SHIRIKA la afya ulimwenguni WHO limetangaza kwamba maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ebola katika mataifa ya Afrika magharibi yamepungua.
Wiki iliyopita, kulikuwa na zaidi ya watu 100 walioambukizwa ugonjwa huo nchini Sierra Leone, Guinea na Liberia.
Wiki hii , maambukizi mapya ya Ebola yamepungua chini ya watu 100, kwa mujibu wa shirika hilo la afya ulimwenguni.
Hata hivyo kituo cha taifa kinachohusika na suala la ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone kimesema wagonjwa wameongezeka.