Local News

WAKAZI WA BANANA WAMO HATARINI KUKUMBWA NA MAGONJWA YA MLIPUKO
Local News

WAKAZI  na  wafanyabiashara  wa  eneo  la banana  jijini Dar es Salaam  wameiomba halmashauri ya  manispaa  ya Ilala  kuondoa  dampo  la taka  ambalo  siyo rasmi ambazo  zinatupwa  kandokando  ya  barabara ili  kuweza kuzuia  magonjwa  ya  mlipuko. Takataka  hizo  ambazo  zimewekwa  katika  eneo  ambalo siyo rasmi  zimekaa  kwa  muda  mrefu bila  kuondolewa  hali  inayosababisha eneo  hilo  kuwa  na harufu  mbaya  kwa  wakazi  hao. Hayo  yamesemwa  leo  jijini Dar es Salaam  na  baadhi  ya...

Like
316
0
Monday, 15 December 2014
CHAGUZI SERIKALI ZA MITAA ZANGIA DOSARI
Local News

UCHAGUZI wa Serikali za Mitaa katika sehemu kubwa nchini umeshindwa kufanyika kwa sababu mbalimbali,zikiwemo za kutofikishwa kwa Vifaa vya kupigia kura Vituoni. Wakati maeneo mengine uchaguzi huo licha ya kufanyika ,umetawaliwa na Vurugu ambazo baadhi ya vurugu hizo zimetokana na utaratibu mbovu uliopo katika kituo husika. Pamoja na hayo Wananchi walio wengi wameilalamikia Serikali kwa kushindwa kuweka utaratibu mzuri wa kupiga kura hivyo wananchi wanaamini kutakuwa na hujma ndani...

Like
253
0
Monday, 15 December 2014
KAULI YA KIKWETE KUVUNJA UKIMYA ESCROW
Local News

 MUDA wowote kuanzia leo Rais JAKAYA KIKWETE atatoa na kutangaza uamuzi wake kuhusiana na baadhi ya Watendaji wakiwemo Mawaziri kuhusishwa katika kashfa ya Akaunti ya Tegeta ESCROW. Wiki iliyopita Rais KIKWETE alipokea na kuanza kuipitia Ripoti,Nyaraka na Ushauri uliotolewa katika maazimio ya Bunge kuhusu Akaunti ya Tegeta ESCROW. Rais KIKWETE ambaye ameanza kazi rasmi Desember 8 mwaka huu, baada ya mapumziko kutokana na upasuaji aliofanyiwa mwezi uliopita amesema atatoa uamuzi wake ndani ya wiki hii....

Like
306
0
Monday, 15 December 2014
MAMA SALMA KIKWETE AWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA
Local News

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa –NEC, ya Chama Cha Mapinduzi –CCM, kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete amewataka wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika  uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii. Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa rai hiyo wakati akiongea na wanachama pamoja na wagombea wa nafasi za Uenyeviti na Wajumbe wa Serikali za mitaa katika kata za Ndoro...

Like
415
0
Friday, 12 December 2014
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI YAJENGA MAABARA 138
Local News

  HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imefanikiwa kujenga maabara 138 ikiwa ni agizo la Rais JAKAYA KIKWETE la kutaka kila shule za Kata ziwe na Maabara. Hayo yamebainishwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mhandisi MUSA NATTY wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa wafanyakazi waliofanya vizuri wakiwamo wasimamizi wa Maabara hizo. Mhandisi NATTY ameeleza kuwa kwa kiasi kikubwa wametimiza agizo la rais kwani awali walikuwa na maabara 12 na vyumba 126 hivyo kufanya idadi ya maabara...

Like
274
0
Friday, 12 December 2014
VIDEO: EFM YAWAASA VIJANA KUSHIRIKI CHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA
Local News

  Vijana wa  TANZANIA  wameaswa kujitokeza kwa wingi kushiriki Chaguzi mbalimbali hususani huu wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Desember 14 mwaka huu ili kupata viongozi bora kwa manufaa ya Taifa. Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa EFM Radio FRANCIS SIZA wakati wa mahojiano katika kipindi cha Joto la Asubuhi ambapo amesema kuwa ni wakati muafaka kwa vijana kutumia fursa hiyo kuchagua viongozi watakaosaidia nchi kufikia katika malengo ya kuwa na maendeleo pamoja na uchumi Imara. Amewaomba watanzania...

Like
247
0
Friday, 12 December 2014
RAIS JAKAYA KIKWETE ATEUA WAKUU WA TAASISI TOFAUTI SERIKALI NA MAHAKAMA
Local News

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Laurence Nyasebwa Mafuru kuwa Msajili wa Hazina kuanzia tarehe 5 Novemba, 2014. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imeeleza kuwa kabla ya uteuzi wake, Bwana Mafuru alikuwa Mkuu wa Idara ya Rasilimali Fedha katika Ofisi ya Rais inayohusika na ufuatiliaji Miradi ya Matokeo Makubwa Sasa -PDB. Aidha Bwana Mafuru pia alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Benki ya FBME iliyowekwa chini ya uangalizi wa...

Like
222
0
Friday, 12 December 2014
LOWASSA: SERIKALI YA KIKWETE IMEFANYA MAKUBWA
Local News

MBUNGE WA MONDULI na waziri Mkuu wa zamani Mheshimiwa EDWARD LOWASSA amesema Serikali ya Awamu ya Nne inayoongozwa na Rais JAKAYA KIKWETE imefanya makubwa ikiwa ni pamoja na usambazaji Umeme na Maji Vijijini. Mheshimiwa LOWASSA ameeleza hayo wakati akizungumza katika Mkutano wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Viongoji huko Bwawani Mto wa Mbu Wilayani Monduli. Amebainisha kuwa haijawahi kutokea Serikali ya Rais KIKWETE imefanya makubwa katika Umeme, Barabara na Maji na kwamba wakati akiwa Waziri wa Maji...

Like
243
0
Friday, 12 December 2014
AU: YAKUTANA DAR LEO
Local News

UMOJA WA AFRICA na nchi zake 13 ikiwemo Tanzania zimekutana leo nchini kujadili mpango wa muda mfupi wa kukabiliana kwa haraka na migogoro na majanga yanayojitokeza wakati wowote Africa ACIRC.  Mpango huo wa ACIRC uliounda jeshi la Afrika la kukabiliana kwa haraka na migogoro na majanga yanayojitokeza wakati wowote kupitia zoezi la utulivu, Africa imelenga kutimiza malengo ya nchi za umoja huo kwa kupima uwezo wa kutatua matatizo yake yenyewe   ambapo kwa mwaka huu Tanzania imekuwa mwenyeji wa hafla hiyo....

Like
206
0
Thursday, 27 November 2014
MUHONGO AWASILISHA HOJA YA MKATABA KATI YA IPTL NA TANESCO
Local News

WAZIRI WA NISHATI na Madini Profesa SOSPITER MUHONGO amewasilisha hoja yenye maelezo juu ya mkataba uliowekwa kati ya kampuni ya –IPTL-na shirika la umeme nchini Tanesco ambapo amesema kuwa taarifa iliyotolewa na kamati  ya  hesabu za serikali na mashirika ya umma- PAC- haina ukweli wowote kwa kuwa fedha za –ESCROW– siyo fedha za umma. Akiwasilisha hoja hiyo leo Bungeni mjini Dodoma Profesa MUHONGO amesema kuwa ingawa kiasi hicho cha fedha za –ESCROW- siyo za umma pia hakuna ukweli wowote juu...

Like
193
0
Thursday, 27 November 2014
WAZAZI KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA ELIMU
Local News

WAZAZI nchini  wameshauriwa kuwekeza katika sekta ya  elimu  ili kuweza kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo hasa kwa  baadhi ya shule za msingi nchini. Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na mtabibu wa tiba mbadala Abdalah Mandai wakati akizungumza na kituo hiki juu ya changamoto mbalimbali za sekta ya elimu nchini. Amesema kuwa baadhi ya shule za msingi zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati pamoja na vyumba vya madasara kitendo kinachochangia wanafunzi kusoma huku wakiwa wamekaa chini na...

Like
205
0
Thursday, 27 November 2014