Mtoto Mchanga Ajeruhiwa Na Chui Nchini India

Mtoto Mchanga Ajeruhiwa Na Chui Nchini India

Like
719
0
Tuesday, 31 July 2018
Global News

Mtoto mchanga wa miezi minne katika jimbo la Magharibi mwa India la Gujarat amejeruhiwa baada ya chui kumnyakua kutoka mikononi mwa mama yake.

Mtoto huyo anaendelea kupatiwa matibabu kwa majeraha aliyoyapata, pamoja na Mama yake kwani na yeye pia alijeruhiwa.

Mama huyo alikuwa amembeba mtoto wake huku akiwa ameketi nyuma ya mumewe ndani ya gari wakati waliposhambuliwa na chui huyo.

Kilio cha baba yake cha kuomba msaada kilisikika kwa wanakijiji kilichopo jirani ambao walikimbia na kumuondoa mnyama huyo.

“Walianza kupiga kelele ambazo zilimtisha chui na akaamua kumdondosha mtoto huyo ,” Afisa wa msitu aliieleza

“Tulikimbia haraka mara baada ya kubaini tukio hilo na tukaita gari la wagonjwa ,” Afisa wa misitu, ambaye alikuwa zamu wakati huo alisema.

Shabulio hilo lilitokea katika eneo lenye misitu mikubwa ambalo huwa kwa kawaida linalindwa na walinzi.

Inakadiriwa kuwa Kuna chui kati ya 12,000 hadi 14,000 nchini India na kwa wastani chui mmoja huuawa kila siku.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *