RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA SHEM IBRAHIM KARENGA

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA SHEM IBRAHIM KARENGA

Like
300
0
Wednesday, 17 December 2014
Local News

RAIS JAKAYA KIKWETE amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dokta FENELLA MUKANGARA kuomboleza kifo cha mwanamuziki mkongwe, SHEM IBRAHIM KARENGA kilichotokea Desember 15 mwaka huu katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam alikokuwa amepelekwa kwa matibabu ya ugonjwa wa shinikizo la damu.

Enzi za uhai wake, Marehemu KARENGA alijaaliwa kipaji cha muziki hususan upigaji wa gitaa la solo na uimbaji, kipaji ambacho kilimwezesha kufanya kazi katika bendi mbalimbali za muziki hapa nchini akianzia na Bendi ya Lake Tanganyika Jazz mwaka 1964, na baadaye Bendi Maarufu ya Tabora Jazz ikijulikana zaidi kama Wana Segere Matata.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeleza kwa Rais KIKWETE ametoa salamu za pole kwa familia ya marehemu KARENGA kwa kupoteza kiongozi na mhimili wa familia.

 

Comments are closed.