VYOMBO vya habari nchini vimetakiwa kuandaa vipindi vya kuelimisha na kupunguza burudani kwa kuongeza idadi ya vipindi vya kujenga uzalendo, amani, mshikamano pamoja na umoja wa kitaifa. Rai hiyo imetolewa na Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Kanda ya Ziwa Enjinia. Lawi Odieri wakati wa ziara ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia Mkoani Simiyu. Naye mheshimiwa Nauye amesema kuwa uwepo wa vituo vya kutosha vya utangazaji katika...
SERIKALI imeagiza kila mkoa na kila Halmashauri nchini kuajiri Maafisa wa Habari na kuwapa nafasi ya kushiriki katika vikao vyote vya maamuzi pamoja na kutenga bajeti kwa ajili ya shughuli za maafisa habari ili kuboresha mawasiliano ndani ya serikali na mawasiliano ya serikali na umma. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Sanaa, Nape Nauye, wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani Kigoma, aliyoifanya kwa ajili ya kutembelea idara zilizo chini ya wizara yake ambapo...
MTU mmoja anasadikiwa kufariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa mara baada ya kuangukiwa na kufunikwa na kifusi katika chumba kimoja maeneo ya Kawe Ukwamani, jijini Dar es salaam . Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kawe Ukwamani SULTANI JETA amesema mnamo alfajiri ya leo kulisikika mshindo ambao ulitokana na ukuta kudondoka na kuwafunika watu wan ne wa familia moja wakiwepo watoto wawili ,mtu mzima mmoja na msichana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na mbili ambao wote...
WANAWAKE nchini wametakiwa kuacha tabia ya kuwa tegemezi na badala yake wajishughulishe ili kujikwamua kiuchumi na kuepukana na ukatili wa kijinsia unaowakabili baadhi ya wanawake. Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Lilian Lihundi wakati alipokuwa akizungumza na kituo hiki juu ya upingaji wa ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Amesema kuwa katika uchunguzi uliofanywa na mtandao huo umebaini kuwa kwa asilimia kubwa ukatili wa kijinsia unawakabili wanawake ambao hawajawezeshwa...
JESHI la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limefanikiwa kukamata pikipiki 519 ambazo zimekuwa zikitelekezwa kutokana na makosa mbalimbali ya barbarani kutoka katika manispaa tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo kamanda wa kanda maalumu ya mkoa huo kamishina Simon Sirro amesema katika kuhakikisha wanapambana na uhalifu mbalimbali ikiwemo wa kutumia pikipiki jeshi hilo limefanikiwa kuzuia pikipiki nyingi ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikitelekezwa na baadhi ya watuhumiwa....
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali ipo katika hatua za mwisho kuanza mradi wa ujenzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda yenye urefu wa Km. 356 kwa kiwango cha lami ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Awamu ya Tano aliyoitoa kwa wananchi wa Mikoa ya Katavi na Tabora. Ametoa kauli hiyo wilayani Sikonge mkoani Tabora, mara baada ya kukagua barabara hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amesema ujenzi huo unatarajia kuanza rasmi hivi karibuni....
CHAMA kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar CUF leo kinatarajiwa kutangaza mikakati yake na msimamo kuhusiana na mzozo wa kisiasa wa Zanzibar. Hata hivyo msimamo huo unatarajiwa kuzungumzia mufaka kati ya chama cha CUF na CCM ambao ulileta uundwaji wa serikali kati ya vyama hivyo viwili. Hivi karibuni shirika la misaada la Marekani MCC lilisitisha msaada wa dola 487 kwa madai ya kutoridhishwa na hali ya kisiasa visiwani...
MKUU wa mkoa wa Dar es salaamu mheshimiwa PAUL MAKONDA amewataka madereva wa boda boda mkoa huo kuhakikisha wanaunda kamati ya muda ya uongozi yenye watu 13 kwa ajili ya kusaidia kurahisha mahusiano kati ya serikali na boda boda. Mheshiwa MAKONDA ameongeza kuwa yeye kama mkuu wa mkoa atasimamia vizuri mgawanyo wa pesa za vijana ambazo hutolewa kwa kila hamashauri kwa asilimia 10 na pia yupo tayari kuwadhamini vijana wote ambao wanajishughulisha na biashara ya boda boda katika kuchukua mikopo...
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye leo amezindua rasmi kamati ya maudhui ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA itakayoangalia maudhui bora ya utangazaji wa vipindi na matangazo katika vyombo vya habari nchini. Aidha, ameitaka taka kamati hiyo kuangalia suala la baadhi ya Watu kushikilia masafa mengi bila ya kutumia pamoja na kuhakikisha kuwa wanasimamia vizuri kanuni za utangazaji ziweze kufuatwa na kuheshimiwa ipasavyo. Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya udhamini ya Mamlaka ya...
IMEBAINIKA kuwa asilimia kubwa ya watoto wanaotumiwa na watu wenye ulemavu kwa ajili ya kuomba fedha barabarani wanashindwa kuhudhuria masomo kutokana na kutumia muda mwingi kwa kazi hiyo. Akizungumza na EFM mwanaharakati wa masuala ya watu wenye ulemavu, Jonathan Haule amesema kuwa watoto hao wamekuwa wakitembea barabarani nyakati za masomo. Amesema kuwa ni vyema serikali ikaanzisha mifumo madhubuti itakayowawezesha watu wenye ulemavu kufanya kazi zao pasipo kutegemea...
SERIKALI imeliagiza Shirika la Reli Tanzania (TRL), kupitia upya mikataba ya ununuzi wa vichwa vya treni na mabehewa ili kubaini kasoro zilizojitokeza na kuchukua hatua stahiki kabla ya maboresho ya reli ya Tanga-Moshi na Arusha. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa agizo hilo mkoani Kigoma wakati akikagua miundombinu ya reli na kusissitiza nia ya serikali kufufua reli ya kanda ya kaskazini ili kuimarisha huduma ya uchukuzi katika mikoa hiyo. Prof. Mbarawa amesema Serikali imedhamiria...