MABAKI YA WATU 40 YAZIKWA SOMALILAND

MABAKI YA WATU 40 YAZIKWA SOMALILAND

Like
206
0
Tuesday, 25 August 2015
Global News

SHUGHULI ya kuzika mabaki ya zaidi ya watu arobaini imefanyika katika eneo lililojitangazia uhuru la Somaliland ambapo Mabaki hayo yalipatikana katika kaburi moja.

Taarifa zinasema kuwa Mifupa hiyo ya watu ilipatikana wakati mitaro ya mabomba ya maji ilipokuwa ikichimbwa katika mji mkuu Hargeisa.

Hata hivyo bado inaaminika kwamba watu hao waliuawa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotokea mwaka 1988.

Comments are closed.