Iran imefanya kosa  kubwa sana

Iran imefanya kosa kubwa sana

Like
482
0
Friday, 21 June 2019
Global News

Rais wa Marekani aliidhinisha majeshi ya Marekani kuishambulia siku ya Alhamisi na kisha kubadili msimamo, vyombo vya habari vya nchi hiyo viaripoti.

Mashambulizi hayo ilikuwa yawe ya kulipiza kisasi baada ya Iran kuitungua ndege isiy na rubani ya Marekani.

Kwa mujibu wa gazeti mashuhuri la The New York Times, tayari matayarisho ya awali ya mashambulizi hayo yalikuwa yakiendelea wakati Trump alipobadili mawazo na kuamuru yasitishwe.

Gazeti hilo linamnukuu afisa mmoja mwanandamizi wa Ikulu ya White House.

Hata hivyo bado hakuna taarifa rasmi kutoka Ikulu hiyo juu mipango hiyo ya mashambulizi.

Iran inasema ndege hiyo ya kijasusui ilikuwa ndani ya anga lake wakati wakiitungua, lakini jeshi la Marekani limekanusha na kusema ilikuwa ikipaa katika anga la kimataifa.

Tukio hilo linaendeleza suitafahamu baina ya mataifa hayo mawili hususani katika eneo la mpaka baina ya Ghuba ya Omani na Ghuba ya Uajemi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Javad Zarif amesema nchi yake itapeleka malalamiko Umoja wa Mataifa (UN) kuwa Marekani inavamia eneo lake.

Balozi wa Iran wa UN Majid Takht Ravanchi amesema ni dhahiri kuwa ndege hiyo ilikuwa inafanya operesheni ya kijasusi wakati ikitunguliwa, kitu ambacho amesema ni uvunjifu wa wazi wa sheria za kimataifa.

Katika barua aliyomuandikia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama, Bw Ravanchi amesema, Japo Iran haitaki kuingia vitani, lakini ina haki ya kujilinda dhidi ya vitisho vya maadui.

Trump amesema nini?

Rais Trump mpaka sasa hajazungumza chochote kuhusu mipango ya mashambulizi ya kulipa kisasi.

Akizungumza awali kutokea Ikulu ya White House, amesema Iran imefanya makosa makubwa kwa kuitungua ndege hiyo na kuwa kuna ushahidi kuwa ilikuwa katika anga la kimataifa na si eneo la Iran.

Hata hivyo Trump amewaeleza waandishi wa habari kuwa tukio hilo yawezekana lilisababishwa na makosa ya kibinaadamu.

“Ni vigumu sana kwangu kuamini kwamba tukio hilo lilikuwa la makusudi,” amesema Trump.

“Nafikiri, huenda Iran ilifanya kosa – Yawezekana kuna jenerali ama mtu mwengine ambaye alifanya kosa hilo la kutungua ndege ile,” amesema.

“Yawezekana alikuwa ni mtu mmoja mpuuzi (ndio alitoa amri ya kutungua).”

Viongozi wengine wamesema nini?

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya kuwa vita baina ya mataifa hayo mawili italeta janga ambalo madhara yake hayayumkiniki.

Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres amezitaka pande zinazokinzana kujizuia.

Nchini Marekani, Spika wa Bunge la Wawakilishi kutoka chama cha upinzania cha Democrats Nancy Pelosi amesema Marekani haina hamu ya vita dhidi ya Iran.

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa taifa hilo, na kinara wa kutaka tiketi ya urais kupitia Democrats, Joe Biden, amemkosoa Trump kwa kusema sera zake dhidi ya Iran ni “janga la kujitakia”.

Kiongozi wa wawakilishi wa chama tawala cha Republicans bungeni, Kevin McCarthy, ametaka kuchukuliwe hatua za kipimo baada ya kufuatia tukio hilo.

cc;BBCswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *