RIADHA: PUTIN AAGIZA MADAI YA DAWA YAFANYIWE UCHUNGUZI

RIADHA: PUTIN AAGIZA MADAI YA DAWA YAFANYIWE UCHUNGUZI

Like
239
0
Thursday, 12 November 2015
Slider

RAIS wa Urusi Vladimir Putin ameagiza uchunguzi ufanyike kuhusiana na madai kwamba wanariadha nchini humo wamekuwa wakitumia dawa za kusisimua misuli.

Rais Putin ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwa mara ya kwanza tangu tume huru ya shirika la kukabiliana na matumizi ya dawa za kusisimua misuli duniani (Wada) kutoa ripoti yake Jumatatu juu ya matumizi ya dawa hizo nchini Urusi.

Kwa upande wake Waziri wa michezo wa Urusi Vitaly Mutko amesema kuwa ingawa wao wanachangamoto ya kimfumo lakini mfumo wa kukabiliana na dawa za kusisimua misuli Uingereza ni mbaya zaidi kuliko wa Urusi.

Comments are closed.