WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea uharibifu wa makusudi wa miundombinu ya barabara na majengo unaofanywa na baadhi ya wananchi na kuwataka waache tabia hiyo mara moja. Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Alhamisi, Mei 17, 2018) Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge wa Magu, Bw. Kiswaga Destery aliyetaka kujua Serikali inachukua hatua gani dhidi ya wananchi wanaoharibu miundombinu ili wakauze kama vyuma chakavu kwa vile Serikali inatumia fedha...
TGNP Mtandao imeanzisha kijiwe maalum cha hedhi kwa wanawake ili kuwawezesha watoto wa kike shuleni kujadili juu ya mwenendo wa hedhi salama. TGNP Mtandao imefikia uamuzi huo wa kuanzisha kijiwe cha hedhi baada ya kubaini uwepo wa watoto wengi wa kike kushindwa kupata taarifa sahihi juu ya afya ya uzazi na hedhi salama, jambo linalochangiwa na baadhi ya mila na desturi potofu. Akizungumza jana katika kijiwe kilicho wakutanisha wanafunzi wa shule za mbalimbali za Dar es Salaam, Meneja wa Idara...
Mwenyekiti wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Harbinder Singh Sethi ameondolewa katika nafasi yake ya uenyekiti na bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo, baada ya kushindwa kuhudhuria vikao vya bodi kwa miezi sita mfululizo tangu Juni 16, 2017. Vilevile, Sethi ameondolewa katika orodha ya wakurugenzi wa bodi ya kampuni hiyo kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao bila ruhusa ya wakurugenzi wa kampuni hiyo. Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa IPTL,...
Mtu na mpenzi wake , wakazi wa wilaya ya Igunga, Tabora wameng’atwa na fisi kichakani walipotaka kufanya Mapenzi. katika tukio hilo mwanamke Mwajuma Masanja (37) Mkazi wa kijiji cha Iduguta , alifariki baada ya kushambuliwa viabaya na fisiw huyo huku mpenzi wake , Shija Maneno (35) Akijeruhiwa vibaya wakati akimuokoa mpenzi wake....
Ni vita kubwa leo jiji Mbeya, ambapo pale wafalme wawili katika jiji hilo, Mbeya City na Tanzania Prisons. Watakapokutana kwenye mchezo wa ligi kuu kutafuta point 3. Mbeya City wanaingia katika mchezo huo wakiwa wameachwa alama 15 na Tanzania Prisons walio na 44 kwenye msimamo wa ligi. Wakati huo Mbeya City wao wamejikusanyia jumla ya pointi 29 pekee katika michezo 27 waliyocheza msimu huu. Taarifa kutoka jijini Mbeya zinaeleza wadau na mashabiki wengi wanausubiria kwa hamu mchezo huo...
Leo ni siku ya Mama duniani hivyo EFM inatambua mchango mkubwa uliotokana/ unaotokona na Mama na tunaungana na kina mama wote kuwatakia siku yao #Wish you Happy Mother’s...
Mvua kubwa imekuwa ikinyesha maeneo mengi Afrika Mashariki na kusababisha uharibifu wa mali na vifo. Nchini Kenya, watu zaidi ya 10 wamefariki baada ya kusombwa na maji ya mafuriko Wengi wao wamefariki wakisafiri kuelekea nyumbani au wakiwa kwenye magari wakijaribu kupitia maeneo yaliyofurika Je, unaweza kujikinga vipi hasa ukiwa safarini? Maafisa wa Mamlaka ya Taifa ya Usalama Barabarani (NTSA) pamoja na Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya wametoa ushauri ambao unaweza kukufaa sana wakati huu wa mvua. Fahamu kwamba wakati wa...
Mbeya. Viongozi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti, Freeman Mbowe waliokwenda Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya kuwalaki Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wamepigwa butwaa baada ya kuelezwa na askari magereza kwamba wameshatoka. Wakiwa nje ya gereza leo Mei 10, 2018, viongozi hao walifuatwa na askari na kuelezwa kwamba wawili hao wameshatoka. Magari mawili ya polisi yaliyokuwa yameimarisha ulinzi gerezani hapo nayo yaliondoka. Happiness Msonge, mkewe Sugu...
AJALI : Watu 3 wamefariki dunia na wengine 5 wamejeruhiwa katika ajali ambayo imetokea jioni hii eneo la Boko Magengeni Manispaa ya Kinondoni ajali hiyo imehusisha magari matatu ikiwemo gari la kubebea michanga na basi la wanafunzi Mkuu wa Trafiki Wilaya ya Kawe Inspekta msaidizi wa Polisi Makame akizungumza na TV E,/ Efm habari amethibitisha na kusema miili ya Marehemu imepelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Mwananyamala ambako pia majeruhi wamepelekwa kwa ajili ya matibabu, wengine wamepelekwa hospitali ya...