Local News

NSSF YATOA MILIONI 2 KWA FAMILIA YA MAREHEMU GURUMO
Local News

MFUKO WA TAIFA wa Hifadhi za Jamii nchini-NSSF umetoa Shilingi Milioni 2 kwa familia ya ya Marehemu MUHIDINI GURUMO ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuthamini mchango wa marehemu Enzi za Uhai wake kupitia shughuli zake za Muziki. Akiwasilisha fedha hizo kwa Familia ya ya Marehemu GURUMO leo jijini Dar es salaam Afisa Uhusiano Mwandamizi wa mfuko huo JUMA KINTU amesema fedha hizo zitakuwa chachu ya kuiwezesha Familia ya marehemu GURUMO kujiletea Maendeleo na Kuisadia...

Like
326
0
Tuesday, 30 December 2014
MAJAMBAZI YAMJERUHI MWALIMU KWA MAPANGA GEITA
Local News

MWALIMU MKUU wa Shule ya Msingi ya Nyanguku iliyopo Halmashauri ya Mji wa Geita FRANCIS KATOTO amejeruhiwa baada ya kukatwa mapanga na watu wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi. Tukio hilo limetokea usiku baada ya Majamzani hao kuvamia nyumba ya Mwalimu huyo na kupora...

Like
418
0
Tuesday, 30 December 2014
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI ATEMBELEA MIRADI YA UMEME MARA
Local News

WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa SOSPETER MUHONGO ametembelea Miradi ya umeme katika Vijiji mkoani Mara. Lengo la kutembelea Miradi hiyo ni kuhakikisha inakamilika mapema mwakani. Akizungumza wakati wa ukaguzi huo Profesa MUHONGO amesema Serikali imeamua kupeleka umeme Vijijini kwa lengo la kufuta Umasikini ikiwa ni pamoja na kuboresha Sekta ya Elimu kwa Shule za Sekondary za Kata ambazo ndio mkombozi kwa wananchi wengi wanaoishi...

Like
308
0
Tuesday, 30 December 2014
JUKWAA LA KATIBA LAWATAKA WANANCHI KUISOMA NA KUILEWA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA
Local News

Jukwaa la Katiba Tanzania-JUKATA limewataka wananchi kuisoma na kuielewa Katiba iliyopendekezwa huku wakilinganisha na Rasimu ya Katiba ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 sanjari na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania HERBRON MWAKAGENDA amesema ili kufanikisha hilo Serikali inatakiwa iwezeshe upatikanaji wa nakala za kutosha za Katiba inayopendekezwa na Rasimu ya katiba ya Tume ya Mabadiliko...

Like
351
0
Monday, 29 December 2014
WANAUME WAASWA KUSHIRIKI KATIKA MALEZI
Local News

WAZAZI hususani wakina baba wameaswa kushiriki katika Malezi ya Watoto ili wawajenge watoto na wakue katika fikra bora zitakazowapa amani, furaha na matumaini ya maisha yao. Hayo yamesemwa leo na Afisa Uhusiano wa Shirika linaloshughulikia Masuala ya watoto la SAVE THE CHILDREN INTERNATIONAL ELLEN OTARU OKOEDION wakati akizungumza na EFM juu ya namna Wazazi wanavyoweza kumlea mtoto katika malezi...

Like
260
0
Monday, 29 December 2014
JAMII YATAKIWA KUKUMBUKA WATOTO WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU NA HATARISHI
Local News

JAMII YA WATANZANIA imeaswa kuikumbuka Jamii ya Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na hatarishi waliopo katika vituo mbalimbali nchini kwa kukaa nao ili kuwapa matumaini na kuwarejeshea furaha. Wito huo umetolewa na hivi karibuni na Mkurugenzi wa Kampuni ya Communication Media ROBERT FRANCIS wakati akizungumza na Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishiwakati wa Kampeni ya Ushindi inayowakutanisha Watoto Yatima zaidi ya...

Like
434
0
Monday, 29 December 2014
WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGIA MIRADI YA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU
Local News

WATANZANIA wametakiwa kuchangia miradi mbalimbali inayolenga kuboresha sekta ya Elimu. Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Mradi wa Vitabu Vya Watoto Tanzania PILI DUMEI wakati akielezea mradi huo. DUMEI amebainisha kuwa Mradi huo unalenga lkuleta mabadiliko mbalimbali hasa kwa Jamii ya wanaopenda kusoma...

Like
307
0
Monday, 29 December 2014
WANANDOA WAUAWA KIKATIRI MARA
Local News

WANANDOA wawili akiwemo mwanaume ambaye ni Mlemavu wa Macho wameawa kwa kukatwatwa mapanga na watu wasiojulikana na kisha kuchukuliwa baadhi ya viungo vyao katika kitongoji cha Mwabasabi,Wilayani Bunda Mkoani Mara. Wanandoa hao wameuawa saa mbili Usiku wakati wakitoka maeneo ya katikati ya kijiji hicho kusaga Nafaka. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara PHILIPO KALAGI amethibitisha kutokea kwa tukio...

Like
271
0
Friday, 26 December 2014
WAKAZI WA KIMARA BARUTI WAMO HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MRIPUKO
Local News

WAKAZI WA KIMARA Baruti Jijini Dar  es salaam wapo hatarini kukumbwa na Magonjwa ya Mripuko baada ya eneo wanalohifadhia taka  kujaa. Wakizungumza na EFM wakazi hao wamesema kuwa hapo awali walikuwa wakiweka taka hizo katika magari ya kuzolea taka lakini cha kushangaza magari hayo hayapiti hali inayowapelekea kukaa na taka hizo majumbani huku wengine wakizipeleka eneo la kilungule kwa ajili ya kutupa. Wameeleza kuwa tarari wameshatoa taarifa kwa Uongozi wa Serikali ya Mtaa ili kutatua tatizo hilo lakini cha kushangaza mpaka...

Like
344
0
Friday, 26 December 2014
WASICHANA ZAIDI YA 100 WAPOKELEWA KATIKA KITUO CHA SERENGETI TUNAWEZA
Local News

WASICHANA zaidi ya 100 wamepokelewa katika kituo cha Mpango Serengeti Tunaweza Bila Ukatili wa Kijinsia,HIV Aids na Ukeketaji. Mratibu wa Mpango huo RHOBI SAMWEL amethibitisha hilo kwa njia ya Simu wakati akiongea na EFM Wilayani Serengeti mkoani Mara. Amesema Wasichana hao wamepokelewa kuanzia Desember 6 mwaka huu ambapo wamekimbia kukwepa msimu wa Ukeketaji ambao hufanyika kila...

Like
277
0
Thursday, 25 December 2014
VIONGOZI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO NA KUACHA ITIKADI ZA KISIASA
Local News

 VIONGOZI nchini wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano na kuacha Itikadi za Kisiasa kwani wananchi wanahitaji kuona viongozi wanatatua kero zinazowakabili katika maeneo yao. Akizungumza na EFM leo Mwenyekiti mpya wa Mtaa wa Mtambani Kata ya Vingunguti kupitia Chama Cha Wananchi -CUF MOHAMED MTUTUMA amesema kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongozi kutoshirikiana na viongozi wa vyama vingine na kujisahau kuwa wanapaswa kuwatumikia wananchi pasipo kuangalia Itikadi...

Like
257
0
Thursday, 25 December 2014