SAUTI  SOL WAWEKA HISTORIA LAS VEGAS

SAUTI SOL WAWEKA HISTORIA LAS VEGAS

Like
431
0
Wednesday, 18 February 2015
Entertanment

Sauti sol ni kundi ambalo kwa sasa linafanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Afrika, ni wazi kuwa kundi hili limeanza kupata mafanikio makubwa kimuziki kwa kutambulika katika ramani ya dunia

Ukitaja orodha ya nyimbo zinazofanya vizuri kutoka Afrika mashariki basi hutoweza kuacha kutaja wimbo wa Sura yako kufuatia kuwa moja ya nyimbo zinazopendwa saana hapa Tanzania

 

Kundi hili hivi karibuni lilikuwa nchini Marekani katika ziara yao ambapo walipata nafasi ya kutumbuiza kwenye mgahawa maarufu duniani wa Hard Rock na kuwa wasanii wa kwanza kutoka Afrika kufanya show kwenye eneo hilo.

Show hiyi ilijaza umati mkubwa wa mashabiki hali iliyolazimu polisi waende kwenye mgahawa huo ili kuweza kuongoza watu.

sauti croped

 

Comments are closed.