HATMA YA WATOVU WA NIDHAMU BADO KIZUNGUMKUTI

HATMA YA WATOVU WA NIDHAMU BADO KIZUNGUMKUTI

Like
319
0
Friday, 07 November 2014
Slider

Kamati ya utendaji ya Klabu ya Simba imekutana jana kuzungumzia suala la Wachezaji watatu waliowasimamishwa kutokana naUtovu wa nidhamu, Lakini kikao hicho kimeshindwa kutoamajibu kuhusu hatima ya wachezaji hao

Wachezaji hao ni pamoja na Shabani Kisiga, Haroun Chanongona, Amry Kiemba ambao wamesimamishwa mara baada ya mchezo wa kati ya Simba dhidi ya Tanzania prison uliopigwa katika dimba la Sokoine huko mkoani mbeya na timu hizo kwenda sare ya kufunganabao 1-1

Msemaji wa Simba Hamphrey Nyasio, Amezungumza na E.sport na kuthibitisha kufanyika kwa kikao hicho cha kamati ya utendaji

Katika hatua nyingine msemaji huyo wa Simba amekanusha taarifa ya kuwa imemtelekeza mlinda mlango wao namba mbili Husein Sharif alieumia katika mechi ya majalibio huko Afrikakusini ambapo Simba ilikwenda kuweka kambi kwaajili ya mechi ya wataniwajadi

 

Comments are closed.