ubunge jimboni hapo kupitia chama hicho Johnson Mwangosi wakati akizungumza na waandishi wa habari juu...

Like
256
0
Tuesday, 03 November 2015
CUF KUSIMAMA MAHAKAMANI KUPINGA MATOKEO MAJIMBO 6
Local News

KUFUATIA dosari mbalimbali zilizojitokeza katika baadhi ya Majimbo ya uchaguzi wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu Chama cha Wananchi-CUF-kinatarajia kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi wa wabunge katika majimbo sita Nchini.   Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Afisa haki za binadamu na Sheria Taifa wa chama hicho Muhamedi Mluwa amesema kumekuwa na dosari nyingi katika uchaguzi mkuu jambo ambalo limesababisha chama hicho kushindwa.   Mluwa ameyataja baadhi ya majimbo hayo kuwa ni...

Like
199
0
Tuesday, 03 November 2015
UTATA CHANZO CHA AJALI YA NDEGE MISRI
Global News

UTATA umeendelea kujitokeza katika ajali ya ndege iliyoanguka katika rasi ya Sinai huko nchini Misri na kuua abiria 224 waliokuwemo kwenye ndege hiyo. Wakati mkuu wa Mamlaka ya Anga ya nchini Urusi Aleksandar Neradko akisema kuwa ni mapema kutabiri chanzo cha ajali hiyo, lakini wamiliki wa ndege hiyo wamesema ajali imesababishwa na nguvu ya mvutano kutoka kutoka nje.   Kwa upande wake Balozi wa Urusi nchini Misri Serge Kirpichenko amesema itachukua muda mrefu kabla ya kupata taarifa sahihi kutoka kwenye...

Like
217
0
Tuesday, 03 November 2015
HATMA YA PISTORIUS KUFAHAMIKA LEO
Slider

MAHAKAMA kuu ya rufaa nchini Afrika Kusini huenda ikaamua leo hii iwapo Mwanariadha mlemavu wa miguu Oscar Pistorius amemuua kwa kukusudia au bila kukusudia mpenzi wake wakati wa sikukuu ya wapendanao mwaka 2013. Mwanariadha huyo, hivi karibuni alianza kutumikia kifungo cha nyumbani akiwa tayari amekwisha kutumikia kifungo cha mwaka mmoja kati ya miaka mitano aliyohukumiwa jela. Endapo majaji wa mahakama hiyo kuu ya rufaa watageuza maamuzi ya awali na kuwa kesi ya mauaji, Oscar Pistorius atarejeshwa tena jela na kutumikia...

Like
196
0
Tuesday, 03 November 2015
SHIRIKISHO LA VYUO VIKUU CCM LAMPONGEZA MAGUFULI
Local News

SHIRIKISHO la Vyuo vikuu la Chama cha mapinduzi-CCM-limempongeza Rais mteule wa Jamhuri  Ya Muungano wa Tanzania dokta John Pombe Magufuli kwa kushinda kiti cha Rais, ikiwa ni kielelezo cha utendaji bora aliouonyesha katika kuwatumikia watanzania kupitia nafasi alizopitia kabla ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo.   Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa shirikisho hilo Bi Zainab Abdallah amesema kuwa Rais Mteule Dokta Magufuli ndiye mtu pekee ambaye watanzania walikuwa wanamuhitaji ili aweze kuwaletea...

Like
353
0
Tuesday, 03 November 2015