VYOMBO VYA HABARI VIMETAKIWA KUWA NA MADAWATI YA HABARI ZA MAHAKAMA

VYOMBO VYA HABARI VIMETAKIWA KUWA NA MADAWATI YA HABARI ZA MAHAKAMA

Like
200
0
Friday, 27 November 2015
Local News

VYOMBO vya habari nchini vimetakiwa kuwa na madawati ya habari za Mahakamani, ili kuboresha uandishi wa habari hizo.

 

Hayo yamebainishwa na Jaji kiongozi wa Mahakama kuu ya Tanzania Shaaban Lila alipokuwa akizungumza na wanahabari wakati wa kufunga semina ya mafunzo ya uandishi wa habari za mahakamani ambapo amesema  pindi mtuhumiwa anapopandishwa  kizimbani  vifungu vya sheria ndivyo vinavyotumika kwa kuzingatia aina ya makosa ya mtuhumiwa.

 

Amewataka wanahabari kutoa taarifa kwa kuzingatia hukumu iliyotolewa badala ya wao kuhukumu kwani kufanya hivyo ni makosa kisheria.

 

Comments are closed.