TETEMEKO kubwa la Ardhi limeyakumba maeneo mengi ya kaskazini mwa Afghanistan, na kutikisa ardhi maeneo ya Pakistan na India. Idara ya Utafiti imesema kuwa Kitovu cha tetemeko hilo lenye nguvu limetikisa katika maeneo mengi yenye milima mingi ya Hindu Kush, kilomita 45 kusini magharibi mwa Jarm. Hata hivyo Maafisa wamesema tetemeko hilo lilitokea kutoka kilomita 212 ndani ya ardhi huku Nguvu za tetemeko hilo awali zimedaiwa kuwa 7.7 lakini baadaye kipimo...
KUFUATIA kukamilika kwa zoezi la upigaji kura katika maeneo mengi nchini baadhi ya vituo vimeendelea kuhesabu kura ingawa kuna ushindani mkubwa kwa wagombea wa vyama mbalimbali. Mbali na hayo hali ya usalama imeonesha kuimarishwa kwa kiwango kikubwa hali inayowawezesha wananchi kuendelea na shughuli za kawaida huku wakisubiri matokeo. Hata hivyo baadhi ya vituo vya kupigia kura vimeanza kutoa matokeo ya awali ya ngazi za Udiwani, Ubunge na Urais ingawa zimejitokeza changamoto mbalimbali wakati wa kupiga na kuhesabu...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joel Laurent kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA). Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu Jijini Dar es salaam inaeleza kwamba Uteuzi wa Mkurugenzi huyo ulianza tangu Oktoba 18, mwaka huu. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Laurent alikuwa Katibu wa Taasisi ya TEA na ndiye aliyekuwa anakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu kwa muda...
SHANGWE za muziki mnene wa 93.7 EFM bado zinaendele.Ijumaa iliyopita ilikuwa zamu ya wakazi wa Tegeta . Burudani ya aina yake ikiongozwa na timu nzima ya EFM ilishushwa ndani ya kimori high way park Tegeta , huku wakazi wa Tegeta wakikutana ana kwa ana na watangazaji na RDJ’s wa 93.7EFM. Burudani ilianza na kabumbu kati ya EFM na Boko beach veteran katika uwanja wa boko beach ambapo EFM waliibuka na ushindi mabao matatu huku Boko beach veteran wakiambulia sifuri. Muziki...
Mshindi wa shindano la kubuni neno la Khanga kupitia Uhondo Sekela Richard amekabidhiwa rasmi kitita cha Shilingi milioni moja ya kitanzania. Shindano hili liliwataka wanawake kushiriki kubuni neno la Khanga kwa kutumia neno Uhondo ambapo njia yake ya ushiriki ilijumuisha makusanyo ya maneno hayo kwa njia ya SMS hadi mshindi kupatikana. Neon lililotangazwa kuibuka na kura nyingi ni MAMA ANA UHONDO WAKE MTUNZE UPATE MEMA YAKE. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Sekela amesema utunzi wake ulizingatia kushirikisha wanawake...
WANAJESHI wa Marekani wakishirikiana na wanajeshi wa Iraq wamefanikiwa kuwakomboa mateka 70 waliokuwa wakizuiliwa na wapiganaji wa Islamic State (IS) nchini Iraq. Idara ya ulinzi ya Marekani imesema operesheni ya kuwakomboa mateka hao ilitekelezwa baada ya kubainika kwamba walikuwa karibu kuuawa. Lakini mwanajeshi wa Marekani aliyejeruhiwa kwenye operesheni hiyo amefariki na ndiye mwanajeshi wa kwanza kufariki tangu kuanza kwa operesheni ya wanajeshi wa Marekani dhidi ya IS mwaka jana. ...
RAIS wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepangiwa kukutana na viongozi wa wanafunzi wa vyuo leo kujadili maandamano ya wanafunzi yaliyosababishwa na kuongezwa kwa ada ya masomo. Wanafunzi wamekuwa wakiandamana wiki moja sasa, hasira nyingi zikielekezwa kwa chama tawala African National Congress (ANC). Jana, maelfu ya wanafunzi walikusanyika nje ya makao makuu ya ANC mjini Johannesburg wakitaka elimu itolewe kwa wote bila malipo...
CHAMA cha Mapinduzi CCM leo kitafanya mkutano wake Mkubwa wa kuhitimisha kampeni zake kwa upande wa Mkoa wa Dar es salaam katika Viwanja vya Jangwani ambapo Mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho ataongea na wananchi wa mkoa huo kwa mara ya mwisho kuomba ridhaa yao ya kumpa kura siku ya Uchaguzi. Kampeni za CCM zitafungwa Kitaifa kwa mikutano mikubwa ya kampeni katika mikoa saba ambayo ni Mwanza, Tanga, Mbeya, Kigoma, Mtwara, Kilimanjaro na Mara ambapo Mikutano hiyo...
KESI ya Kikatiba kuhusu tafsiri ya Umbali wanaotakiwa kusimama wapiga kura baada ya Kupiga kura Wakati wa Uchaguzi mkuu inatolewa hukumu yake leo ikiwa ni maelekezo maalumu. Hukumu hiyo inasomwa baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili kuhusiana na kesi hiyo yaliyotolewa hapo jana ambapo mahakama imesema itatoa maelekezo maalum kuhusu umbali wanaotakiwa kusimama wapiga kura baada ya kupiga kura siku ya chaguzi mkuu. Kesi hiyo ilifunguliwa October16 mwaka ikiiomba mahakama kuu kutoa tafsiri ya sheria ya chaguzi namba...
MAJADILIANO kuhusiana na hatua zinazoweza kuchukuliwa kimataifa kupambana na mabadiliko ya tabia nchi yamelalamikiwa kuwa yanaendelea kwa kasi ndogo . Mazungumzo hayo yanayofanyika mjini Bonn yana lengo la kupata msimamo wa pamoja kabla ya mkutano wa mwezi Desemba wa Umoja wa Mataifa mjini Paris wakati viongozi wa dunia wataamua kuhusu makubaliano yatakayofuatwa kisheria na kila taifa duniani kote. Kundi la mataifa yanayojulikana kama G77, ...
RAIS wa Afrika kusini Jacob Zuma amesema atakutana na viongozi wa wanafunzi na maafisa wa vyuo vikuu kesho Ijumaa kujadili mpango wa kupandisha ada ambao umezusha maandamano ya wiki nzima katika taifa hilo. Wakosoaji wanasema ongezeko hilo litaleta athari kwa wanafunzi Waafrika , ambao tayari ni wachache. Akizungumza leo, rais Zuma hajaweka wazi juu ya maandamano hayo hapo kabla , na jana wanafunzi walivamia viwanja vya bunge mjini Cape...