UBAGUZI WA RANGI: SOULEYMANE SYLLA ADAI FIDIA

UBAGUZI WA RANGI: SOULEYMANE SYLLA ADAI FIDIA

Like
412
0
Friday, 24 July 2015
Slider

Mfaransa mweusi, mwenye asili ya Mauritania, ambaye alitukanwa kutokana na rangi yake ya mwili na mashabiki wa timu ya Chelsea kwenye kituo cha treni mjini Paris mwezi February, amesema kuwa anataka waliomtusi waletwe kutoka Uingereza ili washtakiwe kwenye mahakama ya Ufaransa.

Mkanda wa video ulioonyesha kundi la mashabiki wakimzuia Bwana Souleymane Sylla kupanda treni huku wakipiga mayowe wakisema “sisi ni wabaguzi wa rangi na hivyo ndivyo tunavyopenda”.

Katika mahojiano na BBC, Souleymane Sylla alisema: “nataka fidia kwangu na kwa familia yangu”.

ch

” Wanangu wamefadhaishwa- mimi pia lakini ni athari kwa watoto wangu ndio inaumiza zaidi . ”Bado sijaridhika . Nataka waletwe kutoka Uingereza wapelekwe mbele ya sheria katika nchi yangu.”

Mashabiki hao wanne walipigwa marufuku kuhudhuria mechi za soka kwa miaka mitanokatika kesi iliyoamriwa nchini Uingereza Jumatano wiki hii. Watu hao hawajawahi kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu nchini uingereza kuhusiana na tukio hilo.

 

Comments are closed.