Local News

NAIBU BALOZI WA UINGEREZA AISIFU TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE
Local News

NAIBU balozi wa Uingereza hapa nchini, Matt Sutherland, ameisifu taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kuratibu kambi ya upasuaji wa moyo kwa kushirikiana na madaktari kutoka nje kwa mafanikio makubwa.  Pongezi hizo amezitoa leo baada ya kutembelea kambi hiyo maalum iliyoko kwenye taasisi hiyo na kujionea madaktari wakiendelea na kazi ya kuwafanyia upasuaji watoto wa Kitanzania kutoka sehemu mbalimbali nchini. Taasisi ya Muntada Aid, ni taasisi ya Kiislamu yenye makazi yake nchini Uingereza, ambayo ndiyo iliyowezwesha kuwaleta madaktari na...

Like
201
0
Tuesday, 03 May 2016
WAKULIMA NA WAFUGAJI WAMETAKIWA KUTUMIA NA KUFUATILIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA
Local News

MAMLAKA ya hali ya hewa Nchini-TMA-imewataka Wakulima na Wafugaji kufuatilia na kutumia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa ili kuongeza ufanisi wa uzalishaji katika kilimo na Ufugaji. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Mkurugenzi wa Utafiti na Matumizi ya hali ya hewa Nchini Dokta Ladislaus Chang’a amesema  mifugo mingi pamoja na mazao ya kilimo yamekuwa yakiharibika kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa jambo ambalo  husababisha upungufu katika uzalishaji hivyo ni muhimu kwa wakulima hao kufuatilia taarifa...

Like
190
0
Tuesday, 03 May 2016
NEC YAKAMILISHA RASIMU YA KWANZA YA TARIFA YA UCHAGUZI MKUU WA OCTOBA 2015
Local News

KAMATI Maalumu iliyoundwa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya kuandaa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika nchini Oktoba 25 mwaka 2015 imekamilisha Rasimu ya kwanza ya Taarifa hiyo na kuiwasilisha kwa Tume.   Akizungumza Katika kikao cha Tume baada ya kupokea Rasimu hiyo ya kwanza, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amepongeza kazi iliyofanywa na Kamati hiyo licha ya majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Tume hiyo kwa sasa.   Jaji Lubuva ameeleza kuwa Tume...

Like
270
0
Tuesday, 03 May 2016
MWANZA: KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI
Local News

WAKATI Leo ni kilele cha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, katibu wa baraza la habari Tanzania MCT-KAJUBI MUKAJANGA  amesema kuwa  uwepo  wa vikwazo mbalimbali katika uhuru wa vyombo vya habari ikiwemo uingiliwaj wa urushwaji wa matangazo ya bunge moja kwa moja unaweza kuchangia  kwa kiasi kikubwa urudishwaji nyuma wa  mafanikio yaliopatikana katika tasnia ya habari nchini. Akizungumza na Efm Mukajanga amesema kuwa wadau wa habari wakiwemo waandishi wa Habari na serikali wana kazi kubwa ya kulinda mafanikio yaliopatikana katika...

Like
254
0
Tuesday, 03 May 2016
TAKRIBANI WATU MILIONI 700 DUNIANI WANAISHI KWENYE UMASIKINI ULIOKITHIRI
Local News

WAKATI Tanzania Leo ikiungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, imeelezwa kuwa watu takribani milioni 700 duniani wanaishi katika hali ya umasikini uliokithiri. Hayo yameelezwa na ofisa Habari wa ofisi ya ya umoja wa mataifa Tanzania USIA NKOMA wakati akizungumza katika siku ya kwanza ya maadhimisho ya Uhuru mkoani Mwanza. USIA amesema kuwa watu wengi wameendelea kushuhudia kuongezeka kwa ukosefu wa usawa hata baada ya nchi kufaulu kupata wastani wa maendeleo ya kiuchumi....

Like
227
0
Monday, 02 May 2016
WAKUU WA IDARA WA MANISPAA ZA JIJI LA DARESALAAM WALA KIAPO KUTAFUTA WATUMISHI HEWA
Local News

WAKUU wa Idara zote za Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kuhakikisha wanatoa majina yote ya watumishi hewa ndani ya muda wa siku saba kuanzia leo. Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda wakati akizungumza na wakuu wa idara mbalimbali nchini, maafisa utumishi, wakurugenzi wa wilaya na viongozi wengine. Baada ya kutoa agizo hilo Mheshimiwa makonda amewataka Wakuu wa idara zote za mkoa huo, kusaini Mkataba wa kiapo cha kutojihusisha na suala la...

Like
324
0
Monday, 02 May 2016
WAHUDUMU KATIKA VITENGO VYA KUMBUKUMBU WAMETAKIWA KUFANYA KAZI KWA TAHADHARI
Local News

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu ameziagiza hospitali mbalimbali nchini kuhakikisha zinachukua tahadhari za kuwalinda wafanyakazi wake kitengo cha kumbukumbu katika mazingira ya kupata maambukizi hasa wanapokuwa kazini wakitimiza majukumu yao.   Waziri, Mwalimu ametoa maagizo hayo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Uhakiki Ubora wa Huduma za Afya kutoka wizara hiyo Dkt Mohamed Mohamed alipomwakilisha katika hafla ya kufungwa kwa mkutano wa Chama cha Maofisa Kumbukumbu na Taarifa za...

Like
212
0
Monday, 02 May 2016
SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI KUADHIMISHWA MWANZA KESHO
Local News

TANZANIA leo inaungana na Mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika Jijini Mwanza Mei tatu. Katika maadhimisho ya Mwaka huu kubwa linalohimizwa na wadau wa Habari nchini ni kuitaka Serikali kuharakisha kupitisha Sheria ya Vymbo vya Habari kwa kuzingatia maoni yanayotokana na mapendekezo ya wadau mbalimbali. Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanaenda sambamba na matukio muhimu matatu ya kihistoria ya kuadhimisha miaka 250 ya Sheria ya kwanza ya uhuru wa Habari...

Like
336
0
Monday, 02 May 2016
LIBERIA: GWIJI LA SOKA, GEORGE WEAH ATANGAZA KUWANIA URAIS KWA MARA YA PILI
Local News

GWIJI wa Soka la Kimataifa wa  Liberia George Weah ametangaza rasmi kuwa atawania nafasi ya urais wa nchi hiyo kwa mara ya pili. Weah, ambaye aliwahi kuchezea klabu za PSG, AC Milan, Chelsea,  na Monaco amebainisha kwamba amekuwa na malengo ya kuliletea Taifa hilo mabadiliko, tangu alipoanza kujihusisha na masuala ya kisiasa mara tu baada ya kurejea Liberia mwaka 2003. Rais wa Sasa Johnson Sirleaf anamaliza awamu yake ya pili na ya mwisho katika utawala wake mwaka  2017  ambapo kwa mujibu...

Like
213
0
Friday, 29 April 2016
TAMA YATAKA MITAALA YA UTOAJI WA MAFUNZO YA UKUNGA KUFANYIWA MAREKEBISHO
Local News

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imetakiwa kurekebisha mtaala wa kutoa mafunzo ya ukunga ili kuifanya taaluma hiyo iweze kuheshimika na kunusuru maisha ya watoto na akina mama wakati wa kujifungua. Wito huo umetolewa na Katibu mkuu wa Chama cha Wakunga Tanzania-TAMA-Dokta. Sebalda Leshabari alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika Semina maalumu iliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo amesema Wizara hiyo inatakiwa kuangalia namana ya kurekebisha mitaala ya utoaji wa mafunzo ya ukunga...

Like
217
0
Friday, 29 April 2016
MKUU WA WILAYA YA KINONDONI ATEMBELEA WANANCHI BUNJU
Local News

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam Mh. Ally Hapi leo amewatembelea wananchi maeneo ya Bunju na Mbweni waliokuwa na kero mbalimbali. Katika eneo la Bunju Kilungule, baadhi ya wananchi nyumba zao zimezungukwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.  Akijibu maombi ya wananchi hao, Mheshimiwa, Hapi amewaagiza mainjinia wa manispaa kuhakikisha kuwa wanafanya utaratibu wa kupata pampu kubwa ya kuvuta maji hayo, huku akiwataka wananchi kuwa wale wote waliojenga  katika eneo hatarishi ambalo ramani inaonesha kuwa ni eneo...

Like
292
0
Thursday, 28 April 2016