OBAMA KUWEKA HISTORIA INDIA LEO

OBAMA KUWEKA HISTORIA INDIA LEO

Like
258
0
Monday, 26 January 2015
Global News

RAIS wa Marekani Barack Obama amekuwa rais wa kwanza wa Marekani kuwa mgeni rasmi katika gwaride la siku ya Jamhuri nchini inayoadhimishwa  nchini India leo siku moja baada ya kusifu enzi mpya ya urafiki kati ya nchi hizo mbili.

Mwaliko huo wa kuhudhuria sherehe hizo muhimu za India za kuuonyesha ulimwengu uwezo wake wa kijeshi na tamaduni mbalimbali za India zinaonyesha ni kwa kiasi gani Rais Obama ana uhusiano wa karibu na Waziri mkuu wa India Narendra Modi.

Baadaye hii leo, viongozi hao wawili watawahutubia viongozi wa kampuni za kibiashara katika hafla iliyoandaliwa na baraza la biashara la Marekani na India.

Comments are closed.