Rais wa Gabon Ali Bongo ameelezwa kuwa ni mgonjwa, lakini hata hivyo kwa sasa anaelezwa kupata nafuu.
Habari zilizosambaa kuhusiana na Rais huyo mwenye umri wa miaka 59, zinasema kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi.
Alikuwa akitibiwa Afrika kusini, huku taarifa za awali zilizotolewa mwezi uliopita zikisema kuwa alikuwa akisumbuliwa na uchovu.
Hakujakuwa na taarifa zozote rasmi kuhusiana na afya ya rais tangu matangazo ya mwanzo yalipotolewa kuhusiana na afya yake kwamba amechoka na anahitaji mapumziko.
Msemaji wake Ike Ngouoni amesema Rais Bongo kwa sasa amepata nafuu.
Rais Ali Bongo alichukua madaraka ya kuiuongoza nchi hiyo kutoka kwa babab yake Omar Bongomwaka 2009, ambaye aliiiongoza nchi hiyo ya Afrika magharibi kwa zaidi ya miaka 40.
Alishinda uchaguzi wa marudio mwaka 2006, katika zoezi lililotawaliwa na ghasiana tuhuma za udanganyifu.
Mapema mwezi huu, wakati Rais Bingo yuko katika mji mkuu wa Saudia kwa matibabu, kiongozi wa upinzani nchini humo Jean Ping alijitangazia ushindi.