Dar es Salaam. Watumiaji magari, mashine na mitambo inayotumia petroli na dizeli watapata ahueni baada ya bei ya bidhaa hizo kupungua, huku bei ya mafuta ya taa ikipanda. Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), jana ilitangaza kushuka kwa bei ya petroli na dizeli kwa asilimia 2.7 na asilimia 3.8; na ongezeko la asilimia 0.09 kwa mafuta ya taa. Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzingagwa Mchany ilisema bei hizo mpya zitatumika Tanzania Bara kuanzia...
Siku tatu baada ya Rais Dkt Magufuli kuipandisha hadhi Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesema kuwa, mtu yeyote atakayekamatwa akitupa takataka hovyo, atakamatwa na kutozwa faini ya TZS 50 milioni, ikiwa ni kwa mujibu wa sheria ndogo za usafi. Mkurugenzi Kunambi ameyasema hayo jana Aprili 29 wakati akizungumza na wafanya usafi ndani ya jiji hilo ambapo alizundua mchakato wa kuwapati kadi za matibabu (bima za afya) ambazo wataweza kuzitumia wao na wategemezi wao...
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa upandaji miti, kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, kushoto ni Mhe. Ferdinand Wambali,Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania. Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akipanda mti wake. Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akipanda mti. Watumishi na Wadau mbalimbali nao walishiriki katika zoezi la kupanda miti. Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza...
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imesema kuwa, kupungua kwa asilimia 19.6 bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2018/19 ikilinganishwa na mwana 2017/18 kunatokana na dhamira ya serikali kutekeleza bajeti hiyo kwa kutumia fedha za ndani ya nchi. Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akijibu hoja mbalimbali zilizoibuka ameeleza kuwa, wabunge walishauri serikali ipunguze utegemezi kutoka kwa wafadhili katika kutekeleza bajeti ya afya. Katika mwaka wa fedha 2017/18, bajeti ya wizara hiyo ilikuwa TZS 1.07 trilioni lakini...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Edmund Bernard Mndolwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB). Uteuzi wa Dkt. Mndolwa umeanza leo tarehe 23 Aprili, 2018. Dkt. Mndolwa anachukua nafasi ya Prof. Lettice Rutashobya ambaye amemaliza muda wake. Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dodoma 23 Aprili, 2018...
Muda huu kupitia TV E unaweza kutazama matangazo ya moja kwa moja ya tukio la kuapishwa kwa Majaji 10, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Naibu Mkurugenzi wa Mashtaka pamoja na Naibu Wakili wa Serikali walioteuliwa na Rais Magufuli hivi karibuni. Tazama kwa kubonyeza PLAY kwenye video ya hapa...
Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, Venance Mobeyo, amemuomba Rais Magufuli aridhie mpambe wa Rais wake, Kanali MN Nkelemi kupangiwa kazi nyingine baada ya kupandishwa cheo kutoka Kanali, kuwa Brigedia Jenerali. Hata hivyo amesema kuwa “Pamoja na upandishwaji vyeo huo nimeomba pia aridhie na amekubali kupandishwa cheo Luteni Kanali DPM Mulunga kuwa Kanali na kwa cheo hicho Mh. Rais ameridhia vilevile ateuliwe kuwa mpambe wa Rais kuanzia leo taratibu zingine za kuwavisha vyeo hivyo zitafanyika kesho Makao Makuu ya Jeshi...
Akithibitisha taarifa hizo mbele ya waandishi wa habari, Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa marehemu amejipiga risasi mdomoni na kutokea nyuma ya kichwa. “Tumepokea taarifa za kifo cha mfanyabiashara ambaye ni mkazi wa wilaya ya Sikonge, ambaye anaitwa Sultan Hemed mmiliki wa mabasi ya HBS leo asubuhi majira ya saa tatu amejipiga risasi nyumbani kwake. Risasi ambayo imeingilia mdomoni na kutokea nyuma ya kichwani,“amesema Kamanda Mutafungwa. Hata hivyo, Kamanda Mutafungwa amesema kuwa jeshi la polisi...
Serikali kupitia kwa Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza imesema kuwa inatambua katika kuhakikisha michezo ikiwepo soka inaimarika nchini, imeendelea kundesha mashindano mbalimbali ya michezo mashuleni kitaifa ikiwepo umiseta na umitashunta. Waziri Shonza ameyasema hayo bungeni akiwa anajibu swali la Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Ramadhani Sima aliyetaka kufahamu mikakati ya Serikali juu kuinua soka la...
Kiungo wa Yanga thabani kamusoko anataka nguvu ya mashabiki wa timu yao siku ya Jumamosi wakati Yanga itakapokuwa inacheza nyumbani dhidi ya Wolaitta Dicha mchezo wa mtoano kuwania nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika. Kamusoko amesema kipindi hiki ambacho timu ipo kwenye wakati mgumu wachezaji wanahitaji zaidi sapoti ya mashabiki kuliko kitu kingine. “Timu inapokuwa haifanyi viruri ndiyo inahitaji sapoti kubwa ya mashabiki kwa hiyo nawaomba mashabiki waje kwa wingi kuisapoti timu yao kwa sababu...