MAANDAMANO YAFANYIKA DRESDEN

MAANDAMANO YAFANYIKA DRESDEN

Like
200
0
Tuesday, 20 October 2015
Global News

WATU wasiopungua Elfu 15 wameandamana katika mitaa ya mji wa Dresden jana jioni, kuadhimisha mwaka mmoja tangu yalipofanyika maandamano ya kwanza ya vuguvugu la PEGIDA.

Kauli zilizokuwa zinatumiwa na miongoni mwa waandamanaji hao zilikuwa za hisia kali dhidi ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kuhusiana na msimamo wake wa kuwaunga mkono wakimbizi.

Polisi mjini Dresden imeripoti kuwa makabiliano kati ya waandamanaji wa PEGIDA ikimaanisha Wazalendo wa Ulaya dhidi ya Kusilimishwa kwa mataifa ya Magharibi,” walifanya maandamano yake ya kwanza Oktoba 20 mwaka jana.

Comments are closed.