Ronaldo aingia katika makubaliano na mahakama ili kukwepa kifungo jela

Ronaldo aingia katika makubaliano na mahakama ili kukwepa kifungo jela

Like
575
0
Tuesday, 22 January 2019
Sports

Nyota wa soka Cristiano Ronaldo ameingia katika makubaliano na mahakama ya Madrid kuhusu madai ya kukwepa kulipa kodi baada ya kubali kupigwa faini ya €18.8m (£16.6m) fine. makubaliano yaliofikiwa yanashirikisha kifungo cha miezi 23 jela

Jaji mmoja alikataa ombi la mchezaji huyo kuhudhuria kesi hiyo kupitia kanda ya video ama hata kuingia katika jumba hilo kwa kutumia gari ili kuzuia kuandamwa na vyombo vya habari.

Nchini Uhispania, wafungwa huwa hawahudumii kifungo cha chini ya miaka miwili.

Hali ya makosa ya Ronaldo inamaanisha kwamba hatohudumia kifungo jela.

Kesi hiyo ilichukua dakika chache baada ya Ronaldo kukubali makubaliano yaliotolewa na viongozi wa mashtaka

Mchezaji huyo wa Juventus ambaye aliichezea klabu hiyo usiku wa kuamkia mashtaka hayo aliwasili akiwa anatabasamu.

Wakili wake alikuwa amehoji kwamba kutokana na umaarufu wake , alipaswa kutotumia lango kuu la mahakama kutokana na hali ya usalama.

Ronaldo ambaye ni bingwa mara tano wa taji la Ballon d’Or na miongoni mwa wachezaji bora duniani, anatuhumiwa kwa kukwepa kulipa kodi nchini Uhispania kati ya 2011 na 2014 wakati alipokuwa akiichezea klabu ya Real Madrid wakati huo akiwa na makao yake nchini Uhispania.

Kesi hiyo inaangazia mikataba ya haki za picha zake.

Viongozi wa mashtaka wanasema kuwa fedha hizo zilipitishwa kupitia kampuni zinazotozwa kodi ya chini katika mataifa ya kigeni ili kukwepa kulipa kodi iliohitajika.

Kitita hicho kilidaiwa kuwa cha €14.8m.

Mwaka 2017, wakati madai hayo yalipochipuka, viongozi wa mashtaka walisema kuwa ulikuwa ukiukaji wa ahadi yake nchini Uhispania.

Lakini wakili wa Ronaldo alisema kuwa kutoelewana kuhusu kile kilichohitajika na kili ambacho hakikuhitajika chini ya sheria za Uhispania na kuzuia jaribio lolote la kukwepa kulipa kodi.

Ronaldo

Xabi Alonso anakabiliwa na mashtaka kama hayo

Makubaliano hayo yaliofanyika mwezi Juni mwaka uliopita yaliafikiwa na mamlaka ya ushuru nchini Uhispania.

Yatawasilishwa mbele ya jaji siku ya Jumanne mahakamani.

Jaji huyo atatangaza uamuzi wake katika kipindi cha siku zijazo.

Ronaldo sio mchezaji wa kiwango cha juu wa pekee kukabiliana na mkono wa mamlaka ya ushuru nchini Uhispania.

Mchezaji mwezake wa zamani Xabi Alonso pia anatarajiwa kuwasili mahakamani siku hiyohiyo kwa mara ya kwanza akishtakiwa na shataka kama lake la makosa ya haki za picha zake ya takriban €2m.

Katika siku za hivi karibuni:

  • Nyota wa Barcelona Lionel Messi alizuia kifungo kwa mashtaka kama hayo yanayohusisha haki za picha zake , akilazimika kulipa mamilioni kama faini na ushuru.
  • Neymar da Silva Santos Junior alikuwa katikati ya mgogoro wakati Barcelona ilipopigwa faini ya mamilioni ya fedha baada ya kushtakiwa kwa kukwepa kulipa kodi lakini akazuia kukiri shtaka hilo.
  • Mchezaji wa Real Madrid Marcelo Vieira alikiri mashtaka ya kukwepa kulipa kodi na kukubali kuondolewa kifungo cha miaka minne jela kufuatia hatua yake ya kutumia kampuni za kigeni kumpitishia takriban Yuro nusu milioni ya mapato yake.

Ronaldo pia anakabiliwa na shtaka jingine: Mchezaji huyo anatuhumiwa kutekeleza ubakaji mjini Las Vegas 2009, mashtaka ambayo anapinga.

cc;BBCswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *