NAIBU balozi wa Uingereza hapa nchini, Matt Sutherland, ameisifu taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kuratibu kambi ya upasuaji wa moyo kwa kushirikiana na madaktari kutoka nje kwa mafanikio makubwa. Pongezi hizo amezitoa leo baada ya kutembelea kambi hiyo maalum iliyoko kwenye taasisi hiyo na kujionea madaktari wakiendelea na kazi ya kuwafanyia upasuaji watoto wa Kitanzania kutoka sehemu mbalimbali nchini. Taasisi ya Muntada Aid, ni taasisi ya Kiislamu yenye makazi yake nchini Uingereza, ambayo ndiyo iliyowezwesha kuwaleta madaktari na...
MAMLAKA ya hali ya hewa Nchini-TMA-imewataka Wakulima na Wafugaji kufuatilia na kutumia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa ili kuongeza ufanisi wa uzalishaji katika kilimo na Ufugaji. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya hali ya hewa Nchini Dokta Ladislaus Chang’a amesema mifugo mingi pamoja na mazao ya kilimo yamekuwa yakiharibika kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa jambo ambalo husababisha upungufu katika uzalishaji hivyo ni muhimu kwa wakulima hao kufuatilia taarifa...
KAMATI Maalumu iliyoundwa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kuandaa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika nchini Oktoba 25 mwaka 2015 imekamilisha Rasimu ya kwanza ya Taarifa hiyo na kuiwasilisha kwa Tume. Akizungumza Katika kikao cha Tume baada ya kupokea Rasimu hiyo ya kwanza, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amepongeza kazi iliyofanywa na Kamati hiyo licha ya majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Tume hiyo kwa sasa. Jaji Lubuva ameeleza kuwa Tume...
WAKATI Leo ni kilele cha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, katibu wa baraza la habari Tanzania MCT-KAJUBI MUKAJANGA amesema kuwa uwepo wa vikwazo mbalimbali katika uhuru wa vyombo vya habari ikiwemo uingiliwaj wa urushwaji wa matangazo ya bunge moja kwa moja unaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa urudishwaji nyuma wa mafanikio yaliopatikana katika tasnia ya habari nchini. Akizungumza na Efm Mukajanga amesema kuwa wadau wa habari wakiwemo waandishi wa Habari na serikali wana kazi kubwa ya kulinda mafanikio yaliopatikana katika...
WAKATI Tanzania Leo ikiungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, imeelezwa kuwa watu takribani milioni 700 duniani wanaishi katika hali ya umasikini uliokithiri. Hayo yameelezwa na ofisa Habari wa ofisi ya ya umoja wa mataifa Tanzania USIA NKOMA wakati akizungumza katika siku ya kwanza ya maadhimisho ya Uhuru mkoani Mwanza. USIA amesema kuwa watu wengi wameendelea kushuhudia kuongezeka kwa ukosefu wa usawa hata baada ya nchi kufaulu kupata wastani wa maendeleo ya kiuchumi....
WAKUU wa Idara zote za Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kuhakikisha wanatoa majina yote ya watumishi hewa ndani ya muda wa siku saba kuanzia leo. Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda wakati akizungumza na wakuu wa idara mbalimbali nchini, maafisa utumishi, wakurugenzi wa wilaya na viongozi wengine. Baada ya kutoa agizo hilo Mheshimiwa makonda amewataka Wakuu wa idara zote za mkoa huo, kusaini Mkataba wa kiapo cha kutojihusisha na suala la...
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu ameziagiza hospitali mbalimbali nchini kuhakikisha zinachukua tahadhari za kuwalinda wafanyakazi wake kitengo cha kumbukumbu katika mazingira ya kupata maambukizi hasa wanapokuwa kazini wakitimiza majukumu yao. Waziri, Mwalimu ametoa maagizo hayo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka wizara hiyo Dkt Mohamed Mohamed alipomwakilisha katika hafla ya kufungwa kwa mkutano wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za...
TANZANIA leo inaungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika Jijini Mwanza Mei tatu. Katika maadhimisho ya Mwaka huu kubwa linalohimizwa na wadau wa Habari nchini ni kuitaka Serikali kuharakisha kupitisha Sheria ya Vymbo vya Habari kwa kuzingatia maoni yanayotokana na mapendekezo ya wadau mbalimbali. Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanaenda sambamba na matukio muhimu matatu ya kihistoria ya kuadhimisha miaka 250 ya Sheria ya kwanza ya uhuru wa Habari...
GWIJI wa Soka la Kimataifa wa Liberia George Weah ametangaza rasmi kuwa atawania nafasi ya urais wa nchi hiyo kwa mara ya pili. Weah, ambaye aliwahi kuchezea klabu za PSG, AC Milan, Chelsea, na Monaco amebainisha kwamba amekuwa na malengo ya kuliletea Taifa hilo mabadiliko, tangu alipoanza kujihusisha na masuala ya kisiasa mara tu baada ya kurejea Liberia mwaka 2003. Rais wa Sasa Johnson Sirleaf anamaliza awamu yake ya pili na ya mwisho katika utawala wake mwaka 2017 ambapo kwa mujibu...
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imetakiwa kurekebisha mtaala wa kutoa mafunzo ya ukunga ili kuifanya taaluma hiyo iweze kuheshimika na kunusuru maisha ya watoto na akina mama wakati wa kujifungua. Wito huo umetolewa na Katibu mkuu wa Chama cha Wakunga Tanzania-TAMA-Dokta. Sebalda Leshabari alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika Semina maalumu iliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo amesema Wizara hiyo inatakiwa kuangalia namana ya kurekebisha mitaala ya utoaji wa mafunzo ya ukunga...
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh. Ally Hapi leo amewatembelea wananchi maeneo ya Bunju na Mbweni waliokuwa na kero mbalimbali. Katika eneo la Bunju Kilungule, baadhi ya wananchi nyumba zao zimezungukwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Akijibu maombi ya wananchi hao, Mheshimiwa, Hapi amewaagiza mainjinia wa manispaa kuhakikisha kuwa wanafanya utaratibu wa kupata pampu kubwa ya kuvuta maji hayo, huku akiwataka wananchi kuwa wale wote waliojenga katika eneo hatarishi ambalo ramani inaonesha kuwa ni eneo...