Profesa Ndalichako Asikitishwa na Matokeo ya Jangwani Kidato cha Sita

Profesa Ndalichako Asikitishwa na Matokeo ya Jangwani Kidato cha Sita

Like
533
0
Tuesday, 17 July 2018
Local News

Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako ameeleza kusikitishwa na matokeo mabaya ya Shule ya Sekondari Jangwani ambayo ni miongoni mwa zilizoshika mkia katika matokeo ya kidato cha sita.

Amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika shule hiyo lakini ni miongoni mwa shule kumi zilizofanya vibaya.

Shule hiyo kongwe na ya vipaji maalumu imeingia kwenye nafasi ya shule kumi zilizofanya vibaya katika matokeo yaliyotangazwa Julai 13, 2018 na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta).

Profesa Ndalichako amesema hayo leo Julai 17, 2018 alipozindua mfuko wa elimu wa kuendeleza ujuzi unaolenga kuboresha teknolojia.

“Serikali imekuwa ikifanya juhudi nyingi kuhakikisha shule na vyuo vyetu vinafanya vizuri, tumefanya uwekezaji wa kutosha katika vyuo na hata shule ya Jangwani ambayo imeshika mkia,” amesema Profesa Ndalichako.

Amesema Serikali inafanya juhudi kubwa kuboresha elimu ili matokeo yaonekane lakini kwa shule ya Jangwani wamesikitishwa.

Shule kumi za mwisho kitaifa ni Forest Hill ya mkoani Morogoro, Jang’ombe (Mjini Magharibi), Jangwani (Dar es Salaam), St James Kilolo (Iringa), White Lake (Dar es Salaam), Aggrey (Mbeya), Nyailigamba (Kagera), Musoma Utalii (Mara), Ben Bella (Mjini Magharibi) na Golden Ridge (Geita).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *