TFF YATANGAZA DHAMIRA YA KUVIKATA VILABU VYA LIGI KUU ASILIMIA TANO YA FEDHA

TFF YATANGAZA DHAMIRA YA KUVIKATA VILABU VYA LIGI KUU ASILIMIA TANO YA FEDHA

Like
261
0
Friday, 03 October 2014
Slider

Kamati ya utendaji ya shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF,jana tarehe 2 oct imetamka hadharani kuwa inadhamira ya kweli ya kuvikata vilabu vya ligi kuu asilimia 5 ya fedha za mdhamini,na kwamba yeyote anayepinga agizo hilo anajisumbua.

Hatua ya tff,kujitokeza hadharani kutoa msimamo wake,imekuja baada ya umoja wa vilabu kumteua mwanasheria atakayewakingia kifua kupinga agizo hilo,ambalo wanaliona kama unyonyaji kwenye kiasi kidogo wanachokipata toka kwa mdhamini wa ligi.

Tayari kwa upande wake bodi inayosimamia ligi kuu na ile ya daraja la kwanza Tanzania bara,imeshaweka wazi kuwa msimamo wake ni kutaka vilabu hivyo visikatwe hiyo asilimia tano kama tff inavyotaka.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za shirikisho,rais wa tff Jamal Malinzi,amesema bodi ya ligi itake isitake ni lazima kutekeleza agizo hilo la kuvikata vilabu asilimia tano ya fedha toka kwa mdhamini.

Comments are closed.