Richa ya kutukanwa na kudharaulika zaidi kupitia nyakati ngumu mpaka kwenye maisha ya Familia yake mchezaji huyu hakukatishwa tamaaa katika kuifikia ndoto yake.
Nyota yake ilianza kung’aa pale alipoitumikia Equatorial Guinea mnamo mwaka 2008 katika michuano ya kombe la mabingwa Afrika wanawake
Alipokuwa Mfungaji wa bao la ushindi katika ardhi ya nyumbani na kuifanya timu yake kua ya kwanza kwa kuipiku Nigeria
Hapa ndipo changamoto zilizidi kwa Anonma kutokana na uwezo wake mkubwa kiuchezaji pamoja nguvu hii ilipelekea timu pinzani zianze kumtilia mashaka ya kuwa yeye ni mwanaume
Ndipo shirikisho la soka barani Afrika lilichagua njia ya kumkagua
Anonma amenukuliwa akisema
Waliniambia nivue nguo zote mbele ya maofisa wa CAF kiukweli nilichukizwa saana na nililia saana kutokana na udhalilishaji