WAKATI Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini-NEC-ikiendelea na Zoezi la kuhesabu kura, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi-UKAWA- vimeendelea kupinga Matokeo na kuiomba Tume hiyo kusitisha zoezi hilo kwa madai kuwa zoezi hilo halitendi haki kwa vyama vya upinzani. Hayo yamebainishwa leo na Mgombea wa nafasi ya Uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaeungwa mkono na –UKAWA- Edward Lowasa wakati akizungumz na Waandishi wa habari ambapo amesema ni vyema Tume kuanza upya zoezi hilo kwa kutumia karatasi zilizosainiwa...
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Salim Jecha Salim ametangaza kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi visiwani humo kwa kudai kuwa uchaguzi huo ulijaa kasoro nyingi. Akizungumza kupitia Televisheni ya serikali ya Visiwani Zanzibar-ZBC-Jecha amesema kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki na kwamba kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria za uchaguzi. Aidha amesema kuwa ukiukwaji huo umetokana na baadhi ya makamishna wa Tume hiyo, kutotekeleza majukumu yao kama inavyotakiwa...
JUMLA ya watahiniwa 12,011 wa kidato cha nne Jijini Mbeya wanatarajiwa kuanza mtihani wa Taifa Novemba mbili mwaka huu, ikilinganishwa na wanafunzi 2,895 waliofanya mtihani huo mwaka jana. Hayo yamesemwa na Afisa habari wa halmashauri ya jiji la Mbeya kwa niaba ya Afisa Elimu sekondari Jaquline Msuya amesema kati ya watahiniwa hao wasichana ni 6373 na wavulana 5638. Kwa upande wake mkuu wa shule ya Sekondari ya Southern Highland ya jijini Mbeya Chamila Evarist amesema wamejiandaa vyema kuhakikisha wanafunzi wote...
TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini-NEC-imewataka wananchi kutopotoshwa na maneno ya wanasiasa juu ya matokeo ya nafasi ya Urais yanayotolewa na Tume hiyo kuwa yana upendeleo suala ambalo halina ukweli wowote. Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam leo kabla ya kuanza kutangaza matokeo, mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa Tume inatangaza matokeo kwa mujibu wa taratibu na namna yanavyoifikia. Mbali na hayo Jaji Mstaafu Lubuva ameviasa vyama vya siasa kutoendelea kuwapotosha watanzania kwani...
KUFUATIA uwepo wa mitazamo tofauti kwa tume ya Taifa ya uchaguzi kuhusu kupendelea upande mmoja wakati wa utangazaji wa matokeo, Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema Tume inafanya kazi zake kwa mujibu wa utaratibu iliyojiwekea na sio kwa matakwa ya mtu binafsi. Aidha Jaji mstaafu Lubuva amesema kuwa matokeo ya ngazi ya urais kutoka majimbo ya uchaguzi kote nchni hutangazwa kwa wananchi kwa kadiri yanavyo pokelewa na sio vinginevyo. Hata hivyo amesema kuwa hali hiyo imesababishwa na ucheleweshwaji...
WAANGALIZI wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC leo wametoa ripoti ya awali kuhusu Zoezi la uchaguzi linavyoendelea tangu kuanza kwa zoezi hilo la uchaguzi na kusema kuwa zoezi hilo limemalizika vizuri katika maeneo mengi ya nchi. Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es salaam Kiongozi wa Timu ya Waangalizi kutoka EAC Mheshimiwa Arthur Moody Awori amesema kuwa kwa mara ya kwanza uchaguzi wa mwaka huu umekuwa wa ushindani mkubwa uliobebwa na mabishano bila ya kuwepo na vurugu zozote. Aidha...
PAKUA MATOKE HAPA 1445940504-MATOKEO RASMI YA WAGOMBEA URAIS TANZANIA MAJIMBO...
ASASI isiyo ya kiserikali ya AGENDA imetoa wito kwa serikali na wadau wengine kuelimisha jamii juu ya madhara ya madini ya risasi na jinsi ya kuyaepuka kwani yanaathari kubwa kwa watoto na mama wajawazito. Akizungumza na waandfishi wa habari jijini Dar es salaam katibu mtendaji wa Asasi hiyo Silvani Mng’anya amesema kuwa katika wiki ya kukuza uelewa kwa jamii kuhusu athari za madini ya risasi wananchi wanatakiwa kujua kuwa madini hayo yanaathiri mfumo wa mwili wa binadamu ikiwemo ubongo, moyo...
TUME ya Taifa ya Uchaguzi-NEC-imeendelea kutoa matokeo kwa ngazi ya Urais kutoka majimbo mbalimbali yaliyokamilisha Zoezi la kuhesabu kura zilizopigwa katika Uchaguzi mkuu uliofanyika oktoba 25 mwaka huu. Awali akizungumza kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo leo katika ukumbi wa mikutano wa mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva amewataka wananchi kuondoa wasiwasi kwani Tume imejipanga vyema kuhakikisha kila matokeo yanayopatikana inayatangaza. Leo ni siku ya pili tangu kukamilika kwa Zoezi la...
KUFUATIA kukamilika kwa zoezi la upigaji kura katika maeneo mengi nchini baadhi ya vituo vimeendelea kuhesabu kura ingawa kuna ushindani mkubwa kwa wagombea wa vyama mbalimbali. Mbali na hayo hali ya usalama imeonesha kuimarishwa kwa kiwango kikubwa hali inayowawezesha wananchi kuendelea na shughuli za kawaida huku wakisubiri matokeo. Hata hivyo baadhi ya vituo vya kupigia kura vimeanza kutoa matokeo ya awali ya ngazi za Udiwani, Ubunge na Urais ingawa zimejitokeza changamoto mbalimbali wakati wa kupiga na kuhesabu...
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joel Laurent kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA). Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu Jijini Dar es salaam inaeleza kwamba Uteuzi wa Mkurugenzi huyo ulianza tangu Oktoba 18, mwaka huu. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Laurent alikuwa Katibu wa Taasisi ya TEA na ndiye aliyekuwa anakaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu kwa muda...