Rais Abdelaziz Bouteflika ajiuzulu

Rais Abdelaziz Bouteflika ajiuzulu

2
1040
0
Wednesday, 03 April 2019
Global News

Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika amejiuzulu wadhifa wake baada ya miaka 20 kufuatia wiki kadhaa za maandamano nchini mwake.

Bouteflika amekuwa madarakani kama rais kwa muda wa miaka 20 , tayari alikuwa amefutilia mbali mpango wa kugombea muhula mwingine kutawala kutokana na kukuwa kwa upinzani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika la Habari la nchi hiyo, kiongozi huyo tayari aliondoa mipango yake ya kusaka awamu ya tano madarakani, wakati upinzani dhidi ya serikali yake ukiongezeka.

Jeshi la Algeria ambalo lina nguvu, lilimtaka kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 82 kutangaza kuwa hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya uongozi.

Abdelaziz Bouteflika alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi, miaka sita iliyopita na tangu hapo mara chache amekuwa akionekana katika sehemu za umma.

Kujiuzulu kwake kulitangazwa kwa namna gani?

Rais Abdelaziz Bouteflika,aliweza kutoa taarifa hizo rasmi kwa mujibu wa katiba inayoruhusu rais kusitisha muda wake wa kutawala”

Uamuzi huo wa Rais Bouteflika ulitangazwa pia na Televisheni ya Taifa ya nchi hiyo.

Kwa nini amejiuzulu?

Msukumo wa wananchi kutaka ajiuzulu ulianza kujijenga tangu mwezi Frebruari, na kusitishwa na tangazo la rais Bouteflika baada ya kutangazwa kuwa hatawania tena nafasi ya uraisi.

Maelfu waliandamana nchini kote tarehe 1 Machi.

Bouteflika amehaidi kuhudumia kama watateuliwa katika awamu ya tano, pamoja na mabadiliko kwa waziri mkuu ambaye alishinwa kuondoka.

” Rais wa Jamhuri Bwana Abdelaziz Bouteflika, ametangaza rasmi uamuzi wake wa kumaliza kazi yake kama Rais wa Jamhuri ya Algeria, katika Baraza la Katiba. Uamuzi huo unaanza mara moja kuanzia leo..”

Kuondoka madarakani kwa kiongozi huyo pia kumekuja baada ya kiongozi wa maandamano kukataa ahadi iliyotolewa na Rais Bouteflika wiki hii kwamba atajiuzulu madarakani ifikapo Aprili 28.

Kwa nini maandamano yalikuwa?

Waandamanaji wengi ambao ni vijina wanadai kuwa wanataka mfumo mpya wa serikali.

Kuna madai kuwa Bouteflika alikuwa anatumika katika vikundi vya kisiasa , biashara na maafisa wa jeshi,

Watu wamepokeaje uamuzi wa rais huyo?

Mamia ya watu wanasheherekea katika mji mkuu wa Algiers, huku wakiwa wanapepea bendera ikiwa ishara ya furaha ya ushindi.

Selmaoui Seddik moja ya waliojitokeza barabarani kushangilia anasema ingawa amepokea kwa furaha kujiuzulu kwa Rais Bouteflika, serikali nzima inabidi kuondoka madarakani.

”… Niko nje kusherehekea kujiuzulu kwa Rais Bouteflika. Tumeondoa kisiki madarakani. Kwa mapenzi ya Mungu, tutakuwa na asilimia mia moja ya demokrasia ya mpito. Hilo ni jambo muhimu. Tunahitaji kuondoa utawala wote madarakani na hili ni jambo gumu.

Ni vigumu kulifanya kwa amani, lakini nina imani na watu wa Algeria kulifanya jambo hilo kwa amani na tukaelekea katika taasisi za uongozi na sio magenge ya wahuni, kila kitun kitakuwa sawa. Mungu atasaidia”, Selmaoui.

Abdelaziz Bouteflika ni nani?

Bouteflika aliingia madarakani mwaka 1999 na kusifiwa kwa kutokomeza vita ya wenyewe kwa wenyewe ambayo ilikadiriwa kuuwa watu zaidi ya 100,000.

Waandamanaji dhidi ya ongezeko la gharama ya chakula na ukosefu wa ajira mwaka 2011 wakati wa utawala wa kiarabu , rais huyo aliweza kutatua tatizo hilo kwa haraka.

Mara baada ya kupooza , aliweza kushinda tena uchaguzi licha ya kuwa na upinzani mkali kutoka kwa vyama vya upinzani kwa kudaiwa kuwa afya yake itamfanya ashindwe kutimiza majukumu yake.

Pamoja na ukosoaji huo bwana Bouteflika bado ana nafasi kubwa ya kushinda mwaka huu.

Upinzani nchini Algeria umegawanyika na Bouteflika alishinda uchaguzi wa awali wa urais wa mwaka 2014 pamoja na kutofanya kampeni mwenyewe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *