Magaidi walioshambulia hoteli Nairobi wauawa

Magaidi walioshambulia hoteli Nairobi wauawa

Like
809
0
Wednesday, 16 January 2019
Global News

 

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema kuwa magaidi waliohusika kufanya shambulio la kuvamia hoteli la kifahari ya DusitD2 iliyopo nchini Kenya jijini Nairobi tayari wameuawa na operesheni imekamilika.

Hata hivyo shambulio hilo limeleta madhara makubwa ikiwemo kusababisha vifo vya watu 14 pamoja na majeruhi huku wengine 700 wakiwa wamefanikiwa kuokolewa katika janga hilo lililoikumba nchi ya Kenya siku ya jana.

Ambapo kundi la kigaidi la Al-shabaab limekiri kuhusika na shambulio hilo ambapo jana majira ya saa 9 jioni walivamia hoteli hiyo na kufanya shambulio hilo katika eneo la 14 Riverside.

Shambulio hilo la kigaidi lililotajwa kufanywa na watu sita lililohusisha milio ya risasi pamoja na mabomu yaliyotawala na kusababisha vurugu kubwa katika eneo hilo.

Aidha hali ya sasa ni shwari mara baada ya jeshi la polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama kumaliza operesheni hiyo ya kufanya jiji litulie na kuwa na amani baada ya mtikisiko huo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *