MATOKEO YA MICHEZO YA LIGI KUU TANZANIA BARA

MATOKEO YA MICHEZO YA LIGI KUU TANZANIA BARA

Like
590
0
Monday, 23 February 2015
Slider

Yanga jana ilishuka dimbani kumenyana na Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ambapo mchezo huo ulimalizika kwa vinara hao wa ligi kuu kuichapa Mbeya City 3-1 , ushindi huo unaipeleka Yanga pointi tano mbele huku mabingwa watetezi Azam fc wakishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi

Magaoli ya Yanga yalifungwa na Simon Msuva, Mrisho Ngassa na Amisi Tambwe huku bao la kufuta machozi la Mbeya City lilipachikwa na Peter Mapunda.

Katika michezo mingine ya ligi kuu hapo jana Simba ilipokea kichapo cha 1-0 kutoka kwa Stand United katika viwanja vya Kambarage, Wakati Azam fc walimenyana na Tanzania Prisons katika huko Azam Complex ambapo mchezo huo ulimalizika kwa kutoana jasho kwa kutoka na sare bila kufungana

Comments are closed.