WABUNGE WA KENYA WARUSHIANA NGUMI BUNGENI NA KUCHANIANA NGUO

WABUNGE WA KENYA WARUSHIANA NGUMI BUNGENI NA KUCHANIANA NGUO

Like
364
0
Thursday, 18 December 2014
Global News

WABUNGE Nchini Kenya wametofautiana vikali bungeni na kuvuana mashati huku wakirushiana ngumi kufuatia mjadala kuhusu mswaada tatanishi wa usalama ambao wabunge wa upinzani wanasema unakiuka uhuru wa Wakenya.

 

Bunge limelazimika kuahirisha vikao vyake kwa dakika 30 badala ya kujadili mswada tatanishi kuhusu usalama wa nchi. Kikao cha leo kilikuwa kikao maalum ambacho kilipaswa kupitisha mswada huo ambao baadaye utaidhinishwa na Rais kuwa sheria.

KENYA3

 

Mwenyekiti wa kamati ya usalama wa bunge, Bwana Asman Kamama, alijaribu kufaya mabadiliko yaliyopendekezwa kwenye mswada huo lakini wabunge walianza kuimba na kumzomea spika wa bunge wakiukataa mswada huo wakisema ‘bado mapambano.

 

Mswada huo ambao umewasilishwa bungeni kufuatia matukio ya utovu wa usalama na mashambulizi nchini Kenya, unapendekeza kuwa washukiwa wa Ugaidi wanaweza kuzuiliwa kwa mwaka mmoja huku polisi wakifanya uchunguzi.

KENYA2

 

Ikiwa mswada huo utapistihwa kuwa sheria, mashirika ya habari yatatozwa faini ya hadi shilingi milioni 5 kwa kuchapisha taarifa au picha ambazo zinaleta hofu na kusababisha vurugu.

 

Rais Kenyatta amekuwa akikabiliwa na shinikzo la kuimarisha usalama wa tangu mashambulizi ya Septemba mwaka 2013 katika jengo la maduka ya kifahari la Westgate mjini Nairobi ambapo watu 67 waliuawa.

 

Comments are closed.