Serikali ya Kenya ina mpango wa kuanzisha usafiri wa magari ya nyaya angani mwakani. Hayo ni kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika la huduma za kivuko cha feri nchini Kenya – Bakari Gowa. Gowa ameeleza kwamba tayari magari hayo yataanza kutengenezwa mwezi ujao huko Ujerumani. “Itachukua kama mwaka mmoja hivi magari hayo kutengenezwa kisha yataletwa Kenya mwaka ujao yaanze kazi ya kubeba watu angani kuwavukisha katika kivuko cha Likoni,” anasema Gowa. Je, magari haya ya nyaya yatasafirisha watu vipi?...
Mradi wa reli mpya ya kisasa nchini Kenya SGR umesababisha hasara ya $100m (£76m) katika kipindi cha mwaka wa kwanza wa operesheni zake , kulingana na wizara ya uchukuzi nchini humo. Mradi huo uliofadhiliwa na serikali ya China ambao unaunganisha mji wa pwani wa Mombasa na Nairobi ulifadhiliwa kwa mkopo wa kima cha $3bn kutoka kwa benki ya China ya Exim katika kipindi cha miaka 15. Serikali ya Kenya ilipinga madai kwamba bei ya ujenzi wa mradi huo wa reli...
Mtu aliyetuhumiwa kwa kuuza nyama ya paka wauzaji sambusa amehukumwa kifungo cha miaka mitatu na mahakama ya Nakuru Hakimu mkuu Benard Mararo alimhukumu James Mukangu Kimani baada ya kukiri kosa hilo alipowasili katika mahakama hiyo siku ya Jumatatu. Bwana Kimani alishtakiwa kwa kuchinja na kuuza nyama ya paka kwa wateja wake mnamo mwezi Juni 24 mjini Nakuru. Alishtakiwa kwamba alimchinja paka kwa matumizi ya binaadamu kinyume na sheria ya chakula , dawa na kemikali. Mwanamume huyo alikamatwa Jumapili ambapo inadaiwa...
Wizara ya Elimu nchini Kenya imeivunjilia mbali bodi ya usimamizi wa shule ya Moi Girls na kutangaza kwamba ni marufuku kuwatembelea watoto shuleni baada ya mapumziko ya katikati ya muhula kwa shule zote za upili za umma. Hii ni kufuatia uchunguzi unaoendelea kubaini kesi ya ubakaji wa mwanafunzi katika shule hiyo. Waziri wa Elimu nchini Amina Mohammed alitoa agizo kwa maafisa katika wizara yake wafanye upya ukaguzi wa usalama katika shule zote kuepuka uwezekano wa wanafunzi kuingiliwa. Mwalimu mkuu katika...
Nchini Kenya Wamama wameandamana leo mjini Nairobi kulalamika tuhuma za mwanamke mwenzao kufukuzwa eneo lake la kazi (Mgahawani) kwa sababu alinyonyesha mtoto wake akiwa kazini, jambo ambalo liliinua hasira kwa wakina mama wengi nchini humo na kufikia hatua ya kuanza kuingia barabarani wakielekea katika mgahawa huo, ambako mama huyo anatuhumu kuwa aliambiwa ajifunike wakati anamnyonyesha mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja. Mama huyo alieleza kwamba yeye alipokuwa ananyonyesha mtoto wake aliambiwa akanyonyeshee chooni, jambo lililomfanya...
Zaidi ya watu 40 wamefariki na maelfu wengine wameachwa bila ya makaazi wakati bwawa moja mjini Nakuru nchini Kenya lilipovunja kuta zake Jumatano usiku. Shirika la kupambana na majanga nchini Kenya linasema watu wengine wengi hawajulikani waliko kufikia sasa. Eneo hilo la Solai katika kaunti ya Nakuru Kenya, lina mabwawa saba yanayotumika katika kilimo cha umwagiliaji. Waziri wa mambo ya ndani Kenya Fred Matiang’i amesema serikali imeanzisha uchunguzi kubaini uthabiti wa mabwawa mengine sita yaliosalia. Maafisa wa uokozi kutoka...
Wanasayansi wa anga za juu kutoka Kenya waliokiunda chombo hicho tayari wako katika makao ya Uchunguzi wa Sayansi ya Anga za juu nchini Japan, (JAXA) ambapo chombo hicho kitarushwa kutoka huko. Nchini Kenya kwenyewe raia wataweza kufuatilia shughuli hiyo moja kwa moja kwenye mtandao wa You Tube, na sherehe maalumu ya kushuhudia imeandaliwa katika chuo kikuu cha Nairobi. Satelaiti hiyo ndogo ni ya thamani ya dola milioni moja – gharama inayoonekana kuwa ndogo kifedha kwa kiwango cha sayansi ya anga...