POLISI WAPEWA KIZUNGUMKUTI KWENYE NYUMBA YA WATOTO WA P DIDY

POLISI WAPEWA KIZUNGUMKUTI KWENYE NYUMBA YA WATOTO WA P DIDY

Like
572
0
Friday, 30 January 2015
Entertanment

Idara ya polisi katika jiji la Loss Angels walilazimika kukimbilia kwenye nyumba ya watoto wa P Didy mara baada ya kupata taarifa ya kusikika kwa milio ya bunduki na tishio la kifo.

Polisi walipokea simu yenye kuelezea kuwa kuna barua imeachwa kwenye mlango wa nyumba hiyo yenye vitisho vya kutaka kuuwa watu wote kwenye nyumba hiyo ya mwanamama Kim Poster’s huko L.A

Maafisa hao walifika kwenye nyumba hiyo na kukuta hakuna mtu yeyote wala barua ya vitisho.

Dakika sita baada ya polisi kuondoka eneo hilo simu nyingine ilipigwa ikiripoti kuwa milio ya bunduki imesikika katika nyumba hiyo hivyo walirudi tena na kukuta hali ni shwari hapakuwa na mtu yeyote nyumbani hapo

Hali hii si ngeni katika nchi ya marekani zaidi kwa watu maarufu kama ilivyowahi kutokea kwa , Magic Johnson, Khloe Kardashian, Clint Eastwood, na Rihanna mwaka 2013

Comments are closed.