“DEAL DONE”  MZEE WENGER AMKABIDHI RASMI MIKOBA UNAI EMERY

“DEAL DONE” MZEE WENGER AMKABIDHI RASMI MIKOBA UNAI EMERY

Like
446
0
Wednesday, 23 May 2018
Sports

Unai Emery ametangazwa kuwa meneja mpya wa Arsenal na afisa mkuu mtendaji wa klabu hiyo Ivan Gazidis.

Bw Gazidis amesema Emery amepewa fursa ya kipekee ya kuongoza “sura mpya” yaklabu hiyo ya England.

Emery, 46, amejiunga na Gunners baada ya kuondoka PSG ambapo aliwaongoza kushinda ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1.

Mhispania huyo pia alishinda vikombe vya ligi mara nne akiwa na miamba hao wa Ufaransa.

Awali alikuwa meneja wa Sevilla ambapo aliwasaidia kushinda Europa League mara tatu mtawalia.

Atamrithi Arsene Wenger ambaye aliondoka klabu hiyo baada ya kuwaongoza kwa miaka 22.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *